mwenda wazimu
JF-Expert Member
- Feb 20, 2017
- 819
- 1,283
ACHA KUCHEKESHA ETI OOOHHH ANANIPENDEA PESA
Unaishi nyumba ya kupanga na hata kama umejenga kwa mkopo kudunduliza matufali, una kagari kamkopo au hata ni mtu wa daladala. Akija kwako ukijitahidi sana umempa hela ya Bajaji sana sana utaongezana naye kutembea kujifanya eti mapenzi kumbe ubahili.
Ukimpeleka gest umejitahidi sana elfu hamsini. Halafu kakuomba hela ya saluni unaanza kujishaua ooohh huyu dada anapenda hela oooo hana mapenzi ya kweli anapenda hela tu. Uanchekesha ndugu yangu kwa hela zipi ulizonazo!
Yaani mtu unajiunga Bando la Chuo wakati ni MHENGA halafu uansema unapendewa pesa. Unasema oohhh anataka kuhongwa ndugu yangu ndugu yangu, tofautisha kuhonga na kuhudumia na acha kujipandisha namna hiyo.
Kama hujawahi mnunulia mwanamke Gari unatoa hela ya Bajaji jua wewe huhongi unahudumia, unatoa tu huduma ya usafiri basi. Kama hujawahi mnunulia Brazilian ya milioni moja na laki mbili ndugu yangu wewe ile elfu thelathini ya saluni huku honga ulihudumia.
Kama akikuomba laki mbili ya msibani unatoa elfu ishirini na unataka uende kabisa huko msibani ndugu yangu wewe huhongi unahudumia. Hivyo hembu tulia pambana na hali yako acha kumharibia jina binti wa watu kwa kusema ohhh eti anapenda pesa.
Nikuambie kitu huyo Dada angekua anapenda pesa angekua ashakuacha muda mrefu. Mtu kila siku hata hajawaza kukuomba hela ushaanza kulia shida ili usiombwe. Anakuvumilia tu na wewe huhongi bali unahudumia kutokana na huduma unazopewa!
[HASHTAG]#KaaKimya[/HASHTAG]
COPY AND PASTE