Amepigwa paka, jirani analalamika

Amepigwa paka, jirani analalamika

Void ab initio

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2015
Posts
5,739
Reaction score
5,703
Habari ndugu wa humu ndani.
Hapa ninapoishi huwa kuna mapaka huwa yanakuja usiku yanalia kama watoto. Jana usiku mtoto wa mpangaji wangu amepiga paka mmoja jiwe, sasa jirani yangu amekuja asubuhi kushitaki na analalamika kuwa vijana wangu wanapiga watu mawe.
Hivi inakuwaje anapigwa paka halafu anaumia mtu ?

*Hebu wajuzi mnijuze, hii inakuwaje*
 
kwaiyo wasiambiwe? waache paka wa watu kama hamuwapendi hameni
 
Mapepo hayo,yanatumwa kwako ktk umbo la paka.be careful!..pray more,seek GOD more
 
Habari ndugu wa humu ndani.
Hapa ninapoishi huwa kuna mapaka huwa yanakuja usiku yanalia kama watoto. Jana usiku mtoto wa mpangaji wangu amepiga paka mmoja jiwe, sasa jirani yangu amekuja asubuhi kushitaki na analalamika kuwa vijana wangu wanapiga watu mawe.
Hivi inakuwaje anapigwa paka halafu anaumia mtu ?

*Hebu wajuzi mnijuze, hii inakuwaje*
Akili zetu tumezizika kwenye imani mbovu za kishirikina mpaka tunashindwa kuona logic simple kabisa! Kama walivyo watoto wadogo inawezekana kabisa katika kurusha mawe yalikuwa yanapitiliza na kuangukia uani au karibu na mji wake. Sasa unataka akae kimya? Nakumbuka tulivyokuwa wadogo tulikuwa tunanyang'anywa manati ili tusipige watu wakati tunapowinda ndege!
 
Huenda jiwe lilivuka mpaka njiani, angejuaje kama inapigwa paka
 
Mnawaonea paka bure kwa imani zenu za kishirikina. Paka wanapolia usiku ni dalili kwamba wanataka kupandana, sasa kwanini muwapige mawe?
 
Mnawaonea paka bure kwa imani zenu za kishirikina. Paka wanapolia usiku ni dalili kwamba wanataka kupandana, sasa kwanini muwapige mawe?
Mkuu watu bongo zimeota kutu kwa ushirikina. Halafu wanajifanya hawajui kuwa watoto wanapotupa mawe ovyo kuwapiga paka wanahatarisha usalama wa watu wengine kwani jiwe linaweza kupitiliza na likaumiza!
 
Mwambie kijana wako aache kupiga watu mawe hasa wakiwa kwenye shughuli zao.....hapa kazi tu
 
Sasa nimeamia mtaa wa saba toka pale nilipokuwa nimekaa zaman ile nyumban co nyumban!!!!!
 
Akili zetu tumezizika kwenye imani mbovu za kishirikina mpaka tunashindwa kuona logic simple kabisa! Kama walivyo watoto wadogo inawezekana kabisa katika kurusha mawe yalikuwa yanapitiliza na kuangukia uani au karibu na mji wake. Sasa unataka akae kimya? Nakumbuka tulivyokuwa wadogo tulikuwa tunanyang'anywa manati ili tusipige watu wakati tunapowinda ndege!
Hivii umemuelewa alicho sema! Kuwa kunapaka wa jirani kapigwa jiwe na mtoto wa mpangaji, na aliekuja kulalamika jiran kasema mtoto huyo anapiga watu wake so hayo ni mambo ya kishirikina na usitake kuiaminisha imani yako na mtoa mada alivyoelezea.
 
Unaishi kwenye Jamii ya wazee wa busara.

Hamia mtaa wa saba.
 
Hivii umemuelewa alicho sema! Kuwa kunapaka wa jirani kapigwa jiwe na mtoto wa mpangaji, na aliekuja kulalamika jiran kasema mtoto huyo anapiga watu wake so hayo ni mambo ya kishirikina na usitake kuiaminisha imani yako na mtoa mada alivyoelezea.
Wewe ndio hujaelewa nilichoandika kwasababu ubongo wako umeshangamizwa na kutu ya ushirikina! Ni kawaida kabisa watoto wanaporusha mawe kupiga mnyama/wanyama kama paka walioko kwenye makazi ya watu kujeruhi watu kwa bahati mbaya. Yeye anaweza kuwa alikuwa anamlenga paka aliyekuwa kwenye ukuta au kichaka lakini kwa nyuma kuna makazi au mtu! Tuache imani potofu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom