Ampiga Mume wake kisa Kuichagua CCM

Ampiga Mume wake kisa Kuichagua CCM

AMPIGA MUMEWE KISA KUICHAGUA CCM

Na, Robert Heriel

Unaweza kufikiri ni utani, au mzaha au ni uongo, pengine wengine Mkafikiri ni Propaganda. Lakini ni ukweli kabisa. Mimi mwenyewe niliyeshuhudia sikuamini. Hivi mnaanzaje kupigana kisa vyama vya siasa, tena mnadundana haswa, mnachapana kikamilifu kisa na mkasa Uccm na Uchadema.

Jana Jioni, mida ya saa moja usiku, zimelika ngumi baina ya Mume na Mke hapa mtaani. Nimeshuhudia Mke akimkwida Mume wake na kumuachia kichapo kitakatifu. Hali iliyopelekea Mwanaume huyo kupoteza fahamu.

Ugomvi ulianza kama cheche za moto, na polepole ugomvi ulishika kasi mithili ya moto wa Petrol, sasa kila mmoja ungemuunguza kama angejaribu kuuzima.

Kisa kilianza baada ya Mume kutoka kazini akiwa kavaa Shati la CCM, sijajua cheo chake ndani ya chama hicho lakini shati lake pekee lilinitaarifu kuwa ni mwanachama wa kawaida tuu. Alipofika tuu nyumbani ambapo ni nyumba ya kupanga, Mpangaji mwezake(Mama jirani, mpangaji mwezake) akasema; CCM Hoyeee! Kisha mwanaume huyo akajibu kwa Bashasha huku uso wake ukijivunia kile alichokisikia, akajibu; Hoyeee! Hoyee! Wapinzani wataisoma Namba"

Punde Mke wake ambaye baadaye nilimtambua kama Mama D, akatoka chumbani na kusimama kwenye mlango kisha akimtazama mume wake aliyekuwa anaongea na mama wa chumba cha jirani. Mama D akasema; Wewe mwanaume huna akili kabisa. kisha akatukana matusi matatu aliyotabebanisha. Yalikuwa matusi mazito. Baba D kusikia hivyo akabaki anamtazama.

Alafu akasema; "Mke wangu ni lazima uipigie kura CCM, mimi ndiye Mume wako"

Hapo ndipo kizaazaa kikazaa matusi na mshikemkate. Mama D aliongea maneno mazito sana. Naomba niyanukuu hapa chini;

" Hiyo CCM imekusaidia nini tangu uijue, au hilo shati ulilovaa? eenhe! Unamiaka arobaini bado tumepanga, hatuna kiwanja wala shamba. Kodi yenyewe inatushinda, kodi ya 30,000/= kwa mwezi. Tunadaiwa hapa huu mwezi wa pili hatujalipa, wewe Shishiemu! Shishiemu(anabana pua) Watoto tumewakimbiza kijini kwa Bibi, wewe kwa ujuha wako hata hujielewi unaona mambo yapo sawa, walahi nilikosea kupata Mume"

Mama D anameza mate kisha anaendelea;
" CCM imekusaidia nini wewe? Yaani ungejua unavyonikera. Sijui jianaume gani usiojitambua. Unashindwa hata na wanawake, tena bora sisi wanawake wengi hatuna uwezo wa kuchanganua mambo, lakini sio kwa mwanaume. Hivi unafurahi kunikalisha nyumba za kupanga? kunilisha matembele na dagaa wa chukuchuku? CCM imefanya nini cha ziada?"

Baba D akapata mwanya akajibu, hapo wamesogeleana takribani hatua tano sasa.
"Sikiliza Mama D, CCM ndio imeleta maendeleo(anakatishwa)"
"Imekuletea wewe, au hiyo Tisheti yako ndio maendeleo? Hayo maendeleo uliyopewa na CCM mbona humu ndani hujawahi kuyaleta? Au ndio matembele yako unayoniletea humu kila siku?"

" Mama D! Mama D, wewe huoni maendeleo nchi hii, mpaka yaletwe nyumbani? Tazama ndege.....(anakatsihwa)"
" Akii! Mungu kanipa mkosi, huyu mume Mkosi. Ndege...! Ndege...! Wewe unamiaka mingapi hata Basi hujapanda? nakuuliza unamiaka mingapi hata hujapanda Basi tuu, mwaka wa tano sasa upo hapa hapa mjini unaranda randa, huna mbele wala nyuma. Basi kupanda linakushinda sembuse ndege, kodi ya chumba inakushinda ndege utaweza wewe?"
Mama D aliongea bila kumeza mate, aliongea kama chiriku, huku watu wakizidi kuongezeka kusikiliza malumbano ya wanandoa hao.

