Ambaye ana uzoefu na biashara za Dar-Zanzibar

Niko katika mchakato wa kuangalia fursa za kibiashara maeneo tofauti tofauti ila nimefikia muda wa tathmini ya biashara Zenji.

Nina hamu ya kujua biashara ambazo zinashamiri za kutoka Dar kwenda Zanzibar hasa za vyakula. Naomba ushirikiano wenu ili niweze kupata tathmini halisi ya mambo ya changamoto, gharama na kodi ikibidi kwa wazoefu.

Biashara nayolenga mojawapo ni ya kusafirisha mayai ya jumla. Kutoka Dar to Zenji. Karibuni.
Mayai hapana ndg.. zenji kuna wafugaji wa kuku had vijijin kabisa msee.. wanafuga hao layer kwa wingi.. may be ya kienyeji.

Vitunguu, nyanya, mabonga ni deal sana mzee sema kuna misimu yake, hasa mwez wa 11 wa 6 kwa nyanya na vtunguu, maboga peleka kipnd cha ramadhan utakuja nshukuru.
 
Ni kweli mkuu ata wa shinyanga ni mzuri Ila wa kyela ni special, ule ukipika nyumba nzima inanukia wali, tofauti kidogo na mchele mwingine mtu kujua kama Unatoa hashimu lungwe hadi aone umepalia Moto juu ya mfuniko

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa hv sio kyela tena ni Kamsamba ndio wana mchele mzur ila kyela inatumika kuibrand tu ila kwa watu wa mbeya ndio wanaulizia hyo kamsamba ndio unanukia sana alaf mtamu sana mdomoni.
Na wafanyabiashara wengi wanachanganya na mchele wa Mbarali ili wapate faida mara dufu.
 
Back
Top Bottom