Anataka kumuua anayetembea na mkewe, ushauri !!!

Anataka kumuua anayetembea na mkewe, ushauri !!!

Nndu wa Selote

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2012
Posts
733
Reaction score
521
Ni jamaa yangu, kanipigia simu kaniita bar. Nilipofika kanieleza yaliyoko moyoni.

Miaka kama minne nyuma aligundua kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na jamaa mmoja. Akaendelea kuchunguza akagundua ni kweli akamuonya mkewe. Siku moja akiwa safarini kwenye basi, akampigia mkewe na kisha akampigia jamaa akagundua kuwa wako pamoja. Akamuonya mkewe na badaye akamtumia jamaa message kali. Aliporudi safari ugomvi ukawa mkali kati yake na mkewe huku mkewe akiwa anakataa kuwa na mahusiano na huyo bwana. Lakini alipochukua simu ya mkewe na kuichunguza, akagundua ile message aliyomtumia jamaa iko kwenye simu ya mkewe, yaani alimforwadia.Alipomwuliza mkewe hiyo msg ya jamaa imefikaje kweye simu yake akabaki kujikanyanga.

Juzi hapa, jamaa yangu amegundua mahusiano ya wawili hao yanaendelea kama kawaida. Ameamua kumfuatilia mwizi wake kimya kimya na kugundua anakoishi, kazi zake, nyendo zake zote na vijiwe vyake. Tayari ameshafanya utaratibu wa kumdelete na anasubiri utekelezaji tu. Mimi kanishirikisha kama taarifa tu kwa sababu maamuzi anayotaka kuchukua ni magumu. Namnukuu:
"Kiukweli huyu bwana nilimtumia message ya kumuonya, kwa dharau akaiforward kwa mke wangu, Nimeshamfuatilia, anaitwa Deodatus----, picha yake hii hapa (akanionyesha picha), na namba yake ya simu ni 0754 275170 na anaishi.....(akataja mtaa na nyumba)"

Ndugu wana JF Jamaa yangu yuko serious nimeona nililete hapa kwa maoni zaidi!!! Nawasilisha!
 
Uamuzi anaotaka kufanya si mzuri, mshauri aachane nao kabisa. Hao ni watu wazima na muhimu WAMEKUBALIANA. Atafute chanzo kwa nini mke wake anamkubali huyo bwana, pili akiona haridhiki atengane naye kwa muda kila mtu atafakari mustakabali wa ndoa yao. Mara nyingi hili la kutengana kwanza huwa ndiyo suluhisho. Hakuna Mwanmme anyaetaka mizigo.
 
Mapenzi haya pasua kichwa jamani waliooa walioa zamani tu.
 
Mke wa mtu sumu........ atakojoa dagaa...
 
Hapa tatizo mke si mwaminifu, thats all.
Binafsi huwa siungi mkono mambo kama haya lakini nimejikuta najiuulza maswali mengi ya KIPUUZI kama ifuatavyo: Mbona kuna njia nyingi mbadala za kufanya badala ya kuua ina maana hazifahamu?
Kumuua mtu kutamsaidia nini? Akimuua huyo na mkewe kuanza mahusiano na mwingine, naye pia atamuua? Kwanini kuingia dhambi ya kutoa uhai wa mtu kwa kosa la uaminifu wa mkewe? Kwanini kujikuta unatupwa jela na kupoteza au kuharibu future yako na ya watoto wako kwa uzembe tu wa kutokufikiria sawa sawa? Hivi ina maana wanawake wameisha? Kwani ni lazima aendelee naye huyo huyo mkewe?
 
Mbona anataka kununua jela kwa pesa? ivi kweli unawacha kazi zako kumfatilia mtu kisa amekuchukulia mke? Mwambie jamaa yako kweli sio rahis na inauma lakini kwanini asimalize hili tatizo na mkewe na kama wameshindana tabia basi amuache,yani aumize kichwa kutafuta pesa na akirudi nyumbani pia amani hamna, amalizane na mkewe na huyo mwanamme sio mgonvi wake, ntaelewa kama atapoteza mda kutafuta pesa na ntamuona mwanamme wa mana kuliko maamuzi anayo fikria,sababu mwizi daima atakua mwizi leo akishamuua huyo,,mkewe anaupupu unamuwasha atamaliza kuua..
 
Wanawake wengine wanashangaza sana kwa nini wanakubali kuolewa kama wanajua hawawezi kukaa na mme mmoja heri wangekaa bila kuolewa ili wawe na uhuru wa kufanya watakavyo kuliko kuwatesa waume wao,ndo haohao kazi yao kuwapiga vijembe wasio olewa mara hataolewa huyu ni malaya...chagueni moja kuwa malaya muachane na ndoa au kulinda ndoa zenu.Chagueni leo mtakaye mtumikia.
 
He should walk away ...Miaka 4!

I feel his pain na kinachomsumbua ni kutojikubali.

Nashauri akubaliane na amwachie jamaa tu. Ni ngumu lakini ni ukweli
 
Mshauri adeal zaidi na mke wake kujua sababu hasa zinazomfanya atoke nje ya ndoa,kuua si sawa na itamgharimu sana tu kwa vile damu ya mtu huwa haiendi bure.
 
Binafsi hilo la jamaa kutaka kuua sishangai maana mke anauma jamani,afu unakuta unamgharimia kwa kila kitu akiumwa anavodeka kidume unavumilia tu,at the end of the day mtu anafyatua anavotaka !!!
Ila ameniudhi jinsi anavotaka kumaliza, jina namba za simu za nini !!
HAKIKA HUYU SIO JASIRI .
 
Kama ni tabia ya mkewe ataua wengi.
Inanikumbusha kisa cha jamaa mmoja aliyemfumania mkewe mara kadhaa.

Alimuonya mkewe lkn likawa sikio la kufa.
Siku ya siku alipomfumania tena akamuua mkewe. Yule jamaa aliyekuwa na mke wa mshikaji akabaki na mshangao akiamini adhabu hiyo ilikuwa yake.

Alipomuuliza mwenye mke akajibu, "kwa style ya mke wangu, bora nihukumiwe kwa damu ya mmoja kuliko kuua kila wakati ndo mana nimemuondoa atayesababisha mi niue wengi".
 
Rafiki yako ana mkataba (ndoa) na mkewe na si hawara wa mkewe! Kama ana hasira anatakiwa kuzionesha kwa mkewe. Vyovyote itakavyokuwa hapo raha ya mke haipo tena....,

Ni bora kuachana na mke na kutafuta mwingine au kwa kuwa ukiumwa na nyoka......, aache mke na abaki kama alivyo na amtumike MUNGU wake wa ukamilifu maana atakuwa hana nira na mtu yeyote....
 
chizi huyo...ukamuue jamaa baada ya uzembe wako...yeye amle kabang mke wake tuu.
 
Back
Top Bottom