Wakuu poleni na hongera katika shughuli zenu za hapa na pale
Sasa nimekuja kwenu, mnishauri mimi kama kijana wa kiume nisie na kazi na bado nawategemea wazazi kwa kuwa bado ninasoma
Iko hivi niko kwenye mahusiano na msichana kwa muda ambao ni kama miezi miwili tu.
Yuko chuo na mimi pia nipo chuo.
Sasa kilichonifanya kuja kwenu, anadai natakiwa niwe ninampa pesa ya kusuka kila mwezi kiasi cha sh 20,000 taslimu.
Na akaongezea ya kuwa kama sitampa hiyo hela hakuna mapenzi kwa sababu, haiwezekani niwe namtumia tu alafu nisiwe ninampa hela.
Isitoshe yeye anao mkopo na mimi ninao mkopo.
Lakini mimi sikai ndani ya chuo nipo nje nimepanga, nikipiga gharama za kodi na michango mingine kiukweli sitaweza toka na chochote katika pesa hii ya Boom.
Maana najitahidi nisave angalau visent kadhaa ili nikirudi kitaa nipate pa kuanzia.
Nimemshauri kuhusu swala la kukaa wote ili angalau tusave walau kiasi fulani, ili hapo baadae tuweze anzisha hata kabiashara, kama ikishindikana kuanzisha pamoja bhasi, kila mtu ataanzisha mradi wake na kama tuna malengo ya kweli tutaweza fika mbali, ukizingatia sasa hivi ajira ni changamoto.
Sasa naombeni ushauri wenu wakuu, Je hapo mimi kama kijana, ninae soma na kutegemea wazazi
Natakiwa nitoe 20,000 kila mwezi, nikishindwa nimeambiwa kutakuwa hamna mapenzi. Yatabakia ya mdomoni tu na mwisho yatakufa kabisa.
Ushauri wenu wakuu katika hili.