Anataka kufahamu faida ninayoingiza kwenye biashara yangu. Kaninunia baada ya kumwambia tupige na mshahara

Inawezekana ile namna ulivyomwambia mkimaliza mahesabu yako muhamie yake ndio imemkera...labda sio kwa namna ya upole na kistarabu

Wanaume wanapenda kubembelezwa/kuelekezwa kwa zile sauti romantic/kiupole fulani hivi
Haya material uliyomwaga hapa unaweza ukatunukiwa PhD ya ubanguzi wa korosho. Ni wewe umeandika au umemnukuu mama Maria Nyerere?
 
Mimi hata Nile mwanamke meneja wa nssf ,mavazi yake ,saloon ,marembo kula yake na mafuta ya gari juu yangu ,unajiskiaje mwanamke kuvaa nguo usizojua aliemnunulia ,nadhani Nina tatizo la mfumo dime ,hela ya make ni sumu
 
ndoa nyingi za kisasa watu wanafunga ndoa kwa kuridhisha wanaowazunguka ila hawana chemistry.. wanawake wanakomalia ndoa wakiona mwanaume mambo safi au mzuri au ana kazi nzuri bila kujua tabia yake ilivyo.. wanaume nao wanafunga ndoa hivyo hivyo kwa kuangalia vigezo hasa kazi nzuri au biashara ya mwanake, au uzuri bila kusomana au kukubaliana wataishije..

ndoa zisizo na mgogora sana zama hizi ni za watu wenye asili moja.. kama mhaya na mhaya mwenzake,,mchaga mmarangu akiolewa na mchaga mmarangu mwenzake. mnyaki na mnyaki mwenzake angalau zinadumu dumu...

Mhh This is interesting...NDOA ndoa kabisa!

Ila hapo tuangalie HISTORIA:

Kabla ya NDOA yenu naamini mlikuwa na kipindi cha urafiki/uchumba,

- je, wakati huo alikuwa akikuhudumia kwa lolote? (mf. nguo, zawadi zawadi, nk)

- je, mliwahi kuzungumzia mapato yenu na jinsi gani mtaishi iwapo mkioana? Kama ndiyo, mlikubalianaje na makubaliano hayo yana tofauti gani na mnavyoishi sasa

- je, kuna mambo/miradi ambayo mnaendelea nayo na yeye ndiyo anasimamia peke yake?


Twende kwenye jambo lingine..COMMUNICATION:

Kuna wadau wawili watatu wamezungumzia lugha/tone ya mawasiliano. Kihalisia WANAUME ni viumbe wenye EGO. Ni kweli, kuna baadhi wamepata busara ya kutambua udhaifu wao huo na hata mwanamke amjibuje anaweza kuzuia ego yake isiathiri utendaji wake. Lakini, ni wengi ambao ego hii imewaathiri. Hapa naongea tu randomly na TAFADHALI usione kama ninakuhukumu au kukutuhumu kuwa ndivyo unavyofanya.

Lakini, ukijua jinsi ya kucheza na akili ya mwenza wako..utapata mengi mema ya nchi. Na siri hiyo haianzii kitandani..inaanzia kwenye ulimi wako. [kwa kuongezea ni ULIMI - JIKONI - KITANDANI]

Hapa naongea pia na wanaume wenzangu, siku zote ukiishi na mwenza wako kwa ushindani mtaendelea kugombana TU na kuonana wabaya.
 
Hujakosea kabisa lakini unaweza kudanganywa omba salary slip kama atakubali.

Naombeni ushauri wenu....
Naishi na mwanaume kabla sijawahi nae nilikua nina kipharmacy kidogo ambalo lipo mpaka leo ila tofauti ni kwamba tulipoamua kuishi pamoja nilimfata mkoa mwingine ambapo sio mbali sana na duka lilipo hivyo nikalizimika kuweka mtu wa kuniuzia ambapo hua naenda kumkagua mara kwa mara

Mwenzangu ameajiliwa serikarini anapokea hela nzuri nadhan mara 2 au 3 ya kipato changu jamaa jana nashangaa gafla tu anataka tupige hesabu ya mapato ya duka langu naingiza ngapi faida kwa mwezi mi sikukataa ila nikamwambia tukimaliza kupiga kwangu tuje na kwenye mshahara

Nimemwambia hivyo sababu hajawai kuniambia mshahara wake wala matumizi ya mshahara wake sijui akitoa hela ya matumizi basi na mara kwa mara anatuma hela kwao bt sijawahi kumuumiza chochote sasa nilivyomwambia tupige hesabu dukani na mshahara kanuna tangu Jana hana raha na mimi ananisemesha penye ulazima tu

Je nimekosea kumwambia hivyo?? maana kama matumizi natoa maana tuliwekeana kila mwezi tuna ac ya familia ye anaweka laki 4 mi naweka 2 kwa ajiri ya matumizi ya badae bado nikiona vyombo vizuri, mapazia, shuka yan vitu vidogo vidogo na nunua mbali na hela niliyosave tangu kanioa nguo najinunulia tu mwenyewe sasa nimekosea wapi ndugu zanguni?
 
Back
Top Bottom