Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,180
- 7,356
Ni mwanadada tunafanya nae kazi, anatarajia mtoto wake wa pili kuzaliwa hivi karibuni (Mungu akijalia). Kinachomtatiza ni kuwa amepata housegirl mpya baada ya aliyekuwepo kuolewa hivi karibuni. Haijui sana historia ya huyu mpya japo anajua kijijini kwao, lakini sio mgeni mjini (aliwahi kufanya kazi sehemu zingine, Arusha). Katika kustorisha na wamama wenzie, huyu dada alishtushwa aliposikia stori (hana uhakika), kwamba kuna watoto wawili wa familia moja waliwahi kupata maambukizi ya HIV wakati wazazi wao wakiwa negative, na ilipokuja kuchunguzwa ikagundulika kuwa HG akikuwa positive, na iliaminika walipata maambukizi kutika kwake ama 'makusudi' au 'bahati mbaya'... Huyu mdada amekuwa na wasiwasi kidogo kwani akiwaza ukweli kwamba mdada wa kazi atakuwa karibu sana na watoto, kuwalisha na kuwasafisha na cares nyingine anahofu isije kutokea 'bahati mbaya'
Ingawa baadhi ya wanawake wenzake wamemshauri akampime mdada wa kazi na kumwambia kuwa hata wao wanafanya hivyo, bado huyu mdada anaona ugumu fulani. Ameniomba ushauri, tukalijadili kidogo lakini haikufika conclusion. Pamoja na kufikiria hiyo chance ya 'bahati mbaya', bado tumezingatia 'haki' za mdada wa kazi (maana ni mtu mzima), lakini pia uhakika kwamba negativity ya mdada huyo kama itakuwa kigezo cha usalama wa watoto. Umekuwepo ugumu kuwa endapo kwa bahati mbaya akikutwa positive, mdada huyu atafanya nini, amfukuze? Sio vizuri.. Na asipomfukuza, hatajikuta akimchukulia kwa wasiwasi sana hali inayoweza kujenga unyanyapaa fulani?
Hebu tupieni ushauri wenu wanajamvi, maana nimeishia kumuambia asifanye hivyo kwanza, wakati akiendelea kupata ushauri wa watu tofauti...