Anataka mtoto na mimi

Jaruk

Member
May 7, 2020
44
42
Nina mpenzi tumependana vya kutosha yeye ni single mother na mimi nina ndoa na watoto. Alinishauri niishi naye nikazugazuga alivyoona hivyo akaniomba kuwa anataka mtoto na mimi. Nifanyage japo na mimi nimempenda Kiana tatizo ndoa yangu
 
Keep away from children.

Kuna jamaa aliingia kingi kama wewe, single mother mwenye watoto 3 alimwambia jamaa anaomba amzalishe mtoto ili spate mtoto mweupe.

Jamaa ni white flani na huyo Dada ni white kidogo ila bwana ake aliyezaa nae hao watoto ni black na watoto ni black.

Jamaa alizingua baadae akakubali yaliyotokea..1......2.....3....4...5 Now wanawatoto watatu wote wakiume na wanaendelea na maisha.

Huo ni mtego kuja kushtuka umeozeshwa / kuoa bila kutarajia. Usikubali au ukubali kwa matakwa yako
 
Ukimpachika mtoto tu,jiandae kubeba majukumu....mara leo mtoto anaumwa,mara leo chakula kimeisha n.k kama uko vizuri,mpatie mtoto uumpe na shughuli ya kufanya ili asiwe anakusumbua sumbua huko mbeleni.
 
Vp kipato chako kinaruhusu kuhudumia wake wawili na idadi hiyo ya watoto? Maana hapo kuna mtego unawekwa ili unase na kumpunguzia mzigo wa kulea watoto na maisha huyo single mother.Kiufupi? Naona umeshatekwa kiakili na hisia,umekuwa mpofu katika maamuzi na kuiona/ kuifikiri kesho yako katika ndoa yako na maisha!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah!..kwa hiyo mkuu huogopi kuharibu ndoa yako na familia yako kisa huyo mpitaji.
 
Kama unampenda mkeo kwa dhati please achana na huyo mwanamke.Ninakushauri hivyo kwasababu Sasa hivi yeye kashika makali na ww umeshika mpini.Akijifungua tu itageuka maana kwake utakuwa umejiwekea alama ya kudumu.Atajirasmisha yeye hata Kama ww hujafanya awe rasmi.Jiandae kupafahamu ustawi wa jamii na baadaye mahakama ya Kisutu akidai matunzo ili tu akuvuruge na familia yako.Leo hii atakwambia ntalea mwenyewe,akishazaa anaanza ooh watoto wako unawapeleka mlimani City kucheza wangu apelekwe na Nani? Yaani Visa vingi ikiwemo kupigiwa simu usiku eti mtoto analia sijui anachemka.Shemeji please Kama umevaa viatu via,kunja suruali kimbiaaa kwa speed ya kipunani...sijui wa Kenya.Achana na akili ya mwanamke...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom