Ambwene Mwasongwe kwa sasa ndiyo icon ya nyimbo za injili

Mwalimu wa tuisheni

JF-Expert Member
Oct 19, 2019
5,467
8,565
Habari za jioni wana jamvi, nimekua nikimfuatilia huyu mwimbaji wa nyimbo za injili kwa miaka mingi sana.

Huyu jamaa kwa sasa ndiyo icon ya nyimbo za injili utunzi wake ni wakipekee sana, nyimbo zake zimetulia mno, natamani waimbaji wote wamtafute wajue nini siri ya mafanikio kwenye uimbaji wake

Baadhi ya nyimbo zake ni

  • Nimekumbukwa
  • Mwana wa Azali
  • Upendo wa kweli
  • Natamani sana
 
kuna nif

kuna ile nifundishe kuomba
 
Nabarikiwa Sana na nyimbo zake hasa wimbo wa TULIKOTOKA

"Mengine yalikuja kama mema
Mwisho ukawa mbaya
Mengine yalikuja kama mabaya
Kumbe yanakusudi
Lakini katika yote hayo
Tulikuona Bwana
Ukitetea maisha yetu
Dhidi ya hatari mbaya"
Kwakweli
 
Niliona mahali ame comment upuuzi kwenye hoja ya kweli...
Nikajua yuko kidini na kikanuni zaidi badala ya kuwa kiroho kama walivyokuwa mafarisayo washika sheria
Aah okay
Nimekusoma
Km Bado ana mambo ya udini ashafeli
 
Binafsi namuona ni mwimbaji wa kawaida sana kwenye injili. Uimbaji wake mwingi ni ule ule, anaimba hadithi zake binafsi tu alizozipa melody (huenda ni true story lakini nyingi hazipo ndani ya Biblia). Sioni kama ana kidhi kuwa Icon wa muziki wa gospel.

Kiujumla Ambwene Mwasongwe ni mburudishaji na sio muinjilishaji. Yule ni Bahati Bukuku aliyechangamka.
 
Back
Top Bottom