Anachotaka ni mimba tu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anachotaka ni mimba tu!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by SnowBall, May 24, 2012.

 1. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Heshima mbele wanaMMU

  Ninayoiweka hapa ni mada ya ukweli ambayo rafiki yangu aliniletea tuidisscus..sasa katika kuidiscuss kuna mawazo ambayo nilimpa na of course kuna mengine ambayo tulishindwa kuafikiana. Lakini kwa sababu kisima cha JF hakikaukiwi maji nimeona kabla hajafikia uamuzi rasmi basi niwashirikishe nanyinyi hapa ili nione kama mnaweza kuchangia kitu gani katika huu mpango mzima!

  Iko hivi..Jamaa yangu huyu alishawahi kuwa na rafiki wa kike kama miaka kumi iliyopita maeneo ya huko Mwanza. Na kama mnavyojua raha ya maisha kuhangaika, baada ya muda mrefu kila mtu kuwa kwenye mihanjo yake mawasiliano yalikatika na kila mtu kupata uhusiano mpya. Jamaa yangu alioa na kwenye ndoa yake kajaaliwa kupata mtoto mmoja, halikadhalika bibie naye aliolewa na kubahatika kupata mtoto mmoja pia. Kwa kipindi cha miaka ya karibuni kama miaka mitatu iliyopita marafiki hawa wa zamani walijikuta wameonana na wakawa wamebadilishana mawasiliano na wakaanza kuwa wanajuliana hali na vitu kama hivyo. Kwa mujibu wa huyu jamaa yangu, ilionekana kama mwanamke alikuwa anapenda wakumbushiane na jamaa yangu kwa mujibu wa alivyoniambia alimwambia waheshimu ndoa zao na wabaki kuwa 'friends'. Kwa mujibu wa mshkaji, mwanamke aliliafiki kwa shingo upande tu.

  Sasa, tatizo limekuja,Mume wa yule mama alifariki..na mshkaji wangu hajui kilichomuua japo inasemekana ni 'pressure' na ofcourse ni kama mwaka mmoja uliopita na jamaa kwa mila na desturi baada ya siku nyingi za kutokwenda Mwanza alienda kwao na akaamua kwenda kumpa pole huyu mama. Cha ajabu huyu mama aliipokea pole yake lakini pia akamwambia angependa azae naye kwa sbb anahisi anahitaji mtoto na hayuko tayari kuolewa tena coz umri umeenda. Mshkaji wangu anadai alimchomolea, lakini yule mama alimwambia..'wewe nipe mimba tu hayo ya ulezi niachie mimi'!.

  Sasa ili kufupisha habari hapo ndio kesi ilipo..Jamaa alifanikiwa kuchomoa kwa mara ya kwanza lakini huyu mama kaja hapa Dar na kampata jamaa na madai yake yamesimama vilevile!!..Naomba ushauri hapa 'Je? ampe tu hiyo mimba au asepe mazima!!..

  NB: Matusi na Kejeli sio kitu cha maana hapa, na kama huna la kuchangia please ukimbie huu uzi!!
   
 2. majany

  majany JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Sep 30, 2008
  Messages: 1,199
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  aachane naye.....atulie na ndoa yake.....
   
 3. mkonowapaka

  mkonowapaka JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 1,483
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  ampe imekua nyanya iyo.........mimba zenyewe za siku hizi hivyo vizazi sijui vimeingiwa pepo gani.....unat[neno baya]ba weee miaka mitano ndo inaingia.....ampotezee tu uyo!
   
 4. promiseme

  promiseme JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Mar 15, 2010
  Messages: 2,715
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 135
  Huyo rafiki yako anatakiwa awe na msimamo,na asijifanye kidume yatamtokea puani,kwani mkewe hana uwezo wakuzaa au yeye peke yake nfio mwenye mbegu salama? amuache kama alivyo na aheshimu ndoa yake sababu asicho kipenda yeye asimfanyie mwenzie pindi mkewe akija kujua patakua hapatoshi.
   
 5. d

  dmatemu JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 591
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 60
  sasa kuna haja ya kuomba ushauri hapo kwa situation kama hiyo? Huyo jamaa yako ana tamaa na anataka ndo maana anajiuliza uliza wkt jibu ni rahisi tu, NO. Amwambie haiwezekani bse ye ni mume wa mtu tayari.
   
 6. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Ahsante mkuu kwa ushauri..umezingatiwa
   
 7. samstevie

  samstevie JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wala hakuitaji hata ushauri kwako kuamua, kama anaiheshimu ndoa yake asithubutu pili anauhakika gani kama huyo mama mumewe alikufa kwa maradhi gani. Yeye ni mtu mzima asithubutu kujaribu ni hatari sana kwani akishashawishika kwenye swala la mimba litahamia kwenye malezi na kisha atataka waretain mapenzi. Hivi na mkewe akitaka kukumbushia aliyemtoa bikra na habari zikimfikia rafiki yako atajisiaje?
   