"Kwa hiyo mimi nisiposafiri wengine wasisafiri?" Baba D aliuliza kama swali analodhani litamuabisha Mke wake.

" Wengine kina nani, hapa Morogoro kina nani wanauwezo wa kupanda hizo ndege? Au ndugu zako? heeheee! Aloooh!(anacheka kishambenga). Ukoo wenu wote hakuna aliyewahi kupanda ndege, hapa mtaani hakuna aliyewahi kupanda ndege, uongo? au mwenzetu ushawahi kupanda?"

" Ona kwa sasa Elimu bure kuanzia elimu ya msingi mpaka sekondari, hilo hulioni Mama D, CCM imesaidia watu bhana"
Baba D alisema.

" Nilijua tuu utasema hilo, yaani wanaume wavivu bhana, yanafurahia mambo ya bure kama wanawake. Hivi elimu ya msingi na sekondari mtu akimaliza inamsaidia nini? Yaani Elimu ya msingi na Sekondari bure, alafu ya kusomea fani iwe gharama bado uisifu hiyo serikali" Mama D anameza mate, kisha anameza mate;

" Bora elimu ya chuo au Veta iwe bure kwa maana mtu anasomea fani, kama bure haiwezekani basi walau gharama ipunguzwe, au mkopo usio na riba utolewe. Lakini elimu ya msingi ambayo haya wewe mume wangu unayo ambayo haijakusaidia kitu, huna fani yoyote yaani upo upo tuu"

Hapo wakaingia ndani huku maneno yakiendelea, sisi wambeya tulikuwa bado hatujakubali kuondoka bila kuona mwisho wa mkasa huu.

"CCM Imejenga miundombinu, angalia barabara, embu tazama reli mpya hiyo Mke wangu, embu ona viwanda vipya, vijana wamepata ajira(anakatishwa)"
"Viwanda vya chereheni kweli vimeongezeka, hizo ajira wameajiriwa ukoo wenu siyoo! Nitajie ndugu yako yeyote aliyeajiriwa kwenye hivyo viwanda, ndugu zako wote nawafahamu, wewe mwenyewe Dalali, ukoo wa Kidalali, au viwanda vya udalali?"
Mama D alisema huku akipaliwa kwa kicheko.

" Sasa unafika mbali, mambo ya ukoo wetu achana nayo, ukoo wetu sio wakidalali"
" Kwani uongo, Wewe Dalali, shemeji X Dalali, Mzee wako alikuwa Dalali, mimi mkeo Dalali, hahahah! Damu ya kidalali.
Ndio maana hata akili yako imekaa kidalali, labda ungekuwa unabiashara ungenielewa?"
"Wewe hiyo biashara unayo?" Baba D aliuliza kwa sauti kavu.
" Mama na Baba yangu ni wafanyabiashara, kila siku wanalalamika, mdogo wangu kamaliza chuo hajaajiriwa, bado hujapata majibu ya kwa nini siipendi CCM?"

" Embu acha nipumzike, nimechoka!"
" Usiweke hilo shati lako humu ndani, nimevumilia ujinga wako miaka mingi, nimevumilia umasikini wako uliosababishwa na hao hao unaowatetea, miaka arobaini huna hata kibanda, unashindwa kulipa kodi ya chumba cha 30,000, unashindwa kulisha familia yako mpaka unapeleka watoto kwa wazazi, unashindwa kunitunza kwa upuuzi wako, yote nimevumilia lakini sitavumilia kuliona hilo shati lako humu ndani" Mama D alisema mara hii akiwa anamaanisha.

"Hii ni nyumba yangu, mimi ndio kichwa cha nyumba, usinipangie"
" Thubutuu! Nyumba yako si ungeringa, wanaume wengine kama machizi. Kama nyumba yako hiyo miezi miwili unayodaiwa kodi ni utopolo wako amaa!"

Hapo hapo wakashikana, walichapana haswa. Walipasuana, wakasagana. Kilichomsaidia Mama D ni mwili wake mkubwa wenye nguvu wenye asili ya Nyanda za juu kusini. Alimpiga mume wake huku akimtukana matusi ya nguoni. Mpaka anamuachia Baba D alikuwa kalala isijulikane kama amekufa ama amezimia. Mama D alipiga ukunga kuwa kaua, tulipofika ndani tulimkuta Baba D kalala kama Maiti inayosubiria kuoshwa. Kumkagua bado alikuwa mzima, mapigo yalikuwa chini sana kama beat ya muziki wa the Blues.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa huku kwetu uswahilini. Sasa sijajua Baba D akizinduka ataandika talaka au itakuwaje, lakini sikuwahijua kuwa kuna wanawake wanapiga hivi. Jamani, alipigwa haswa.

Sasa nauliza, inakuwaje mtu apigane na mwenza wake kisa masuala ya siasa?

Wewe unaona ni halali alichofanyiwa Baba D?
Je alichoongea Mama D ni sahihi?
Je alichoongea Baba D ni sahihi?

Mimi sijawahi kupanda ndege, hata ukoo wangu wote iwe kwa Baba au Mama haujawahi. Je vipi wewe na ukoo wenu, mliwahi?
Au huyu Mama D anatutafuta maneno?

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Hii ni tungo wala siyo tukio la kweli.
 
Mleta mada hujui faida ya ndege kwa mtu wa kawaida?

Kila tiketi ya ndege abiria anayonunua kuna kodi ya serikali.Hiyo kodi ndio inatumika kulipa mishahara ya wafanyakazi wa serikali nduguzo pia ndio inajenga zahanati,kutoa mikopo walimu ya juu,mikopo kwa akina mama na vijana ,kutengeneza barabara no

Faida ya ndege si tu kwa mpanda ndege!! Kodi ya kila tiketi ya mpanda ndege inamshukia mwananchi wa kawaida .N.a. hujusanywa ukikata tiketi tu

Chadema kwa hoja hizi mna safari ndefu ya wapiga kura kuwaelewa.
Mna hoja za Kyoto

Nenda usukumani hadi mtaani wanajua faida za ndege sababu hubeba samaki zao walizovua na wanazouza kupeleka Dar es salaam na nje ya nchi.

Ulichoandika cha kutunga halafu cha Kitoto kisicho na hoja
Acha upuuzi wako ilikuwaje shirika la ndege la mwanzo likafa ndege hazijazi abiria wa kutosha na biashara ya ndege ni ngumu sana sio kama akili yako ya kiccm inavyofikiria ifikie wakati tuongee ukweli sio kuleta mahaba ya kiccm,
Umesikia juzi tu south Africa shirika lake la ndege limefilisika hujiulizi kwa nini,

Hapo mtaani au wilaya yenu hapo kungeangaliwa ni nini kipo kiwanda kikajengwa si hata ndugu zako wangefaidika kuliko hao ndugu zako wanao landa landa mtaani,

Na sifa zenu za kujenga viwanda 60000 wakati nikipita sivioni sa sijui ni hii Tanzania au kuna Tanzania nyingine, kama ni hii ujinga wenu wa kuhesabu cherehani ya mtu unajumlisha ni kiwanda acheni ujinga..

Mwaka huu mnatoa ahadi za kutengeneza ajira 8,000,000
Upuuzi mtupu ajira 100,000 tu zinawashinda hizo millioni mtaweka mikakati ipi nyie majizi.
 
Acha upuuzi wako ilikuwaje shirika la ndege la mwanzo likafa ndege hazijazi abiria wa kutosha
Ilikuwa sababu ya ufisadi wa maofisa wa serikali wala rushwa na mawakala wa ndege wala rushwa na wafanyakazi wa ATCL wala rushwa
Tiketi walikuwa wakikata za Fast Jet na precision

Sasa hivi ufisadi umedhibitiwa.Ndege ya Fast Jet ilishafungashwa virago ambayo ilikuwa ya mafisadi

Sasa hivi ATCL inajaza
 
AMPIGA MUMEWE KISA KUICHAGUA CCM

Na, Robert Heriel

Unaweza kufikiri ni utani, au mzaha au ni uongo, pengine wengine Mkafikiri ni Propaganda. Lakini ni ukweli kabisa. Mimi mwenyewe niliyeshuhudia sikuamini. Hivi mnaanzaje kupigana kisa vyama vya siasa, tena mnadundana haswa, mnachapana kikamilifu kisa na mkasa Uccm na Uchadema.

Jana Jioni, mida ya saa moja usiku, zimelika ngumi baina ya Mume na Mke hapa mtaani. Nimeshuhudia Mke akimkwida Mume wake na kumuachia kichapo kitakatifu. Hali iliyopelekea Mwanaume huyo kupoteza fahamu.

Ugomvi ulianza kama cheche za moto, na polepole ugomvi ulishika kasi mithili ya moto wa Petrol, sasa kila mmoja ungemuunguza kama angejaribu kuuzima.

Kisa kilianza baada ya Mume kutoka kazini akiwa kavaa Shati la CCM, sijajua cheo chake ndani ya chama hicho lakini shati lake pekee lilinitaarifu kuwa ni mwanachama wa kawaida tuu. Alipofika tuu nyumbani ambapo ni nyumba ya kupanga, Mpangaji mwezake(Mama jirani, mpangaji mwezake) akasema; CCM Hoyeee! Kisha mwanaume huyo akajibu kwa Bashasha huku uso wake ukijivunia kile alichokisikia, akajibu; Hoyeee! Hoyee! Wapinzani wataisoma Namba"

Punde Mke wake ambaye baadaye nilimtambua kama Mama D, akatoka chumbani na kusimama kwenye mlango kisha akimtazama mume wake aliyekuwa anaongea na mama wa chumba cha jirani. Mama D akasema; Wewe mwanaume huna akili kabisa. kisha akatukana matusi matatu aliyotabebanisha. Yalikuwa matusi mazito. Baba D kusikia hivyo akabaki anamtazama.

Alafu akasema; "Mke wangu ni lazima uipigie kura CCM, mimi ndiye Mume wako"

Hapo ndipo kizaazaa kikazaa matusi na mshikemkate. Mama D aliongea maneno mazito sana. Naomba niyanukuu hapa chini;

" Hiyo CCM imekusaidia nini tangu uijue, au hilo shati ulilovaa? eenhe! Unamiaka arobaini bado tumepanga, hatuna kiwanja wala shamba. Kodi yenyewe inatushinda, kodi ya 30,000/= kwa mwezi. Tunadaiwa hapa huu mwezi wa pili hatujalipa, wewe Shishiemu! Shishiemu(anabana pua) Watoto tumewakimbiza kijini kwa Bibi, wewe kwa ujuha wako hata hujielewi unaona mambo yapo sawa, walahi nilikosea kupata Mume"

Mama D anameza mate kisha anaendelea;
" CCM imekusaidia nini wewe? Yaani ungejua unavyonikera. Sijui jianaume gani usiojitambua. Unashindwa hata na wanawake, tena bora sisi wanawake wengi hatuna uwezo wa kuchanganua mambo, lakini sio kwa mwanaume. Hivi unafurahi kunikalisha nyumba za kupanga? kunilisha matembele na dagaa wa chukuchuku? CCM imefanya nini cha ziada?"

Baba D akapata mwanya akajibu, hapo wamesogeleana takribani hatua tano sasa.
"Sikiliza Mama D, CCM ndio imeleta maendeleo(anakatishwa)"
"Imekuletea wewe, au hiyo Tisheti yako ndio maendeleo? Hayo maendeleo uliyopewa na CCM mbona humu ndani hujawahi kuyaleta? Au ndio matembele yako unayoniletea humu kila siku?"

" Mama D! Mama D, wewe huoni maendeleo nchi hii, mpaka yaletwe nyumbani? Tazama ndege.....(anakatsihwa)"
" Akii! Mungu kanipa mkosi, huyu mume Mkosi. Ndege...! Ndege...! Wewe unamiaka mingapi hata Basi hujapanda? nakuuliza unamiaka mingapi hata hujapanda Basi tuu, mwaka wa tano sasa upo hapa hapa mjini unaranda randa, huna mbele wala nyuma. Basi kupanda linakushinda sembuse ndege, kodi ya chumba inakushinda ndege utaweza wewe?"
Mama D aliongea bila kumeza mate, aliongea kama chiriku, huku watu wakizidi kuongezeka kusikiliza malumbano ya wanandoa hao.

"Kwa hiyo mimi nisiposafiri wengine wasisafiri?" Baba D aliuliza kama swali analodhani litamuabisha Mke wake.

" Wengine kina nani, hapa Morogoro kina nani wanauwezo wa kupanda hizo ndege? Au ndugu zako? heeheee! Aloooh!(anacheka kishambenga). Ukoo wenu wote hakuna aliyewahi kupanda ndege, hapa mtaani hakuna aliyewahi kupanda ndege, uongo? au mwenzetu ushawahi kupanda?"

