Ulimbo
JF-Expert Member
- Aug 14, 2009
- 3,766
- 4,048
Wazee Weekend Kareem.
Kuna kijana wa makamo, ana kama 40 years hivi, anataka kuoa, lakini hana mahari.
Alikuwa anafanya kazi kwenye magesi huko Mtwara, alipoingia bwana Mkubwa kampuni yao ikafungiwa kuendelea na kazi nchini TZ.
Jamaa hadi Leo hawajalipwa NSSF na hajapata kazi hadi Leo, kapigika kichizi.
Sasa tunamsaidiaje, kaja kuniomba mawazo nimemwambia Naomba masaa mawili Ntakuja na majibu
Kwani shida iko wapi?
Kwani kazi na mahari ndivyo vinataka kuoa au yeye ndiye anataka kuoa.
Mimi namshauri oaoe tu, hivyo vitu vingine sijui kazi na mahari vitakuja tu. Ni vizuri afanye kile kilichopo ndani ya uwezo wake.