Ananiambia nijipange kwao Mahari huwa ni kubwa. Nimempa assignment

Mahari Inategemea sana na tamaduni/uelewa wa baba upande wa binti, kwa mfano kuna jamii moja ya kanda ya kati hapa Tz kuku kadhaa tu ni mahari tosha unaoa! then kuna ukanda mwingine ni ng'ombe kadhaa nakama bint mweupe mahari inapanda maradufu, yet kuna jamii nyingine mahari anataja bint, nakubuka kuna mkubwa mmoja wa jeshi la polisi mahari alisema bint na alisema anataka msahafu wa dini yao tu hana jengine. Na kwa mfano baadhi ya jamii ya kikomoro aisee wana mahari kubwa na wao wako happy kuzitoa.

Kwa ufupi mara nyingi mahari hutemea upande wa muolewa wanasemaje (mara nyingi baba) na anayeoa aseme anataka mahari iwe kama anavyotaka yeye. Ingawa hizi pande mbili zinaweza kukaa zikanegotiate
Ma baba hili nalo waliangalie,wanawasotesha mabinti zao wanaishia kuzalishwa tu nyumbani,
 
Ni uhuni tuu na Mila za kishenzi.
Kumuuza Binti yako sio uungwana.
Unataka Mahari Kwa vigezo vipi?
Kama ulimlea Binti yako hata huyo kijana alilelewa na Wazazi wake,
Binti ndio ataje Mahari, Kwa sababu yeye ndiye muolewaji, yeye ndiye MKE mtarajiwa na ndiye mwenye uhitaji wa kuolewa.
Mzazi anataka Mahari Kwa misingi ipi?
Watoto wa kike ni mitaji
 
Ungejua nafasi yako kama mwanaume unayetegemea kuanzisha familia itakayokutegema kama mkuu wa kaya kuna vitu ungevitazama kwa jicho la tofauti sana.

Yaani umemchambua binti watu kiasi hicho!? Hapo kisa sio mahari tuu! Hayo maneno yameonyesha ulivyo na roho chungu na mbinafsi.

Kama hakufai si umwache? Au ukiambiwa umwoe bila mahari ndio unamwona mwanamke bora??

Tafuta wakubwa wakueleze maana ya mahari watakuambia Mahari ni kipimo cha kujua kama mwanaume yuko tayari kubeba jukumu la ndoa na familia.

Halafu ukiwa mwanaume ukapangiwa mahari kitendo cha kuikubali tuu ni alama tosha kwamba wewe ni mwanaume mwenye kujielewa, mpambanaji na mpiganaji. Mahari unaweza kulipa yote mahari unaweza lipa kwa awamu.

Halafu, Kama mahari imekushinda utaweza kulea mke na watoto?
Nianze na ww..mwanao wa kike mahari yake bei gani?
 
Kama mahari ni kipimo cha ukomavu wa mwanaume, mwanamke kipimo chake cha ukomavu ni nini?
 
Mfano,

Kuna binti alitolewa barua laki saba,mbuzi sijui na mablanket,

Mahari alitaja milion tatu,kwa wazazi

Na akachukuliwa kuishi na huyo bwana,

Sasa maisha ya humo ndani yashamshinda/amechoka na kuondoka hawezi mila zao hadi azae na huyo bwana tena mtoto wa kiume ndiyo atoke

Sasa mtu unateseka kisa wazazi wako walikula pesa za mahari, hii hapana
 
Nianze na ww..mwanao wa kike mahari yake bei gani?

Utaratibu wa mahari hautoki kwangu, kuhusu mwanangu itajadiliwa na kuamuliwa kadri ya imani na desturi zetu

Ikiwa ni gram 900 za dhahabu, ng'ombe na Punda powa tuu
 
Naenda kugalagazwa mie halafu mahari wale wengine,

Tumetofautiana imani kwa nyie waarabu ni sawa wewe mtt wa kike kutaja mahari yako
 
Utaratibu wa mahari hautoki kwangu, kuhusu mwanangu itajadiliwa na kuamuliwa kadri ya imani na desturi zetu

Ikiwa ni gram 900 za dhahabu, ng'ombe na Punda powa tuu
Kama baba yake akikataa izo gram 900 na ng'ombe utakaa asiolewe?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom