Anataka kumuua anayetembea na mkewe, ushauri !!!

Anataka kumuua anayetembea na mkewe, ushauri !!!

Dah....!

mimi mwenyewe nipo ndani ya ndoa ila kuna kaka nampenda saaaaana, na tumekuta toka niko na mume wangu kama wachumba, na kweli tunapendana... kwa hiyo katika maisha mambo hayo yapo, sema unakula kwa step usijiachie, na kila siku nikujikumbusha kwamba upo ndani ya ndoo, so mipaka muhimu, kwa mfano muwe na mida ya kuwasiliana na msg katika simu hazikubaliki.... ukienda ivyo utadumu sana na wapembeni...
 
Aende kwa mganga tu amroge uume uhamie kwenye pua

Amroge ili jamaa ashike mimba na azae baada ya miezi 24 tena hicho kitakachozaliwa kitokee kwenye 071... afe awe nungunungu
 
Ni jamaa yangu, kanipigia simu kaniita bar. Nilipofika kanieleza yaliyoko moyoni.

Miaka kama minne nyuma aligundua kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na jamaa mmoja. Akaendelea kuchunguza akagundua ni kweli akamuonya mkewe. Siku moja akiwa safarini kwenye basi, akampigia mkewe na kisha akampigia jamaa akagundua kuwa wako pamoja. Akamuonya mkewe na badaye akamtumia jamaa message kali. Aliporudi safari ugomvi ukawa mkali kati yake na mkewe huku mkewe akiwa anakataa kuwa na mahusiano na huyo bwana. Lakini alipochukua simu ya mkewe na kuichunguza, akagundua ile message aliyomtumia jamaa iko kwenye simu ya mkewe, yaani alimforwadia.Alipomwuliza mkewe hiyo msg ya jamaa imefikaje kweye simu yake akabaki kujikanyanga.

Juzi hapa, jamaa yangu amegundua mahusiano ya wawili hao yanaendelea kama kawaida. Ameamua kumfuatilia mwizi wake kimya kimya na kugundua anakoishi, kazi zake, nyendo zake zote na vijiwe vyake. Tayari ameshafanya utaratibu wa kumdelete na anasubiri utekelezaji tu. Mimi kanishirikisha kama taarifa tu kwa sababu maamuzi anayotaka kuchukua ni magumu. Namnukuu:
"Kiukweli huyu bwana nilimtumia message ya kumuonya, kwa dharau akaiforward kwa mke wangu, Nimeshamfuatilia, anaitwa Deodatus----, picha yake hii hapa (akanionyesha picha), na namba yake ya simu ni 0754 275170 na anaishi.....(akataja mtaa na nyumba)"

Ndugu wana JF Jamaa yangu yuko serious nimeona nililete hapa kwa maoni zaidi!!! Nawasilisha!

Mkuu kwa ushahidi huuu wa namba ya mtu umetoa hapa akipatikana na janga lolote wewe utakuwa shahidi namba moja!! Na ukicheza wanakuweka selo maana ungetakiwa uripoti crime polisi! Imekula kwako. Omba Mungu yaishe kwa amani.
 
Mke kama haelewi somo jamaa si apige chini tu, nawe ushakuwa proxy kwenye hii kitu maana umetoa mpaka namba ya simu, so mweleweshe jamaa yako km vp abwage manyanga tu asijejuta
 
Ni jamaa yangu, kanipigia simu kaniita bar. Nilipofika kanieleza yaliyoko moyoni.

Miaka kama minne nyuma aligundua kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na jamaa mmoja. Akaendelea kuchunguza akagundua ni kweli akamuonya mkewe. Siku moja akiwa safarini kwenye basi, akampigia mkewe na kisha akampigia jamaa akagundua kuwa wako pamoja. Akamuonya mkewe na badaye akamtumia jamaa message kali. Aliporudi safari ugomvi ukawa mkali kati yake na mkewe huku mkewe akiwa anakataa kuwa na mahusiano na huyo bwana. Lakini alipochukua simu ya mkewe na kuichunguza, akagundua ile message aliyomtumia jamaa iko kwenye simu ya mkewe, yaani alimforwadia.Alipomwuliza mkewe hiyo msg ya jamaa imefikaje kweye simu yake akabaki kujikanyanga.

Juzi hapa, jamaa yangu amegundua mahusiano ya wawili hao yanaendelea kama kawaida. Ameamua kumfuatilia mwizi wake kimya kimya na kugundua anakoishi, kazi zake, nyendo zake zote na vijiwe vyake. Tayari ameshafanya utaratibu wa kumdelete na anasubiri utekelezaji tu. Mimi kanishirikisha kama taarifa tu kwa sababu maamuzi anayotaka kuchukua ni magumu. Namnukuu:
"Kiukweli huyu bwana nilimtumia message ya kumuonya, kwa dharau akaiforward kwa mke wangu, Nimeshamfuatilia, anaitwa Deodatus----, picha yake hii hapa (akanionyesha picha), na namba yake ya simu ni 0754 275170 na anaishi.....(akataja mtaa na nyumba)"

Ndugu wana JF Jamaa yangu yuko serious nimeona nililete hapa kwa maoni zaidi!!! Nawasilisha!
mwanamke huo hajatulia,aachane naye ndo suluisho.
 
Swali zuri, gumu na lenye kuelimisha sana.

(1) Kwa vile una taarifa ya kusudio la mtu kufanya kosa la jinai; una lazimika kutoa taarifa polisi. Ikujulikana kuwa ulikuwa na taarifa halafu hukutoa taarifa polisi unaweza kujikuta unaunganishwa kwenye kesi kama accomplice.

