Anachofanyiwa Masanja ni kinyume na utu

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
13,369
10,778
NInashare nanyi ujumbe nilioukuta kwenye Whatsapp Group
IMG-20221010-WA0058.jpg


Hizi picha zimesambaa sana mitandaoni these few days.

Mtanisamehe kama ninawakwaza kwa kuiweka hiyo. Lakini nina lengo la kuijadili kidogo.

Huyu Mch. Masanja anapitia wakati mgumu sana kipindi hiki kutokana na mtiririko wa matukio yaliyomtokea na hasa kadhia iliyojiri baada ya kifo cha Katibu wa Kanisa lake. Yamesemwa mengi na yeye ameongea mengi pia.
Kuna jambo ambalo naona jamii haijastukia nalo ni kutumika kwenye vita baina ya Masanja na wanaopambana naye.

Kuna jambo linalazimishwa ambapo ikifikia hatua watu kuitaka polisi ichukue hatua ya kumhoji Masanja na Mkewe kuhusu kifo kile. Hata baada ya ufafanuzi wa polisi kuhusiana na uchunguzi wa awali, lakini bado watu hao wenye malengo hasi wamehamia kwenye kuisambaratisha familia.

Inaonekana lengo kubwa ni kuhakikisha familia ya huyu mtumishi isiwe na utulivu hata wa kutafakari na kujirejeleza baada ya matukio haya waliyopitia.

PICHA
Hizi picha zinasambazwa kwa lengo mahsusi kumchafua ama kudhalilisha mwanamke na hata kumshambulia marehemu. Sisi leo tunajipa uhalali wa kuhukumu wakati tunajua kabisa kwa usahihi hatuna wema ama usafi wowote kiroho, kimawazo hata kitabia. Picha za mtoto zinasambazwa kama silaha ya kuhukumu na hata watetezi wa watoto wamekaa kimya.

Je lengo la wasambazaji ni kutaka mtoto adhuriwe? Inawezekana Masanja asifanye lolote kumdhuru mtoto. Je vipi kuhusu ndugu na washabiki wake? Je vipi ikiwa lengo la wanaosambaza hizi picha ni maandalizi ya kisaikolojia kwamba wamdhuru mtoto ili jumba bovu limuangukie Masanja?

Tujifunze kuwa na kiasi. Tuishi kwa kudumisha mila na desturi nzuri kwamba kumsema marehemu ni sasa na kumkaripia mtoto ambaye hajazaliwa bado. Tumsitiri huyu malaika wa Mungu kwani hapo baadaye akijakuwa mtu mzima na kukutana na stories zilizomchafua akiwa bado hajitambui anaweza kugeuka animal au akaathirika kisaikolojia.

Simtetei Masanja kwani hata mimi hapo mwanzo nilipeperushwa na upepo wa hawa wanaomchafua lakini nilipoona amezengumza neno la msamaha nikaanza kujenga picha namna jamii inavyoweza kujiponya kwa eneo la kusamehe na kuachilia. Msimkoseshe amani mke wake kwa sababu ya malengo maovu ya wanaomchafua.

Msimdhuru mtoto kwa kuharibu uwepo wake kupitia keyboards zetu.

Mungu wa Mbinguni awajaze hekima na awape kutafakari kisha kutenda yaliyo sahihi.
Atusamehe makosa yetu na kuponya magonjwa yetu
Atusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe waliotukosea
 

Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
9,119
5,383
mshauri masanja aache kumwanika mkewe kila mahali. Mke ni utupu wa mume, si sahihi kuuanika kila mahali, petrol stations, car wash, garage, ukiwa shopping, ukitibua/akitibua hata kidogo tu maneno lazima yawepo
 

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
13,369
10,778
mshauri masanja aache kumwanika mkewe kila mahali. mke ni utupu wa mume, si sahihi kuuanika kila mahali...petrol stations, car wash, garage, ukiwa shopping.....ukitibua kidogo una-attract maneno
Nadhani itakuwa faraja kumpotezea badala ya kuingilia uhuru wake.

Inabidi na kumpasa kila mmoja kuelewa kuwa uhuru hulinda utashi.
 

Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
9,119
5,383
Nadhani itakuwa faraja kumpotezea badala ya kuingilia uhuru wake.

Inabidi na kumpasa kila mmoja kuelewa kuwa uhuru hulinda utashi.
uko sahihi lakini hatuwezi kuwa na mtazamo mmoja. yeye mwenyewe anapaswa kujifunza kuwa kimya na masuala yake binafsi yawe private. Si kila anachofanya ikiwa ni pamoja na shughuli hata biashara zake, kilimo, mke etc kila mtu ajue.

Hakuna mwenye tabia kama ya masanja ya kuanika maisha yake hadharani aliyebaki salama. Hakuna.
 

Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
222,146
977,684
Kiki sasa hivi ni kalyinda,ya Masanja yamebaki kuwa suala la kifamilia. Ila mkewe kakonda sana daah maisha haya ni misuko suko anyway matatizo ni daraja.

Masanja ajifunze kuchunga mdomo wake ilikua too much, aige kwa mwenzie AY walishatosana na mkewe zamaaani ila wananzengo wakakosa cha kumsakamia maana hakua na maneno mengi ya kumpamba mkewe
 

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
17,467
27,283
uko sahihi lakini hatuwezi kuwa na mtazamo mmoja. yeye mwenyewe anapaswa kujifunza kuwa kimya na masuala yake binafsi yawe private si kila anachofanya hata biashara zake, kilimo, mke etc kila mtu ajue. Hakuna mwenye tabia kama ya masanja ya kuanika maisha yake hadharani aliyebaki salama. Hakuna...shetani yupo kazini kila wakati
Hizi kadhia ya viwango vya chini huwa sifuatilii lakini ninachojua ni kuwa ''If you don't live by the praises of men you won't die by their criticisms''. Unapofanya maisha yako ya binafsi kuwa wazi kwa umma, basi jiandae kuzomewa kwa mabaya yote yatakayokupata.
 

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
13,369
10,778
uko sahihi lakini hatuwezi kuwa na mtazamo mmoja. yeye mwenyewe anapaswa kujifunza kuwa kimya na masuala yake binafsi yawe private si kila anachofanya hata biashara zake, kilimo, mke etc kila mtu ajue. Hakuna mwenye tabia kama ya masanja ya kuanika maisha yake hadharani aliyebaki salama. Hakuna...shetani yupo kazini kila wakati
Kwa hiyo anaadhibiwa kwa sababu kidomodomo chake?
 
40 Reactions
Reply
Top Bottom