Amwua Mwanaye Ili Aolewe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amwua Mwanaye Ili Aolewe!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by X-PASTER, Aug 31, 2011.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Aug 31, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Amwua Mwanaye Ili Aolewe!

  Polisi wilayani Bariadi mkoani hapa inamshikilia mwanamke mkazi wa kijiji cha Mwamabu wilayani humo kwa tuhuma za kumnyonga mtoto wake wa kumzaa ili aolewe.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Diwani Athumani, alisema ofisini kwake jana kuwa, Tabu Maimatha mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu ameuawa kikatili kwa kunyongwa na mama yake mzazi, akishirikiana na mpenzi wake, Kijiji Nyamagu ambaye alitoroka baada ya mauaji hayo.

  Alimtaja mwanamke huyo kuwa ni Limi Limbu (22) mkazi wa kijiji cha Mwamabu kata ya Bumera na kwamba tukio hilo lilitokea juzi saa saba za mchana kijijini hapo baada ya Limi kurubuniwa na mpenzi wake Nyamagu, kuwa wakimuua mtoto wake wataoana.

  Baada ya kukamatwa, Limi alikiri mbele ya polisi kuwa alishirikiana na mpenzi wake huyo kumwua mtoto wake, ili waishi kwa amani na waoane na kuanza maisha mapya katika ndoa yao.

  Inadaiwa Limi baada ya kukubaliana na mpenzi wake huyo walifanya kitendo hicho cha kikatili ili kuondokana na bughudha ya mtoto huyo wa nje ya ndoa na hivyo wazae watoto wao wa ndani ya ndoa.


  habariLeo
   
 2. Little Angel

  Little Angel JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Poor innocent kid!! Its so sad. Sasa hata kama angeishi nae angekua ana amani kuwa huyo mwanaume hatamwua na yy?
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Aug 31, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  huu ni ukatili wa kutisha!
   
 4. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Tumelithi kunyanyaswa na ccm sasa watu wameiga, tukitoka hapo tunaing'oa yenyewe. Pole mama siyo wewe ni ccm
   
 5. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Binaadamu wakati mwingine kama wanyama
   
 6. Amyner

  Amyner JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 2,404
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kweli ulee mimba kwa miezi 9, umzae mtoto, uishi nae mwaka na nusu ukutane tu na lijamaa likushawishi uue mwanao nawe ukubali tu!!! VERY CRUEL, EVIL, STUPID AND CRIMINAL!!!
   
 7. M

  Mr.creative JF-Expert Member

  #7
  Aug 31, 2011
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 504
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  akili zao za kichina
   
 8. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #8
  Aug 31, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Anastahili kila aina ya adhabu huyu mama
  Duh huo ukatili wa aina yake na kiumbe kimepata adhabu ambayo hakikustahili mungu amrehemu mtoto huyo
   
 9. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #9
  Aug 31, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Nimeshasikia case kama hizi saaan. Na si Tz tu hata nje ya nchi. Sielewi kama wahusika hasa yule ambaye mtoto ni wake wanakuwa kwenye akili timamu au vichaa.
   
 10. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #10
  Aug 31, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Nafikiri kunakuwa na kitu kama kuchanganyikiwa au vipi ila huu ni unyama wa hali ya juu
   
 11. kisute

  kisute Member

  #11
  Aug 31, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  shetani kamzidi akili kiasi cha kujikuta akimtumukia bila ya kujijua.
  Naye anastaili adhabu hiyo hiyo iwe fundisho kwa wale wote wazaao na kuua.
  Bora amtelekeze na sio kuua. Kapoteza kiongozi mzuri wa kesho. Balaa na zimwandame maisha yake yote na mungu amnyike mtoto maisha yake yote.
   
 12. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #12
  Aug 31, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  na yeye angeuawa tena kikatili, huyo ana roho ya kishetani kabisa.................
   
Loading...