Ananishawishi sana kuingia kwenye QNET mpaka anakera!

Ananishawishi sana kuingia kwenye QNET mpaka anakera!

Ndivo walivyo na wengi wao hawajali ratiba za wengine ,wanaona izo habar zao ndo za muhimu kuepuka karaha usipokee simu zake au mblock
 
Daaah Mkuu poleee sana na Hongera kwa kuukimbia mkenge.. Mimi kuna Demu Mmoja nilijuana nae kama Rafiki tu akaleta issue hizo za kuniforce nijiunge hiyo mishe nikawa namzungusha simu kibao nikaona usumbufu nikamwambia aje Geto anieleweshe vizuri akaje ndo hapo mwanzo wa isidingo ukaanzia akaishia tu kupigwa Mashine na habari ya kunishawishi ikaishia hapo...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kauli mbiu yao ni '' Haina kufeli'',hapo mkazie mwambie huna mrengo huo wala wito huo.Wanadanganyaga na gari za kifahari,maisha south africa nk,huo ni upigaji.
 
Hawa jamaa wa Qnet wamemtengeneza jamaa yangu na yeye kachukua mikopo kibao na yeye kajiunga na tena baada ya hapo walimwambia achague zawadi akachukua saa kwa 4.8M akawa analazimisha watu kibao kwenda mpaka anatukodia bodaboda ili atuingize kwenye mtandao na tulienda pale cha maana hakuna, wakawa wanaosifia tu hiyo Qnet sijui wanaodhamini Man city ya Uingereza na pia wanakidhamini chama cha mpira Africa (CAF) blah blah nyingiii hakuna cha maana hawakueleza huo utajiri unaupataje? Na watu kibao hasa wa kina Mama na wazee wastafu wamejazana pale Sinza Mori ndani ndani, kwa blah blah zile sikurudi tena. Na huyo jamaa kawa mtumwa wa kulipa madeni ya mikopo na hata huo utajiri sijauona, hahahaa kwenye DP WhatsApp kila siku anaweka picha za magari makali halafu anaandika DOLLARS, Lakini hakuna lolote na mwezi uliopita walimwalika RC Makonda sijui kulikuwa na event gani? In short ni ndoto za mchana na hakuna cha maana pale.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee mkuu na mimi niliitwa hapo hapo sinza mori na demu mmoja rafiki yangu,
Akasema ana fursa sijui, nikaenda nimefika humo kwenye nyumba kuna vimeza na viti, mara GOOD MORNING na ilikuwa kama saa tisa hiyo, nikasema hawa watu vipi?

Nikaona wananiletea stori tuu, wananiambia habari za man city kuwa QNET ndo wazamini ,

Wakasema niende siku nyingine nikawapotezea . Yaani simu ilikuwa inapigwa kila dakika .

Ving'ang'anizi sana , harafu wao wamechoka tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jiulizeni Kwanini nchi ya India kuna wanajimu wengi sana wa nyota.Jiulizeni kwanini mchina akikuambia shati ni shs 10,000 wewe ukamwambia nitengenezee ya 2000 anakutengenezea anachofanya ni ubora unakuwa wa hovyo.
Point yangu hapa ni kwamba idadi yao ni kubwa huku hakuna ajira na wasomi ni wengi.
Tukija kwetu Tanzania wasomi wengi mno ajira hakuna watu wanatumia akili ya ziada kutafuta maisha take care.
Kwa wakina dada hasa walioachika na wasio na ndoa maisha ni magumu siku hizi wanaume nao wana hali ngumu hawahongi.
Mdada mmoja aliachika kwenye ndoa yake alinisumbua sana kuniambia nimuunganishe na dada yangu wafanye Qnet nikagundua ameniambia hivyo vile amegundua anastaafu atapata mafao.Inshort nilimtolea nje nikamuambia my sister is well off sana hawezi kufanya hivi vitu
Kufanya fursa na mwanamke inahitajika roho ya ziada.
Ukiambiwa mtafute fursa jua wewe ndio fursa.

Sio wanawake walio achika tu wapo na wanaume tena wengine mke na mme wapo humo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu iyo sehemu ni Makumbusho?

Aisee mkuu na mimi niliitwa hapo hapo sinza mori na demu mmoja rafiki yangu,
Akasema ana fursa sijui, nikaenda nimefika humo kwenye nyumba kuna vimeza na viti, mara GOOD MORNING na ilikuwa kama saa tisa hiyo, nikasema hawa watu vipi?

Nikaona wananiletea stori tuu, wananiambia habari za man city kuwa QNET ndo wazamini ,

Wakasema niende siku nyingine nikawapotezea . Yaani simu ilikuwa inapigwa kila dakika .

Ving'ang'anizi sana , harafu wao wamechoka tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom