Amani yetu ndiyo maendeleo yetu,tutailinda daima.

Amani yetu ndiyo maendeleo yetu,tutailinda daima.

nkoge

Member
Joined
Jun 7, 2018
Posts
53
Reaction score
90
Angalizo...!

Hii siyo Id mpya kama wachache wasiofikri vyema, ambao yeyote kwao anayeongelea amani na utulivu kwenye jamii wanamgeuza kuwa adui. Niko hapa tangu 2018.

Binafsi nimechagua kuwa balozi wa amani wa kujitegemea. Sijawahi kupewa chochote na kiongozi yeyote na hata mahusiano na viongozi Sina maana kulingana na shughuli zangu ni ngumu kuonana nao,lakini nimechagua amani.

Kuna watu wanafikri kutukana Kila kitu humu jukwaani, wakifikri Kuna faida ya hayo,l akini kumbe wanapoteza muda bila kujua kuwa kundi kubwa la wananchi linapenda utulivu,nikiwemo na Mimi.

Bila amani na utulivu kwenye taifa, hakuna usafiri,hakuna shule,hakuna hospitali na hakuna biashara Wala internet inayowawezesha kutukana watu majukwaani Kila wakati.

Tuendelee kudumisha amani na utulivu wetu ili tujenge maendeleo yetu. Wale mnaoishi Kwa mashemeji zenu mtusamehe tuna majukumu ya msingi ya kutafutia mkate familia zetu.Kwa hiyo tunahitaji utulivu na ustaarabu katika kutimiza hayo.
 
CCM NI WAPUMBAVU SANA MKUU, LAKINI NITAKUJIBU KWA KIFUPI ANAEVUNJA UTULIVU/AMANI NI....

1. Anayeteka watanzania Wenzetu akina Soka, Polepole, Mdude, Chaula nk.

2. Anayepiga watu Risasi Akina TUNDU LISSU, SATIVA AKWILINA MAWAZO NK

3. Anayezuia haki ya Kikatiba ya Mikutano ya Vyama vya siasa.
(Kushiriki mikutano ya hadhara na Mikutano ya ndani.

4. Anayezuia Maandamano ambayo ni haki ya kikatiba ya Tanzania.

5. Anayezuia na Kupora Haki ya watanganyika ya kuchagua kiongozi wanaye mtaka.

6.Anayeficha Kila aina ya mikataba, Bandari,Umeme,Gas, Ardhi Madini nk nk.

7. Anayekandamiza uhuru wa vyombo vya Habari
mitandao ya kijamii JF, TwiterX, nk
CCM WAMETUONA WATANGANYIKA NI MALOFA SANA


AMKENI WATANGANYIKA
 
Back
Top Bottom