Heshima yako mkuu, nafikili unamaanisha Digital to Analogue Converter (DAC) lakini hiyo ni sehemu ndogo ndani ya kingamuzi kamili chenye subassemblies nyingi kama vile ku-decompress picha/rangi/sauti na mambo mengine chungu mzima za kukuwezesha uone picha na kusikia sauti in analogue form.
Mkuu wangekwambia ununue a Digital TUNER ningewaelewa, sina uhakika kama tuner hizo zinapatikana nchi, na ukihamua kununua tuner ya Digitali basi utahitaji vile vile huwe na ramani (circuit diagram ya TV yenyewe na ya Digital tuner vile vile) ili uweze kujuwa jinsi ya kufanya modification/kuzifunga, hii inahitaji utaalamu na umakini sana, tatizo la njia hii ni kwamba utakuwa unaona channels ambazo siza kulipia.
Mimi nakushauri jikakamue ununue vingamzi au nunua StarTimes TV yenye inbuilt kingamuzi, TV za StarTimes yenye screen ya inchi 21 sio gharama sana na ni NZURI. Sasa hivi nilikuwa nasikiliza kwenye redio kuna vingamuzi vinahuzwa kwa shilling elfu thelathini elfu tu, kanunue hivyo basi.