Millad Ayo do somethingHabari Wakuu, heri ya Sikukuu ya Mapinduzi...................
Awali ya yote napenda kusema mimi ni moja ya vijana wachache hapa mjini ambao bado tuko "very loyal" kwa radio hii maarufu ya Clouds Fm. Despite vipindi vya redio hii pendwa kwa vijana (kwa mujibu wa IPSOS 2015), kujaa matangazo ya biashara na content zisizo na tija kwa Taifa, ni nadra sana kwa mimi kukosa kusikiliza vipindi vya "Amplifier" by Millard Ayo, "Sports Extra" na "Nambie" kwa Zaidi ya miaka saba sasa, pengine sababu content ya vipindi hivi vinaendana na character yangu.
Ni kama wiki mbili au tatu zimepita tangu Dada huyu Amina Ally aliekuwa akifanya vizuri sana katika kipindi cha "Nambie" aanze kusika hewani katika kipindi cha Amplifier akiwa na Millard Ayo. Nilipomsikia kwa mara ya kwanza nilifurahi na kuhuzunika kwa pamoja. Nilifurahi nikijua kipindi kitakuwa kizuri Zaidi maana mafundi wawili wamekutana, na nilihuzunika na kuwa na hofu kidogo nikidhani pengine soon Millard Ayo atakiacha kipindi hiki na hivyo Amina Ally anaandaliwa kama replacement.
Cha ajabu tangu Dada huyu aingie kwenye kipindi hiki, amekua hovyo kweli, anacheka cheka bila msingi na kuleta stori zisizoendana na flow ya kipindi. Kwa kifupi amekuja kuiharibu Amplifier na kuifanya ishindwe kueleweka kwa wasikilizaji makini kama mimi. Nahisi Millard Ayo ameshaligundua hili ila anashindwa tu kumchana yule dada.
Nashauri program manager wa "Mawingu FM" kulitazama hili kwa jicho la tatu maana yule dada kawa kero kabisa na kipindi kinamshinda katika Nyanja zoote na ikiwezekana arudishwe kwenye kipindi chake cha zamani.
Nimewasilisha mawazo ya wengi ambao wanakerwa na uwepo wa dada huyu kweny kipindi hiki kupitia platform hii nikiamini taarifa hii itawafikia Clouds Media Group.
Wekeni hapa Picha ya Amina Ally tumuone ndio mjadala utakuwa mzuri.... maneno mengi ya nini
Hivi hakutokea huko EA Radio??Of course yule Amina Ally angefaa aende East Africa Radio wana kipindi flani ambapo wanacheka cheka kile cha kina Sam Misago
May be ametokea ile radio ya ya ubiaHivi hakutokea huko EA Radio??
Inaitwa Choice fmMay be ametokea ile radio ya ya ubia
102.5FM Dar es Salaam
Hahahahahahhh, I wish kangekua hapa kakaona jinsi kanavowakosea watu, pengine kangejirekebishaNimeacha kusikiliza kipindi kutokana na kukereka kwa vicheko na kupayuka kwa huyu Dada.Yani utafikiri anashindana na Millard...shemeji shemeji nyingii!Ananikera binafsi na anasumbua masikio yangu.
Hakana mpangilio kanaruka ruka tu na kupayuka.Mchomvu naye sifa nyingiiii!Lugha yake haina mvuto tena na swagga zake naona kama zimepitwa na wakati.
Hahahahab....Asante Mkuu kwa kunirekebisha.Kuna dokta mmoja yuko pale,MD,labda mpaka apelekewe maiti kutoka muhimbili pale pale studio,otherwise walitakiwa wawe na yaliyojiri-post-mortem.
Ikishindikana Mimi ntawakusanya masela tutinge pale studio na jeneza la mwili wa marehemu kwa ajili ya postmortem
Wanamuita Meena - Anyway ngoja nikuelezee kwanini walimuweka pale.. East Africa Radio wana The cruise kuna Queen Fifi na yule jamaa watu wengi sana ikifika mida ile huwa wanasikiliza sana East Africa Radio kutokana na Amplifier kupwaya na kua na matangazo 10000 ingawa ndipo hela inaingia wakaona wa mlete ili wawe kama Ea Radio..
2- Inasemekana Amplifire ilikuwa inafanyaka nyumbani kwa Ayo na kurekodiwa na kutumwa studio alafu Faraja (producer) akawa ana play vipande kuringana na news (Ayo yuko busy na ujenzi wa taifa) katika station yoyote huwa kuna classfied adverts ambazo huwa zinasomwa hapo hapo wakati kipindi kinaendelea sasa zile zilishindwa kusomwa kwa sababu Ayo hayupo kwa io wakaona ni dharau hii kwa vile kijana ameona amefahamika kaanza dharau.. Wakamfuata Meena Bbc waka panda dau mazaga kede kede mkataba wakampa wakaja kumuweka hapo bila Ayo kufahamu siku ikafika akaambiwa utakua unafanya kipindi na uyu bidada wakampa na stress zingine.. Imebidi jamaa (ayo) avunje utaratibu wa zamani sa ivi kipindi kinafanyika studio (clouds) na hawezi kumuelekeza njia kuringana na maisha ya utangazaji yalivo
huu ubuyu kabisaaa