" Ona kwa sasa Elimu bure kuanzia elimu ya msingi mpaka sekondari, hilo hulioni Mama D, CCM imesaidia watu bhana"
Baba D alisema.

" Nilijua tuu utasema hilo, yaani wanaume wavivu bhana, yanafurahia mambo ya bure kama wanawake. Hivi elimu ya msingi na sekondari mtu akimaliza inamsaidia nini? Yaani Elimu ya msingi na Sekondari bure, alafu ya kusomea fani iwe gharama bado uisifu hiyo serikali" Mama D anameza mate, kisha anameza mate;

" Bora elimu ya chuo au Veta iwe bure kwa maana mtu anasomea fani, kama bure haiwezekani basi walau gharama ipunguzwe, au mkopo usio na riba utolewe. Lakini elimu ya msingi ambayo haya wewe mume wangu unayo ambayo haijakusaidia kitu, huna fani yoyote yaani upo upo tuu"

Hapo wakaingia ndani huku maneno yakiendelea, sisi wambeya tulikuwa bado hatujakubali kuondoka bila kuona mwisho wa mkasa huu.

"CCM Imejenga miundombinu, angalia barabara, embu tazama reli mpya hiyo Mke wangu, embu ona viwanda vipya, vijana wamepata ajira(anakatishwa)"
"Viwanda vya chereheni kweli vimeongezeka, hizo ajira wameajiriwa ukoo wenu siyoo! Nitajie ndugu yako yeyote aliyeajiriwa kwenye hivyo viwanda, ndugu zako wote nawafahamu, wewe mwenyewe Dalali, ukoo wa Kidalali, au viwanda vya udalali?"
Mama D alisema huku akipaliwa kwa kicheko.

" Sasa unafika mbali, mambo ya ukoo wetu achana nayo, ukoo wetu sio wakidalali"
" Kwani uongo, Wewe Dalali, shemeji X Dalali, Mzee wako alikuwa Dalali, mimi mkeo Dalali, hahahah! Damu ya kidalali.
Ndio maana hata akili yako imekaa kidalali, labda ungekuwa unabiashara ungenielewa?"
"Wewe hiyo biashara unayo?" Baba D aliuliza kwa sauti kavu.
" Mama na Baba yangu ni wafanyabiashara, kila siku wanalalamika, mdogo wangu kamaliza chuo hajaajiriwa, bado hujapata majibu ya kwa nini siipendi CCM?"

" Embu acha nipumzike, nimechoka!"
" Usiweke hilo shati lako humu ndani, nimevumilia ujinga wako miaka mingi, nimevumilia umasikini wako uliosababishwa na hao hao unaowatetea, miaka arobaini huna hata kibanda, unashindwa kulipa kodi ya chumba cha 30,000, unashindwa kulisha familia yako mpaka unapeleka watoto kwa wazazi, unashindwa kunitunza kwa upuuzi wako, yote nimevumilia lakini sitavumilia kuliona hilo shati lako humu ndani" Mama D alisema mara hii akiwa anamaanisha.

"Hii ni nyumba yangu, mimi ndio kichwa cha nyumba, usinipangie"
" Thubutuu! Nyumba yako si ungeringa, wanaume wengine kama machizi. Kama nyumba yako hiyo miezi miwili unayodaiwa kodi ni utopolo wako amaa!"

Hapo hapo wakashikana, walichapana haswa. Walipasuana, wakasagana. Kilichomsaidia Mama D ni mwili wake mkubwa wenye nguvu wenye asili ya Nyanda za juu kusini. Alimpiga mume wake huku akimtukana matusi ya nguoni. Mpaka anamuachia Baba D alikuwa kalala isijulikane kama amekufa ama amezimia. Mama D alipiga ukunga kuwa kaua, tulipofika ndani tulimkuta Baba D kalala kama Maiti inayosubiria kuoshwa. Kumkagua bado alikuwa mzima, mapigo yalikuwa chini sana kama beat ya muziki wa the Blues.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa huku kwetu uswahilini. Sasa sijajua Baba D akizinduka ataandika talaka au itakuwaje, lakini sikuwahijua kuwa kuna wanawake wanapiga hivi. Jamani, alipigwa haswa.

Sasa nauliza, inakuwaje mtu apigane na mwenza wake kisa masuala ya siasa?

Wewe unaona ni halali alichofanyiwa Baba D?
Je alichoongea Mama D ni sahihi?
Je alichoongea Baba D ni sahihi?

