Dharra
JF-Expert Member
- Jun 23, 2017
- 1,661
- 2,975
Mi mida ya lunch hours wakati naenda kupata zangu ugali basi kwenye zile corridor za posta macho yangu yalitua kwa mdada mmoja taanusi sana, nikamsalimia na kushika njia, kidogo nasikia are you in hurry? nikamwambia sio sana. Moyoni nikajua ni mzinga unakuja aidha nitaonyeshwa cheti cha hospitali zinahitajika dawa na hana nauli, ila roho nayo ilikuwa inakataa kuamini hivyo kutokana na mueonekano wa binti ulivyokuwa, fasta nikapewa business card na kesho yake muda kama huo nikaalikwa holiday inn mezzanine floor kwa maongezi ya biashara. Njoo na huojutia, nikasema sawa. Mjini hapa ni bora usikatae wito nikaenda, kaa chini nikaletewa juice... akaanza mimi ni wakala wa Oriflame, kafungua mkoba na vichupa chupa kibao, kaongea alivyomaliza nikamuuliza Juice umelipia ama ninalipa? akasema nimelipa, nikamwambia ahsante sana kwa maelezo yako lakini sipo interested, ila wewe ni mdada mrembo sana. Kwaheri. Alipigwa na butwaa akanyamaza kimya, nilisimama na kuondoka.