(2) Kisheria rafiki yako anaweza kufanya mauaji hayo na akatoka huru iwapo atamfumania jamaa red-handed akiwa anammegea mkewe na kumwua on the spot. Kuna vifungu vya sheraia anavyoweza kutumia kujitetea na mambo yakaisha. Lakini kwenda kutafuta background information na kupanga mauaji ni kosa la jinai, na iwapo atalitekeleza kwa mkono wake, basi ajue adhabu yake ni kwa yeye mwenyewe kunyongwa hadi afe. Na iwapo atalitekeleza kwa kuajri watu wengine wafanye hivyo, bado atakuwa na kosa la kushiriki na kutekeleza njama za mauaji, jambo ambalo linaweza kumtupa jela kwa miaka karibu 20.

(3) Siku njema huonekana asubuhi. Iwapo mke wake amekuwa anatemebea na mwanamme mwingine ndani ya ndoa kwa miaka minne, ajue kuwa huyo mwanamke hampendi kama mme bali labda yuko pale kwa ajili ya economic protection tu. Alitakiwa awe amejua hilo miaka minne iliyopita na kuachana na ndoa hiyo. Iwapo alisubiri muda weote huo na huenda kuwa amepata watoto basi atakuwa alifanya makosa sana. Ushahidi wa message za huko nyuma zilitosha kudissolve ndoa yao akatafuta mke atakayempenda ki-ukweli.

(4) Kutoka kwa yule anayewindwa tunapata somo kubwa sana hasa kwa vijana wa siku hizi. Kutembea na mke wa mwenzio ni kosa linaloweza kukupotezea uhai wako. Hata kama mmwanamke ni mzuri kiasi gani, na unamzimia sana, epuka kutembea na mke wa mtu ili upate baraka na ujiepushe na balaa. Wanaume hujisikia vibaya sana wanapomegewa na wake zao na wengine wao huweza kufanya maamuzi ambayo huenda yakaondoa uhai wako kama ambavyo jamaa huyu anapanga.

(5) Jamii nyingi za kistaarabu duniani haziruhusu mtu kutembea na mke wa mtu mwingine, na ni utamaduni ulioko hata katika vitabu vitakatifu kwenye Exodus. Unapotembea na mke wa mtu mwingine, siyo kuwa unafanya maudhi kwa mwenye mke tu, bali unakuwa umeudhi jamii nzima, hasa ya walio katika maisha ya ndoa. Unfortunately, mambo hayo yanpotekea yule mwanamke huwa halaumiwi sana bali ni mwanmme ndiye hubeba lawama zote, na hiyo ni natural. Kwa hiyo iwapo utatembea na mke wa mtu bila kujua, jitahidi ujitokeze mbele ya jamii uombe radhi na hasa iwapo ulikuwa hujui kuwa yule mama kaolewa. Na kama ulikuwa unajua, tafuta sababu ya msingi kuonyesha kuwa unajajutia ulilofanya na hutafanya tena. Kujiondokea kimya kimya kama vile huoni tatizo kwa wewe kummega mke wa mwenzio au kuendelea kumega licha ya maonyo unayopewa si njia nzuri na mambo yanaweza kugeuka kuwa mabaya sana dhidi yako; ama directly kutoka kwa uliyemmegea au kutoka kwa watu wengine ndani ya jamii.

Hili linaingia moja kwa moja katika tukio la aina hiyo la wiki tatu zilizopita kuhusu Diamond kummega Uwoya, halafu Ndikumana kuzirai baada kusikia kamegewa, na baada ya hapo Diamond kutojali kabisa na wala kutoongelea kabisa tukio hilo. Nadhani Diamond hakupata mshauri mzuri sana wa ku-handle situation ile hasa kwa vile inahusu celebrities; kimsingi alitakiwa atamke mara moja kujutia tukio hilo na hasa aonyeshe kuwa hakujua Irene alikuwa bado ndani ya ndoa yake na Ndikumana, kisha akaomba radhi kwa Ndikumana na jamii yote kwa yaliyotokea, akimalizia na kukemea vitendo vya ngono nje ya ndoa.

Naona umeamua ushushe desa la criminal law first year..kitu fragrante delicto ni ngumu..!!kama vp aache mke huyo !!maana hata bible inasema mwanamke mpunbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake
 
Anachodhamiria kufanya kitamcost maisha yake yote. Dawa ya mtu anaecheat ni kuachana nae kila mmoja awe huru. Hakuna mwenye haki ya kutoa uhai wa mwenzake hapa duniani. Huyo jamaa hana kosa sababu mkewe ndiye alieruhusu hayo mahusiano kama angesema no pengine kungekua na kesi ya ubakaji. So ushauri wangu asiue , maisha ni zaidi ya hapo bwana kuwa na mtu asie mwaminifu sio mwisho wa dunia cha msingi waseparate ndio maana kuna talaka. Akumbuke kuwa hayo yanayomkuta yeye sio wa kwanza na hatakua wa mwisho so akae na mkewe wajadili hatma ya ndoa yao na ikibidi wamuite mgoni wao ili huyo mama achague anamtaka yupi au kama vipi huyo mbaba amfungashe mkewe na kumkabidhi mgoni wake. Na akitaka kumkera zaidi mkewe amuombe awapangie zamue ie iwe ya siku ngapi ngapi ili kila mmoja awe na amani aone mkewe atakavyoreact.
 
Huyu jamaa angekuwa na nia ya kuua wala asingekwambia.

Sema anataka umfikishie habari huyu bwana ili aache kula mkewe.
 
Back
Top Bottom