Mimi sijawahi kupanda ndege, hata ukoo wangu wote iwe kwa Baba au Mama haujawahi. Je vipi wewe na ukoo wenu, mliwahi?
Au huyu Mama D anatutafuta maneno?

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Umeandika story ya kufikirika kama za akina willy gamba, ila unajitahidi,
Endelea hivyohivyo unaweza kuwa mwandishi wa story za kufikilika na ukapata pesa, usikate tamaa.
 
Mleta mada hujui faida ya ndege kwa mtu wa kawaida?

Kila tiketi ya ndege abiria anayonunua kuna kodi ya serikali.Hiyo kodi ndio inatumika kulipa mishahara ya wafanyakazi wa serikali nduguzo pia ndio inajenga zahanati,kutoa mikopo walimu ya juu,mikopo kwa akina mama na vijana ,kutengeneza barabara no

Faida ya ndege si tu kwa mpanda ndege!! Kodi ya kila tiketi ya mpanda ndege inamshukia mwananchi wa kawaida .N.a. hujusanywa ukikata tiketi tu

Chadema kwa hoja hizi mna safari ndefu ya wapiga kura kuwaelewa.
Mna hoja za Kyoto

Nenda usukumani hadi mtaani wanajua faida za ndege sababu hubeba samaki zao walizovua na wanazouza kupeleka Dar es salaam na nje ya nchi.

Ulichoandika cha kutunga halafu cha Kitoto kisicho na hoja
Inamaana zamani kabla ya bombadia, samaki walikuwa wanakula wenyewe .? au pia zilikuwa zinaenda nje .?
 
Nimekupata taikun
 
Mleta mada hujui faida ya ndege kwa mtu wa kawaida?

Kila tiketi ya ndege abiria anayonunua kuna kodi ya serikali.Hiyo kodi ndio inatumika kulipa mishahara ya wafanyakazi wa serikali nduguzo pia ndio inajenga zahanati,kutoa mikopo walimu ya juu,mikopo kwa akina mama na vijana ,kutengeneza barabara no

Faida ya ndege si tu kwa mpanda ndege!! Kodi ya kila tiketi ya mpanda ndege inamshukia mwananchi wa kawaida .N.a. hujusanywa ukikata tiketi tu

Chadema kwa hoja hizi mna safari ndefu ya wapiga kura kuwaelewa.
Mna hoja za Kyoto

Nenda usukumani hadi mtaani wanajua faida za ndege sababu hubeba samaki zao walizovua na wanazouza kupeleka Dar es salaam na nje ya nchi.

Ulichoandika cha kutunga halafu cha Kitoto kisicho na hoja
Mbona CAG kazuiwa kukagua ATCL..hakuna faida ni show off za kishamba na 10% za manunuzi
 
AMPIGA MUMEWE KISA KUICHAGUA CCM

Na, Robert Heriel

Unaweza kufikiri ni utani, au mzaha au ni uongo, pengine wengine Mkafikiri ni Propaganda. Lakini ni ukweli kabisa. Mimi mwenyewe niliyeshuhudia sikuamini. Hivi mnaanzaje kupigana kisa vyama vya siasa, tena mnadundana haswa, mnachapana kikamilifu kisa na mkasa Uccm na Uchadema.

Jana Jioni, mida ya saa moja usiku, zimelika ngumi baina ya Mume na Mke hapa mtaani. Nimeshuhudia Mke akimkwida Mume wake na kumuachia kichapo kitakatifu. Hali iliyopelekea Mwanaume huyo kupoteza fahamu.

Ugomvi ulianza kama cheche za moto, na polepole ugomvi ulishika kasi mithili ya moto wa Petrol, sasa kila mmoja ungemuunguza kama angejaribu kuuzima.

Kisa kilianza baada ya Mume kutoka kazini akiwa kavaa Shati la CCM, sijajua cheo chake ndani ya chama hicho lakini shati lake pekee lilinitaarifu kuwa ni mwanachama wa kawaida tuu. Alipofika tuu nyumbani ambapo ni nyumba ya kupanga, Mpangaji mwezake(Mama jirani, mpangaji mwezake) akasema; CCM Hoyeee! Kisha mwanaume huyo akajibu kwa Bashasha huku uso wake ukijivunia kile alichokisikia, akajibu; Hoyeee! Hoyee! Wapinzani wataisoma Namba"

Punde Mke wake ambaye baadaye nilimtambua kama Mama D, akatoka chumbani na kusimama kwenye mlango kisha akimtazama mume wake aliyekuwa anaongea na mama wa chumba cha jirani. Mama D akasema; Wewe mwanaume huna akili kabisa. kisha akatukana matusi matatu aliyotabebanisha. Yalikuwa matusi mazito. Baba D kusikia hivyo akabaki anamtazama.

