ana hasira za kuogopesha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ana hasira za kuogopesha

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by jlm, Dec 28, 2009.

 1. jlm

  jlm Member

  #1
  Dec 28, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 29
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 5
  habarini za leo..
  nipo njia panda yani nahitaji msaada wa mawazo na nadhani hapa nitapata.
  nilikuwa na bf wangu kwa kama miaka miwili hivi baadae nikagundua ananicheat basi nikaamua tuachane sababu sikuona sababu ya kuendelea nae. basi nikaamua niwe single hadi nitapompata wa kunifaa,basi nikakaa kama mwaka mzima then mwaka huu mwezi wa pili nikapata bf mwingine kwakweli nimekuwa niki-enjoy sana huu uhusiano hakuna nisichopata kutoka kwake.
  sasa tatizo yule jamaa wa zamani akaanza kunisumbua anatuma msg zisizoeleweka nikamwabia aache huo ujinga akawa haelewi basi bf wangu akaziona zile msg siku moja nikamwambia ukweli na pia nilikuwa nilishamweleza kuhusu uhusiano wangu uliopita.
  akanielewa akasema mpige marufuku huyo mtu kutuma msg. basi yule ex akaacha kweli sasa akawa ananifuata physically hadi home mi nikampiga biti matata akatulia. sasa ghafla mwezi huu wa 12 akatuma msg nziiiito ya mapenzi akikumbushia enzi nzetu then anataka kuniona eti anakuja home.
  sasa bf wangu ndo alikuwa na simu yangu akaisoma ilivyoingia tu..basi kwa hasira akanipa nisome mimi moyo paa akauliza nani huyu sababu namba yenyewe nishadelete ingawa naikumbuka, nikamwambia atakuwa fulani..jamani nilishtukia pwaaaaaaaaa bonge la kibao cha shavu..nilizirai kuja kushtuka nipo massana hospital mbezi presha ipo juu sana na malaria 2. huyu mwenzangu ameniomba msamaha hadi uchozi tena mbele ya daktari mi nimemsamehe lakini jamani nipo njia panda hivi akinioa huyu si nitakula makonde hadi nife kabisa..jamani huyu ananifaa kweli?? kumpenda bado nampenda sana tu lakini kila akinishika uso nahofu yani nahisi kama anataka kunitwanga kibao..
   
 2. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,586
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Sasa ulitegemea nini kama mtu ameona msg ya mapenzi kutoka kwa ex-boyfriend? pili tangu muanze mahusiano umesema kuwa mlikuwa mkifurahi na hakuna ulichokosa kutoka kwake, sasa sioni hiyo njia panda unayoisema.!!! wewe endelea kuwa nae KAMA UNAMPENDA.
   
 3. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2009
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Huo ni wivu 2 aliokuwa nao bf wako na kama amekuomba msamaha msamehe, na pili umkanye huyo ex wako ache hiyo tabia ya kukutumia msg wakati wewe una mtu wako, huyo ex wako anajaribu juu chini kuharibu mahusiano mapya ulioyokuwa nayo ili muwe droo, hapendi ulivyo move on with your life.
   
 4. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...Safi sana, I hope hutawasilana tena na Ex-wako. Hata mimi ninge 'deliver same message!'.
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Pole na ukome kuwasiliana na ex wako.
  Cha msingi badili namba ya simu hiyo uliyo nayo hatokupata labda uamue kumpa mwenyewe.
  Kama anakufata ina maana unamuintatein
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kosa kubwa sana unafanya..Kwetu wanasema "Mtalaka hatongozwi", kwa maana kwamba muda wowote akikutaka anakulamba, maana may be hamkuachana shari yoyote!

  Utaua mahusiano yako haraka sana kwa mchezo huo!
   
 7. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Pole kwa kofi kubwa la kukufanya uzirai hata kufikishwa kwenye dhahanati. Hata hivo, kofi hilo linaonesha ni jinsi gani jamaa amewekeza moyoni kwake kwako wewe, kwenda kinyume na matarajio yake ni sawa na kumtwanga makofi ya kiroho yeye.

  Aidha hujaeleza ni mara ngapi alishawahi kukupiga kimtindo huo au kuelezea hasira zake kwa ubavu kwa jambo hilo hilo au jingine lolote lile katika mahusiano yenu, maana maelezo yako yaliyojificha yanaonesha kuwa hizo hasira zake si za mara moja.

  Yawezekana kabisa kuwa alisha kuasa kubadili namba na kutokuona text ya jamaa huyo tena lakini ukawa umekaidi kwasababu zako mwenyewe. Yawezekana ulikuwa unaonesha ku-entertain text za huyo jamaa ki-design na jamaa yako wa sasa akawa ameshitukia muda mrefu, hivyo alikuwa anasubirishia evidence tu. Yawezekana pia hiyo text iliyo prompt kofi hilo ilielezea mambo ya chumbani baina ya huyo wa zamani na wewe against huyo wa sasa, hivyo kuonesha kuwa ulikuwa unam-feed news za ndani jamaa yako wa zamani katika uhusiano mpya.

  Basi, kama hilo kofi limekuwa la kwanza na la mwisho, wewe msamehe, tafuta namba mpya na kuendeleza upendo wako kwake bila visasi vya kukumbushiana mambo yaliyopita, isitoshe ameshakuomba msamaha. Pia unaweza kujipanga gado na jamaa wawili au watatu hivi akiwemo mpenzi wako wa sasa na kumfungia safari huyo jamaa wa zamani. Hamna haja ya kumpatia kipigo cha mwizi wala nini, ila mnampa live akome na kuachana na wewe. Itafaa kama hiyo itakuwa mbele ya rafiki zake au hata familia yake kuonesha visa anavyofanya ili kuharibu uhusiano ulionao sasa.
   
 8. _ BABA _

  _ BABA _ JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2009
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  cha muhimu hapo ukitaka maliza hilo tatizo ni kubadili line ya simu yako au kuiblock hiyo namba ya xb kwa phone yako.
   
 9. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2009
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwambie wazi bila kuogopa kwamba mapenzi ya kupigwa pigwa wewe huyapendi wala huyataki kabisa. Akikupiga tena ndiyo utakuwa mwisho wenu na utaenda kumshtaki polisi kwa kukupiga na huyo daktari ambaye aliomba samahani mbele yako atakuwa shahidi wako.
   
 10. M

  Mende dume Member

  #10
  Dec 28, 2009
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dada yangu, kwanza sidhani kama hilo kofi ni kipimo sasa cha hasira. Andekuchekea baadaye ungemwona Bushoke, hizo ni salam tu za kawaida na hiyo kukuomba msamaha ni alama ni nyingine kwamba sio kama unavyomfikiria- that was msj and it is sent!
  Ushauri kama vipi cheki simu yenye akili, samsung wanafunction ya kublock simu kama unaona vipi unaiblock namba akituma msj haiingii and ur safe.

  kama anakupa kila utakacho ktk mapenzi- whatever that means, afu eti upo njia panda kwa kitu unachokijua ubaya wake. na wewe utakuwa kimeo! kwani yeye ukimkuta na msj za she- wake wa zamani anataka kuja, utasmile? kimsingi ni kuwa kakuwahi tu, wewe ndo ulipaswa kumtaka radhi.

  ukimbia huyo kwa hako kawivu kama mapenzi unakutana na kimeo kinakupa nusu ya mapenzi hayo afu kibano ni squared.

  kama kunaishu nyingine poa, mpige chini- kwangu mimi nadhani hamna ishu sana sana ulikuwa unatujulisha kuwa hupo available tuangalie utaratibu mwingine-senksi for zat- hujaacha mdogo homu, maana wengine ni MBA= Married But Available.

  senks again
   
 11. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #11
  Dec 29, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  jlm
  Junior Member
  [​IMG][​IMG][​IMG][​IMG] [​IMG] [​IMG]
  Join Date: Tue Dec 2009
  Posts: 4 <<<<<<
  Thanks: 0
  Thanked 1 Time in 1 Post


  Kazi kweli kweli......ila karibu sana
   
 12. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #12
  Dec 29, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  mh! hili suala gumu saana usichukulie suala la kuwashwa kibao kikubwa hivyo na BOYFRIEND kirahisi bibie,...hiyo inamaanisha ana matatizo katika ku control temper, kwenye ndoa kuna mambo mengi tu ya kuudhi na kutia hasira, hata wanaofuata kuvunja ndoa za watu kwa kufata fata wake za watu wapo kibao, ukisema umpe second chance kibao cha pili ...tatu nk kinaweza kukuta ndani ya ndoa hapo ndio utajikuta kwenye njia panda yenyewe hasa...

  fikiria kwa undani na umchunguze zaidi ukiona hasira zake hazieleweki eleeweki anza mbele kwa usalama wa maisha yako...
   
 13. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #13
  Dec 29, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..Ujengelele, demu kulambwa kofi mara moja moja ni sawa tu. Unajaribu kumkumbusha kuwa anatakiwa kujua yuko na mwanaume kwa hiyo heshima, adabu lazima iwepo.Haina maana unapompiga mwanamke ina maana humpendi wakati mwingine hawa mademu wana vijimambo fulani ambavyo bila ya kumkwangua kiganja atakusumbua...Pole kadadaaa!
   
 14. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #14
  Dec 29, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  HUYO BOIFRENDI ndiye aliyekubikiri?
   
 15. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #15
  Dec 29, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
   
 16. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #16
  Dec 29, 2009
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nina wasiwasi huyo new bf wako ni kutoka Tarime!
   
 17. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #17
  Dec 29, 2009
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kofi la mpenzi haliumi. Kibao kile kilimaanisha anakupenda ukomo na hataki kuona chakula chake kinaarandiwa na wengine. Makarangizo unayompa hataki mwingine aonje. Sasa ulitaka achekelee sms ya mahaba kutoka kwa dume lingine? Hata wanyama hawana utani katika suala hili. Hujaona majogoo wawili hawakai salama zizi moja?
  Leka
   
 18. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #18
  Dec 29, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,064
  Trophy Points: 280
  Going back to the previous guy would the stupidest thing to do. Just slog it on with the current guy kwani according 2 u he looks earnest and understanding kuhusu kibao thats just part of it kwani roll zingereverse ingekuaje????????
   
 19. MWAKISALU

  MWAKISALU Member

  #19
  Dec 14, 2013
  Joined: Nov 1, 2013
  Messages: 94
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 25
  Jlm ushauri wa ujengelele ni wa kipumbavu na nadhani kama ni mwanamke hataweza kuolewa na kama ataolewa hatokaa kwenye ndoa kabisa. Ukweli ni kwamba unamakosa makubwa sana tena sana. Wenzako makini kama ulikuwa na bf na ukaachana naye na ukajua ni msumbufu badilisha namba za simu. Huyu wa sasa ndiye dume lako shikiria sana hata kukuomba msamaha amefanya kosa we ndo ulitakiwa umuombe msamaha but kwa kuwa anakupenda hakuwa na jinsi. Mshikilie huyo man dada yangu
   
 20. foshizzle

  foshizzle JF-Expert Member

  #20
  Dec 14, 2013
  Joined: Dec 4, 2013
  Messages: 378
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ana bastola?
   
Loading...