Mambo ya muhimu katika kukuza biashara (business diversification)

MrProsecutor

JF-Expert Member
Jun 12, 2017
281
274
Ciao famiglia, come stai?

Leo tuongelee kidogo kuhusu business diversification. Ulimwengu wa sasa katika ushindani wa biashara, diversification ni key mojawapo ya kukufanya uendelee kukua zaidi na kuwa imara sokoni. Diversification ni pamoja na kuongeza wigo wa biashara kwa kuIntroduce bidhaa mpya, kuexplore fresh market ama kuexpand georgraphical.

Diversification haipunguzi tu hasara kwa maana ukiInvest sehemu tofauti tofauti sio rahisi kupata hasara sehemu zote, yani huwezi kuwa na biashara tatu af zote zikawa znakupa hasara tu, inawezekana pia if haujafanya diversification kwa kutumia akili. Faida nyingine ni kuongeza mapato/vyanzo vipya vya hela. So now tuangalie vitu viwili muhimu kabisa katika diversification,.

1. AINA YA DIVERSIFICATION

Kuna aina nyingi lakini ntaongelea tatu tu ambazo ni product diversification (kuongeza bidhaa mpya au huduma mpya katika biashara uliyonayo, mfn kama unauza ubuyu tu ukaanza kutengeneza na juice ya ubuyu etc.), Market diversification (hapa ni kuingia katika soko jipya mfn umezoea kuuza vinywaji baridi ukaamua sasa kuingia soko jipya uanze kuuza nguo), Geographic diversification (Biashara yako iko Dar tu sas unaamua kufungua branches nje ya dar ama nje ya nchi, kimsingi ni kwenda zaidi ya eneo ulilopo kibiashara ukifanya biashara ile ile)

2. CHALLENGES & SUCCESS

Hii ni sehemu muhimu zaidi ambayo wetu wengi huisahau wanapofanya diversifications kwenye biashara. Diver.. ina challenges na risk zake muhim sana kuzingatia. Fanya research ya kutosha na uandae strategies nzuri ambazo utaingilia sokoni, jifunze kwenye biashara za watu wengine jinsi walivyofanya mpaka wakafanikiwa kudiversify vizuri na wakafanikiwa. Mfn Bakhresa Group ilianza na vyakula lakini wako na Usafiri, wako na fintech, wako na media etc..

MUHIMU KABLA SIJAMALIZA
Hakikisha biashara unayofanya imekuwa stable sana kias kwamba unapata faida nzuri na hata ikitokea unaanzisha biashara mpya kwa kutumia faida hiyo haitaathiri chochote ili kuepuka kufunga biashara zote.
Thanks & nice weekend fam.
 
Shida yetu unakuta biashara mtu ipo in ideation stage badala ya mtu akazane idea ije into real life anakuwa na idea zaidi ya kumi halafu kichwa kimoja
Ni vyema kabla mtu hajaingia/kufikiria idea nyingine ahakikishe ile ya kwanza imesimama
 
Nataka kuhamisha biashara kutoka sehemu flani kwenda mjini je naweza fainikiwa ni biashara ya accessories maana nilipo haiendi kabisa huu mwaka wa tatu unaweza maliza wiki bila wateja
Fanya uchunguzi wa kutosha juu ya bidhaa unayouza, ubora wake, muhimu zaidi wajue wateja wako ni wakina nani na hali zao za vipato zikoje. Mfno unaweza kuwa unauza mafuta mazuri sana ya nywele na yanamatokeo mazuri sana na target ni wadada ukienda fungua hii duka kijijini kweli kuna wadada lakini vipato vyao(spendings) haziko kwnye urembo ziko kwenye basic needs so sio rahisi kuuza.
Angali eneo ulilopo lina kasoro gani au wewe ndo unakasoro, je eneo unalotaka kwenda lina tofauti gani na ulipo, je waliopo eneo unalotaka kwenda wanafanya biashara kama yako matokeo yakoje etc. I hope umepata pakuanzia kufkiria upya.
 
Nataka kuhamisha biashara kutoka sehemu flani kwenda mjini je naweza fainikiwa ni biashara ya accessories maana nilipo haiendi kabisa huu mwaka wa tatu unaweza maliza wiki bila wateja
Ila jamaa wewe ni mvumilivu sana startup ya ndoa itakufaa sana
Wiki bila wateja kwa miaka mitatu bado upo tu???? Mimi zikipita siku mbili bila mteja siku ya tatu iwe jua iwe mvua watapatikana tu
 
Nataka kuhamisha biashara kutoka sehemu flani kwenda mjini je naweza fainikiwa ni biashara ya accessories maana nilipo haiendi kabisa huu mwaka wa tatu unaweza maliza wiki bila wateja
Ukihamishia dsm nishtue...Nkufanyie marketing kwa makubaliano lakini.
 
Back
Top Bottom