Alafu akasema; "Mke wangu ni lazima uipigie kura CCM, mimi ndiye Mume wako"

Hapo ndipo kizaazaa kikazaa matusi na mshikemkate. Mama D aliongea maneno mazito sana. Naomba niyanukuu hapa chini;

" Hiyo CCM imekusaidia nini tangu uijue, au hilo shati ulilovaa? eenhe! Unamiaka arobaini bado tumepanga, hatuna kiwanja wala shamba. Kodi yenyewe inatushinda, kodi ya 30,000/= kwa mwezi. Tunadaiwa hapa huu mwezi wa pili hatujalipa, wewe Shishiemu! Shishiemu(anabana pua) Watoto tumewakimbiza kijini kwa Bibi, wewe kwa ujuha wako hata hujielewi unaona mambo yapo sawa, walahi nilikosea kupata Mume"

Mama D anameza mate kisha anaendelea;
" CCM imekusaidia nini wewe? Yaani ungejua unavyonikera. Sijui jianaume gani usiojitambua. Unashindwa hata na wanawake, tena bora sisi wanawake wengi hatuna uwezo wa kuchanganua mambo, lakini sio kwa mwanaume. Hivi unafurahi kunikalisha nyumba za kupanga? kunilisha matembele na dagaa wa chukuchuku? CCM imefanya nini cha ziada?"

Baba D akapata mwanya akajibu, hapo wamesogeleana takribani hatua tano sasa.
"Sikiliza Mama D, CCM ndio imeleta maendeleo(anakatishwa)"
"Imekuletea wewe, au hiyo Tisheti yako ndio maendeleo? Hayo maendeleo uliyopewa na CCM mbona humu ndani hujawahi kuyaleta? Au ndio matembele yako unayoniletea humu kila siku?"

" Mama D! Mama D, wewe huoni maendeleo nchi hii, mpaka yaletwe nyumbani? Tazama ndege.....(anakatsihwa)"
" Akii! Mungu kanipa mkosi, huyu mume Mkosi. Ndege...! Ndege...! Wewe unamiaka mingapi hata Basi hujapanda? nakuuliza unamiaka mingapi hata hujapanda Basi tuu, mwaka wa tano sasa upo hapa hapa mjini unaranda randa, huna mbele wala nyuma. Basi kupanda linakushinda sembuse ndege, kodi ya chumba inakushinda ndege utaweza wewe?"
Mama D aliongea bila kumeza mate, aliongea kama chiriku, huku watu wakizidi kuongezeka kusikiliza malumbano ya wanandoa hao.

"Kwa hiyo mimi nisiposafiri wengine wasisafiri?" Baba D aliuliza kama swali analodhani litamuabisha Mke wake.

" Wengine kina nani, hapa Morogoro kina nani wanauwezo wa kupanda hizo ndege? Au ndugu zako? heeheee! Aloooh!(anacheka kishambenga). Ukoo wenu wote hakuna aliyewahi kupanda ndege, hapa mtaani hakuna aliyewahi kupanda ndege, uongo? au mwenzetu ushawahi kupanda?"

" Ona kwa sasa Elimu bure kuanzia elimu ya msingi mpaka sekondari, hilo hulioni Mama D, CCM imesaidia watu bhana"
Baba D alisema.

" Nilijua tuu utasema hilo, yaani wanaume wavivu bhana, yanafurahia mambo ya bure kama wanawake. Hivi elimu ya msingi na sekondari mtu akimaliza inamsaidia nini? Yaani Elimu ya msingi na Sekondari bure, alafu ya kusomea fani iwe gharama bado uisifu hiyo serikali" Mama D anameza mate, kisha anameza mate;

" Bora elimu ya chuo au Veta iwe bure kwa maana mtu anasomea fani, kama bure haiwezekani basi walau gharama ipunguzwe, au mkopo usio na riba utolewe. Lakini elimu ya msingi ambayo haya wewe mume wangu unayo ambayo haijakusaidia kitu, huna fani yoyote yaani upo upo tuu"

Hapo wakaingia ndani huku maneno yakiendelea, sisi wambeya tulikuwa bado hatujakubali kuondoka bila kuona mwisho wa mkasa huu.