 8. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Mkuu mkonowapaka unamaanisha ingekuwa inaingia kwa wepesi sio issue??..yaan taabu ni kwa sbb inachelewa kuingia??..Funguka bro!
   
 9. steveachi

  steveachi JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 4,129
  Likes Received: 1,731
  Trophy Points: 280
  kwa nini analazimisha wazae tu,mmmh,kuna k2 hapa anakificha huyo mwanamke,,isije ikawa anataka kujaribisha kuzaa aone kama atazaa salama ajiridhishe kuwa hana ngwengwe manake hv ndo vipimo vya huku kwe2 uswazi,amchomolee tu ukizingatia ana mke ampendae,ajitahidi asimkaribie kwani atamtia vishawishini sana
   
 10. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Umesomeka bro!
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,335
  Likes Received: 1,797
  Trophy Points: 280
  Eeeh..haya weee
   
 12. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Nimekusoma mkuu!..kweli za kuambiwa changanya na za kwako!
   
 13. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Aache tamaa maana tayari yeye ana mke. Hilo la kusema ampe mimba tu ni mtego wa kumrudisha tena kwenye kukumbushia enzi ambayo itamsababishia huyo kaka aje aharibu ndoa yake. Mwambie asimamie ule ule msimamo wake wa awali ...
  Kupewa mimba ni lazima ku-do, na ukisha do mara moja, wenyewe wanasema safari moja huanzisha nyingine, take care!
  Akimzingua sana, amuwekee mambo kwenye chupa akajitilie mwenyewe huko, shauri yake, alaaah !!! <Hapa am joking!...>
   
 14. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Unajua unapokuwa kwenye eneo la tukio kuna mengi yanajitokeza mkuu na nadhani kuna mengineyo ambayo hakuniambia huenda ndo yamepelekea yeye kushindwa kutoa jibu la moja kwa moja kama 'YES' ama 'NO'. Na kwa sababu hiyo sioni kama alifanya vibaya kuja kuomba ushauri mkuu!!..Anyway ushauri wako umezingatiwa!
   
 15. Ennie

  Ennie JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2012
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 7,145
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Mwambie akaombe ushauri kwa mkewe.
   
 16. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #16
  May 24, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,860
  Likes Received: 1,134
  Trophy Points: 280
  haa! mbna kitu iko open kabisa. huyo mama anataka kurudisha mapenzi tena ya muda mrefu. sa kaona ili kumtia kitanzi hyo baba ni kutaka abebeshwe mimba. mwambie jamaa ako huo ni mtego tena kitanzi ambacho anakikaribisha kwa mikono miwili. kama kaichoka ndoa yake akubali upuuzi wa huyo mama! aheshimu ndoa yake yalopita yashapita, na huo wema utamgharimu...
   
 17. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Kama shida ni mtoto tu si wapo wakupandikiza? huyo mama akanunue mbegu.
   
 18. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Nimekusoma dada/kaka Charminggirl..message received!
   
 19. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #19
  May 24, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  rafiki yako anamtamani huyo "mpenzi" wake wa "zamani?'
  kama hamtamani mbona iko wazi kabisa?
  amkatalie
  na avunje mawasiliano ya aina zote....
   
 20. stephot

  stephot JF-Expert Member

  #20
  May 24, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 5,027
  Likes Received: 2,648
  Trophy Points: 280
  Hiyo tabia ya wanawake kusema nipe mimba siju huwa ni wanawake wote wanapopagwa na mapenzi ndio huwazia hayo au ni baadhi tu,utampa hiyo mimba na kintakachokuja kuzaliwa ni kiumbe kinachoishi na kitakuwa kina mahitaji ya lazima kama kuwa na Baba na Mama,na mengine ambayo yatamfanya aishi,sasa unapokubali hayo ujue atakapozaliwa lazima hivyo vitu avipate na huyo anaesema we nipe mimba halafu uniachie nitatunza mtoto nakuhakikishia hakuna ukweli kwenye hilo bro,moto utakaokuwakia utajuta kwanini ulifanya huo ujinga kwani mkeo ujue ni lazima atakuja ajue kwani hakuna siri kwenye hayo mambo na ndoa yako itakuwa tayari imeingia mahali pabaya sana,nakushauri uachane na hivyo vishawishi vyake vya kijinga na kama anahitaji sex use a Condom.
   
Loading...