msaada wenu wandugu, huyu kaka tulisoma wote o-level hakuwai kusema chochote, baadae tumepotezana kwa miaka mingi, tulivoonana tena, akawa kama amechanganyikiwa kuniona, haamini. cha kwanza aliniuliza kama nimeolewa, nikamjibu bado, akasema "HATIMAYE NIMEMPATA MWANAMKE WA NDOTO ZANGU" nilimuuliza maana ya maneno yake alinijibu kuwa alinipenda toka tuko shule, nilipomuuliza kama ameoa, aliniambia amefunga ndoa na ana watoto wawili, nikamwambia siko tayari kuolewa naye na isitoshe siwezi kumuumiza mwanamke mwenzangu, alijibu "vyovyote itakavyokuwa ikiwezekana hata kumuacha nitamuacha maadam nimekupata tena" akadai ananipenda kuliko kawaida na nikimkataa nitamuaribia future yake. sasa, naombeni mnishauri jamani haya mambo yanaendaje?