"CCM Imejenga miundombinu, angalia barabara, embu tazama reli mpya hiyo Mke wangu, embu ona viwanda vipya, vijana wamepata ajira(anakatishwa)"
"Viwanda vya chereheni kweli vimeongezeka, hizo ajira wameajiriwa ukoo wenu siyoo! Nitajie ndugu yako yeyote aliyeajiriwa kwenye hivyo viwanda, ndugu zako wote nawafahamu, wewe mwenyewe Dalali, ukoo wa Kidalali, au viwanda vya udalali?"
Mama D alisema huku akipaliwa kwa kicheko.

" Sasa unafika mbali, mambo ya ukoo wetu achana nayo, ukoo wetu sio wakidalali"
" Kwani uongo, Wewe Dalali, shemeji X Dalali, Mzee wako alikuwa Dalali, mimi mkeo Dalali, hahahah! Damu ya kidalali.
Ndio maana hata akili yako imekaa kidalali, labda ungekuwa unabiashara ungenielewa?"
"Wewe hiyo biashara unayo?" Baba D aliuliza kwa sauti kavu.
" Mama na Baba yangu ni wafanyabiashara, kila siku wanalalamika, mdogo wangu kamaliza chuo hajaajiriwa, bado hujapata majibu ya kwa nini siipendi CCM?"

" Embu acha nipumzike, nimechoka!"
" Usiweke hilo shati lako humu ndani, nimevumilia ujinga wako miaka mingi, nimevumilia umasikini wako uliosababishwa na hao hao unaowatetea, miaka arobaini huna hata kibanda, unashindwa kulipa kodi ya chumba cha 30,000, unashindwa kulisha familia yako mpaka unapeleka watoto kwa wazazi, unashindwa kunitunza kwa upuuzi wako, yote nimevumilia lakini sitavumilia kuliona hilo shati lako humu ndani" Mama D alisema mara hii akiwa anamaanisha.

"Hii ni nyumba yangu, mimi ndio kichwa cha nyumba, usinipangie"
" Thubutuu! Nyumba yako si ungeringa, wanaume wengine kama machizi. Kama nyumba yako hiyo miezi miwili unayodaiwa kodi ni utopolo wako amaa!"

Hapo hapo wakashikana, walichapana haswa. Walipasuana, wakasagana. Kilichomsaidia Mama D ni mwili wake mkubwa wenye nguvu wenye asili ya Nyanda za juu kusini. Alimpiga mume wake huku akimtukana matusi ya nguoni. Mpaka anamuachia Baba D alikuwa kalala isijulikane kama amekufa ama amezimia. Mama D alipiga ukunga kuwa kaua, tulipofika ndani tulimkuta Baba D kalala kama Maiti inayosubiria kuoshwa. Kumkagua bado alikuwa mzima, mapigo yalikuwa chini sana kama beat ya muziki wa the Blues.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa huku kwetu uswahilini. Sasa sijajua Baba D akizinduka ataandika talaka au itakuwaje, lakini sikuwahijua kuwa kuna wanawake wanapiga hivi. Jamani, alipigwa haswa.

Sasa nauliza, inakuwaje mtu apigane na mwenza wake kisa masuala ya siasa?

Wewe unaona ni halali alichofanyiwa Baba D?
Je alichoongea Mama D ni sahihi?
Je alichoongea Baba D ni sahihi?

Mimi sijawahi kupanda ndege, hata ukoo wangu wote iwe kwa Baba au Mama haujawahi. Je vipi wewe na ukoo wenu, mliwahi?
Au huyu Mama D anatutafuta maneno?

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Ni kama vile story ya kutunga, hahahahaha Ila katamu hakana party 2 tuendelee kujua serikali imezalisha vilaza % ngapi kwenye utawala huu..
 
Ilikuwa sababu ya ufisadi wa maofisa wa serikali wala rushwa na mawakala wa ndege wala rushwa na wafanyakazi wa ATCL wala rushwa
Tiketi walikuwa wakikata za Fast Jet na precision

Sasa hivi ufisadi umedhibitiwa.Ndege ya Fast Jet ilishafungashwa virago ambayo ilikuwa ya mafisadi

Sasa hivi ATCL inajaza
Walio sababisha huo ufisadi wamechukuliwa hatua gani, mbona mahakama kuu 'division ya ufisadi' imejaa vumbi?
 
Watu wa aina ya baba Diii wapo wengi sanaa.

Hatujapandishwa madaraja tangu 2014./mishahara haijaongezwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom