Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 93,484
- 119,336
Yule bwana mwingine alikuwa mpole sana hadi akaitwa 'dhaifu'. Yeye alikuwa hatengui tengui teuzi zake.
Yeye ilikuwa mtu akipwaya sana anapewa muda mwingi wa kujirudi. Hali hiyo ilipelekea yeye kuitwa kila aina ya majina ya dhihaka na wanachama wa JF ndo walikuwa mstari wa mbele kumkosoa kwa huo 'udhaifu' wake.
Zama zake zilikuja na zikaisha. Sasa tupo kwenye zama za Ngosha.
Huyu ngosha yeye yuko tofauti sana na bwana yule aliyemtangulia. Ngosha yeye akikuteua leo na baadaye kidogo akikuona unapwaya anatengua uteuzi wako mara moja.
Hiyo ni sifa ambayo bwana yule hakuwa nayo.
Lakini sasa cha ajabu huyu Ngosha akifanya kile ambacho yule bwana hakuwa na mazoea ya kukifanya, naye anaishia kulaumiwa, kubezwa, na kulaaniwa eti anatengua sana teuzi zake.
Kwa kweli watu wameshavurugwa kiasi kwamba hawajui hata wakitakacho tena.
Sasa kama huyu Ngosha anamteua mtu na baadaye anakuja kuona huyo mtu anapwaya watu mlitakaje? Mlitaka amchekee chekee tu?
Hata ingekuwa mimi ndo nimekuteua halafu nakuona unapwaya kwenye hiyo nafasi natengua tu uteuzi wako. Sina kabisa muda wa kuvumilia ukadiri [mediocrity].
Ila kusema ukweli uongozi wa umma ni kazi ngumu sana. Manake ukifanya yale ambayo yalikuwa yanapigiwa makelele na watu kuwa hayafanyiki mwisho wake unaishia kulalamikiwa tu na wewe kuwa umezidi kuwa hivi na vile!
Ni kazi ambayo haina shukurani za papo kwa hapo. Na ndo maana hata rais Kikwete ambaye alidhihakiwa sana kipindi chake leo hii eti anasifiwa na hao hao walokuwa wanamdhihaki na kumwita 'dhaifu'.
Hivyo naamini ipo siku tu hata huyu Ngosha mtamkumbuka, mtamshukuru, na mtamsifu. Ni suala la muda tu.....