Kyoma
Senior Member
- Jun 2, 2006
- 101
- 86
Mkandara,
I wish ningekuwa Mzee ES. Huyo Sam nilimsikia sikuwahi kusoma maandishi yake. Lakini jamaa yule alikuwa maarufu sana. Mzee ES nimempenda kwa sababu ni Honest. Mkiwa na jamii ya watu wenye kuelezea mawazo yao bila kuona haya, nirahisi kuweka masuala mezani kuliko wale wanopitisha mgomo baridi.
Si umeona Mzee ES anasema viongozi wa CCM wanaogopa kusema hadharani kuwa Salim wanampinga kwa sababu ya uarabu wake? Utamu wa demokrasia siyo matokeo ya kura. Ni zile taratibu zinazotumika kuwapata wagombea, kuandikisha wapiga kura, kupiga kampeni, elimu kwa wapiga kura, na zoezi zima la upigaji kura. Watashi wanafupisha na kusema due process.
Sasa kama due process ya kumpata mgombea wa CCM, na vigezo vilivyotumika inakuwa ni jando, basi wanajua kuwa vigezo vyao siyo kwa manufaa ya taifa. Kama ni kwa manufaa ya taifa, inabidi ielezwe kwa msisitizo wa hali ya juu ili hata mtoto mchanga aelewe. Si kwa manufaa ya taifa bwana? sasa tunaficha nini? kwa nini wanaona haya kusema hadharani kuwa hatupendi waarabu?
Hivi CCM si walikuwa vinara na hasa kututia umaskini kutokana na sera zao za kupinga ubaguzi wa aina yoyote barani Afrika na dunia nzima. Au zilikuwa ni sera za Nyerere? Si wale wale akina Mkapa ndiyo walikuwa wakiziuza nchi za nje mpaka kikaeleweka? Au walikuwa hawajapata akili timamu. Ni lini wamebadilisha sera yao? Au ndiyo mambo ya unafiki?
Ni vizuri kubadili sera, itikadi, na mitizamo katika maisha, huna haja ya kuwaeleza watu kama misimamo yenyewe ulikuwa unafanyia bafuni wakati unaoga. Lakini CCM wametueleza msimamo wao juu ya ubaguzi wa rangi miaka nenda rudi. Wanaposhushiwa na mwangaza wa roho mtakatifu na kubadilika, inabidi watueleze ati! kwa nini waliamini yale waliyotuaminisha na kitu gani kimewafanya wabadilike na kuamini haya mapya. Si chama tawala? Umuhumi wa CCM kwa hili unatokana na udhoofu wa vyama vya upinzani, Mwalimu aliwahi kusema kuwa unapomtangaza mgombea uraisi wa CCM, si ajabu ukawa unamtangaza Raisi wa nchi. Ndiyo maana due process zao ni muhimu kwa mustakabali wa nchi yetu.
Kificho cha vigezo kinaashilia uhuni. Huu ndiyo utamadunu tunaotaka kuujenga. Mimi nadhani watu tuupinge bila kujali itikadi zetu za vyama. Hakuna jando kwenye mambo ya nchi. Hawa wasioweza kusema hadhalani kuwa ni wabaguzi, wataweza kusema kuwa ni wezi au wala rushwa? Mzee ES ebu nisaidie hapa.