Amani Karume: Nilishangaa wana-CCM wenzangu wanahofia wapinzani kushinda, Uchaguzi 2015 Zanzibar nilisikitika, niliwauliza hawa wenzetu si Watanzania?

View attachment 2002168

Rais huyo Mstaafu wa Zanzibar amedai kwamba miongoni mwa mambo ambayo yamemsononesha na ambayo hatokuja kuyasahau kamwe ni hili la Jecha Salum Jecha kufuta matokeo halali ya uchaguzi wa 2015 , huku wao wakiwa kwenye vikao na Maalim Seif vya kujadili hatima ya Zanzibar .

Amewashangaa wanaccm kuogopa kuongozwa na Wapinzani .
CCM ni walewale sema tu ameamua kuzuga
 
View attachment 2002168

Rais huyo Mstaafu wa Zanzibar amedai kwamba miongoni mwa mambo ambayo yamemsononesha na ambayo hatokuja kuyasahau kamwe ni hili la Jecha Salum Jecha kufuta matokeo halali ya uchaguzi wa 2015 , huku wao wakiwa kwenye vikao na Maalim Seif vya kujadili hatima ya Zanzibar .

Amewashangaa wanaccm kuogopa kuongozwa na Wapinzani .
Mungu akuongezee umri na afya tele.....wachache sana tena wqlioonja keki ya Taifa ukiweza kusema ukweli wa moyo....blessed Baba na mwana mko fikra huru
 
Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume amesema miongoni mwa mambo yaliyowahi kumsikitisha ni kuitishwa kwa uchaguzi wa marudio mwaka 2015, wakati wakiwa kwenye kikao cha kujadili yaliyotokea katika uchaguzi huo akisema yeye alikuwa miongoni mwa wajumbe wa CCM waliokuwa wakifanya majadiliano na Maalim Seif baada ya uchaguzi ili kujua hatma ya Zanzibar.

Uchaguzi huo ulifutwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) wakati huo Mwenyekiti wake akiwa Jecha Salim Jecha aliyeamua kufuta matokeo yaliyokuwa yakiendelea kutangazwa kisha ukatangazwa uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 2016 ambao Maalim Seif aliususia.

"Nilishangaa hata wana CCM wenzangu wanahofia wapinzani kushinda, niliwauliza kwani hawa wenzetu si Watanzania? Hawataki haki na usawa? Niliwaambia Maalim Seif ni mtu muungwana kuliko hata walivyokuwa wakimuona na kumpa majina mabaya"-Karume.
Mbali ya kutosema hadharani tokea wakati huo juu ya dhulma hiyo, je alichukuwa hatua gani kama mmoja wa viongozi ndani ya chama chake ambacho kilifanya dhulma ya aina hiyo? Je ameendelea kuwa kwenye nafasi yake ndani ya chama ama alijiweka pembeni kupinga kwa vitendo juu ya dhulma hiyo? Je aliye dhulumiwa alikuwa ni maalim seif ama ni wananchi wa zanzibar akiwemo na yeye mzee karume?
 
Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume amesema miongoni mwa mambo yaliyowahi kumsikitisha ni kuitishwa kwa uchaguzi wa marudio mwaka 2015, wakati wakiwa kwenye kikao cha kujadili yaliyotokea katika uchaguzi huo akisema yeye alikuwa miongoni mwa wajumbe wa CCM waliokuwa wakifanya majadiliano na Maalim Seif baada ya uchaguzi ili kujua hatma ya Zanzibar.

Uchaguzi huo ulifutwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) wakati huo Mwenyekiti wake akiwa Jecha Salim Jecha aliyeamua kufuta matokeo yaliyokuwa yakiendelea kutangazwa kisha ukatangazwa uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 2016 ambao Maalim Seif aliususia.

"Nilishangaa hata wana CCM wenzangu wanahofia wapinzani kushinda, niliwauliza kwani hawa wenzetu si Watanzania? Hawataki haki na usawa? Niliwaambia Maalim Seif ni mtu muungwana kuliko hata walivyokuwa wakimuona na kumpa majina mabaya"-Karume.
Shetani akizeeka anageuka kuwa malaika
 
Walao kikubwa ameyasema akiwa yeye binafsi bado yupo hai na CCM kama taasisi inayolea huo uharamu bado ipo madarakani,amechelewa lakini ametimiza wajibu wake wa kuweka wazi na umma umemsikia
Kwa nini hakusimama na kuyapinga hayo hadharani wakati yalipo fanyika? Kwa nini hakukiri hadharani kwamba serikali iliyopo madarakani (kwa wakati huo) ilikuwa serikali haramu? Kwa nini ayaseme hayo miaka 6 baadae, tena baada ya mwenye kudhulumu na aliye dhulumiwa kufariki?
 
Haya maneno huwa wanayasema baada ya kustaafu, siwaamini, yale yale ya Mkapa kitaka Katiba Mpya kwenye kitabu chake baada ya kustaafu.

Hata Karume binafsi asingekubali kushindwa na Seif na angetumia njia yoyote kuhakikisha anashinda.
Kuna maneno kutoka vijiwe vya gahawa kuwa kuna mmoja Kati ya sheni au karume alikubali matokeo ya kushinda kwa sababu alisema kudhulumu matokeo kwa mujibu wa dini yake ni dhambi,na yeye haitaki dhambi hiyo.
Nasikia Mkapa na konvoi lake wakatua visiwani kwenda kumchana live,
Baada ya kichano hicho akatanganzwa kuwa mshindi.
Vijiwe vya gahawa bana!
 
Huyu mbona alimaliza Urais wake kabla ya 2015, wakati huo Rais alikuwa Dr Shein ambaye ndiye baada ya kufutwa kwa matokeo na uchaguzi kurudiwa alishinda awamu ya pili na kuendelea kuongoza.
Nilisha sahau kama jecha S. Jecha ilikuwa kwa shein nae hakutaka kulikemea hilo
 
Amani aka HAPA PANGU ni mnafik mkubwa! Hata awamu zote alizogombea yeye Maalim seif alisema ameshinda uchaguzi je ilikuwa kweli?
 
Back
Top Bottom