Analysis: The World’s Biggest Arms Importing Countries In 2018

Halafu kuna kitu cha muhimu sikukiweka hapa. Nchi kama Pakistan, Uchina na Saudi Arabia zinaongoza kununua silaha kwenye soko haramu (Black Market). Serikali ya Pakistan ilitengeneza silaha zake za nyuklia kimya kimya bila dunia kujua kwasababu vifaa vyote ilivinunua kwenye soko haramu. Serikali ya India nayo ikafanya hivyo hivyo kutengeneza silaha zake za kinyuklia.

Sasa tukiweka na bajeti inayotumika kununua silaha kwenye soko haramu, basi tunaweza kukuta bajeti ni kubwa zaidi ya hiyo hapo juu...
Kwenye black market East Africa inaingia nchi ya maziwa na asali
 
Ni dhahiri kumekuwa na utofauti mkubwa tu katika hizi taarifa hasa ukifuatilia kuhusu East Africa maana hawa SIPRI kuna kipimo chao huwa wanakitumia katika taarifa zao.

Mfano kuna hizi takwimu hapa za SIPRI zinaonesha kuwa, Kwa mwaka 2017, Tanzania haikufanya manunuzi yeyote yale ya silaha yanayotambulika, huku Kenya na Uganda wakiwa vinara kwa mwaka huo wa 2017 kwa manunuzi ya takriban $13 milioni ambayo ni ya Kenya na $18 milioni kwa Uganda ambaye ndiye aliongoza kwa mwaka huo.

View attachment 1132969

Uko sawa kabisa, kuna utofauti mkubwa sana lakini nadhani at a mainstream level SIPRI is very credible.
 
Hahahaha....hawa Pakistan na India hawa ugomvi wao sijui kama utaisha.Yaani kila mtu anajihami kwa ajili ya mwingine..
Pili nchi za kiarabu mfano Saudia...wananunua silaha nyingi lkn uwezo wa kuzitumia hawajui....Saudia na silaha zote bado Houthi rebels wanawasumbua....wameshindwa kabisa kuwateketeza...na hapo wametengeneza coalition ya nchi....
Halafu kuna kitu cha muhimu sikukiweka hapa. Nchi kama Pakistan, Uchina na Saudi Arabia zinaongoza kununua silaha kwenye soko haramu (Black Market). Serikali ya Pakistan ilitengeneza silaha zake za nyuklia kimya kimya bila dunia kujua kwasababu vifaa vyote ilivinunua kwenye soko haramu. Serikali ya India nayo ikafanya hivyo hivyo kutengeneza silaha zake za kinyuklia.

Sasa tukiweka na bajeti inayotumika kununua silaha kwenye soko haramu, basi tunaweza kukuta bajeti ni kubwa zaidi ya hiyo hapo juu...
 
Wakijaribu kutengeneza silaha zao makampuni kama Raytheon, Kalashnikov Concern, Boeing etc yatakula wapi ? Technological Colonialism is very real, if any of these growing countries try to walk away from Washington's/Russia's/ Orbits of influence by building or diversifying technological dependence then assuredly i tell you, Corporatists in Washington will be lobbying for a regime change whilst spooks in Moscow will be formenting instability and chaos: Turkey's F-35 deal is a good example for the former and Ukraine's bid to join the EU and NATO for the latter.....

Hivi hizi silaha kubwa kubwa (excluding small arms zinazoweza kutengenezwa hata na watunduwatundu wa mtaani) zinazouzwa kinyemela kwa waasi in which way they've got in the hands of rebels?

Maana kweli hao Defence contractors wanaweza uza Silaha zao Black market bila Washington kujua?
 
Hakuna data zinazoonesha Tz aliwai kununua silaha Israel

Cha kushangaza zaidi siku hizi wana kitengo cha drone ambazo pia hakuna data
Kuwa hizo drone zilitoka wap

Mkuu ununuaji wa Silaha lazima uwe katika mfumo wa Siri ili kuzuia mivutano na mashindano ya Silaha na majirani

Kama hizo data zingekuwa kama magazeti ni tatizo, na nature ya Jeshi ni kama vyombo vya ujasusi kunatakiwa usiri katika uendeshaji wa mambo yake
 
Hivi hizi silaha kubwa kubwa (excluding small arms zinazoweza kutengenezwa hata na watunduwatundu wa mtaani) zinazouzwa kinyemela kwa waasi in which way they've got in the hands of rebels?

Maana kweli hao Defence contractors wanaweza uza Silaha zao Black market bila Washington kujua?

Kwenye soko haramu hata silaha kubwa kutoka kwa makampuni makubwa zinauzwa tena kwa baraka za Washington. Mfano mzuri ni Iran-Contra Scandal ya mwaka 1985-1987, ambapo serikali ya Ronald Reagan iliiuzia silaha serikali ya Iran ambayo kwa wakati huo ilikuwa imewekewa vikwazo na inachukuliwa kama adui wao.

Nchi za Warsaw Pact walikuwa na sera ya kutuma wanasayansi kwenye nchi husika ili kujenga usiri. Wanawaambia mkusanye vifaa, malighafi na mtengeneze maabara halafu wao wanatuma wataalamu kutengenza hizo silaha. Hapa kinachouzwa kwenye soko haramu ni huduma (Service) na siyo bidhaa (Goods/Weapons)

Walifanya huo mchezo kipindi cha utawala wa Serikali ya Gamal Nasser wa Misri ambapo East Germany (Communist Germany) walikuwa wanatuma wanasayansi kuwasaidia wamisri kuunda makombora ili kuwapigia wayahudi kule Israel. Sasa wakina Moshe Dayan wakaanza kutuma Mossad kuwaua wanasayansi wale hadi wakaanza kwenda Misri kwa siri sana.

NB: Soko haramu ni pana na tuliangalie kwa jicho la tatu, maana hata hawa Private Military Contractors kama ACADEMI (Black Water) n.k wanapochukua kandarasi za kufundisha makundi ya magaidi huko mashariki ya kati nayo hiyo inahesabika kama biashara haramu.
 
Sio kweli kuwa ununuzi wa silaha ni siri ili nchi yoyote iuze silaha au kununua ni lazima ipate baraka za umoja wa mataifa that why tunaona kuna baadhi ya nchi haziruhusiwi kununua silaha mfano ni Eritrea

Usiri wa ununuzi wa silaha uwa unafanywa na nchi yenyewe mfano wewe unaamini kuwa ni kweli mwaka 2017 Tanzania haikununua silaha yoyote ?
Mkuu ununuaji wa Silaha lazima uwe katika mfumo wa Siri ili kuzuia mivutano na mashindano ya Silaha na majirani

Kama hizo data zingekuwa kama magazeti ni tatizo, na nature ya Jeshi ni kama vyombo vya ujasusi kunatakiwa usiri katika uendeshaji wa mambo yake
 
Wanahistoria husema hivi "it was rapid militarization of the European continent, which built aggrandized overconfidence on the part of Imperial Powers and eventually created an awful spectre for world war one and world war two"
Uko sahihi. Jukwaa linaandaliwa kwa jili ya vita ya tatu na ya mwisho, mbaya kuliko zilizotangulia. Kuna mambo hayana jinsi ila kutukia. Alliance ya Russia, Turkey, Iran na Afrika ya Kaskazini itazidi kuwa na nguvu. Asia lazima itazidi kuongezeka kijeshi kwa sababu kuna assignment ya wao kufanya.

Dunia lazima ianze kukosa uongozi bora na vilio, maumivu na kuonewa viwe vingi. Siku zijazo kutakuwa na turbulence kubwa ya kiuongozi. Lazima ifike mahali dunia iwe na mashaka kuliko sasa.

Wakati wa drama kuanza unazidi kusogea, lakini ni lini sijui. Naona Key players wanakaa kwenye nafasi zao. Kelele za maandalizi nyuma ya pazia. Mfungua pazia hajafungua bado ili drama ianze....
 
Mwadamu mwanadamu. Sijapata majibu ya haya yote. For what? Why not investing in peace than war?
Kuna msemo unasema;

"If you want peace, prepare for war"

Yaani, ili kujihakikishia amani, muda wote ni kuwa na silaha na kuwa tayari kujilinda mwenyewe.
 
Unahitaji akili kubwa kutengeza silaha zako
Wakijaribu kutengeneza silaha zao makampuni kama Raytheon, Kalashnikov Concern, Boeing etc yatakula wapi ? Technological Colonialism is very real, if any of these growing countries try to walk away from Washington's/Russia's/ Orbits of influence by building or diversifying technological dependence then assuredly i tell you, Corporatists in Washington will be lobbying for a regime change whilst spooks in Moscow will be formenting instability and chaos: Turkey's F-35 deal is a good example for the former and Ukraine's bid to join the EU and NATO for the latter.....
 
Saudi Arabia haina silaha za nyuklia

Back
Top Bottom