Amani Karume: Nilishangaa wana-CCM wenzangu wanahofia wapinzani kushinda, Uchaguzi 2015 Zanzibar nilisikitika, niliwauliza hawa wenzetu si Watanzania?

Jagina

JF-Expert Member
Jan 29, 2019
999
500
UINGEREZA ndiyo iliyokuja kumsaidia baba wa taifa hayati JKN baada ya mapinduzi yale.....

UINGEREZA ileile iliyokuwa BOSS wa JAMSHID.....UINGEREZA ileile iliyomsimamia Jemshid "aeneze Uislam Zanzibar" ndiyo iliyokuja tena kumsaidia BABA WA TAIFA HAYATI JKN.....

Ni uingereza haohao WAANGLIKANA na si WAKATOLIKI.....

Tupende kudadavua mambo kwa upana na mawanda yake......

Binadamu hana ADUI na RAFIKI wa kudumu........huo ndio ukweli wenyewe na ndio maana JAMSHID na familia yake yuko hifadhini Uingereza......na kule kwao Oman Muscat.....ni haohao WAINGEREZA waliompa nguvu baba yake hayati sultan Qaboos,hayati Qaboos mwenyewe na huyu wa sasa......

Lete ushahidi muingereza alimsimamia Jemshid aeneze uislamuu Zanzibar

Unajifanya kukimbia ki Aina swali,
Wale wasomi waliomtoa makosa Padri Peter Smith
Ni Nani Na makosa yapi ?

Usisahau jukumu ulilopewa Na mungu la kulinda muungano
 

Mtoto wa Shule

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
8,126
2,000
Hiyo ni hali aliyokuwa anaitaka miaka mingi,awe Rais angalau apate nafasi ya kuikwamua Zanzibar,na alijaribu kufanya mambo mengi bila kuyashirikisha haya maccm bara. Lakini mambo mengi pia aliyoyawazia kuikwamua Zanzibar alikwamishwa na miccm bara
Labda nikwambie kitu. Kuanzia babaake Mzee Abeid Amani Karume na yeye Amani Abeid Amani Karume wote waliitegemea zaidi CCM kwa mustakabali wa maisha yao ya kisiasa kuliko CCM ilivyowategemea wao. Sana sana CCM imewatumia sana kwa faida yake. Na hata leo ( and mark my words), Family ya Karume is NOTHING bila back up ya CCM and they (Karume Family) knows it! Need I say more?
 

Wakulonga

JF-Expert Member
Oct 29, 2012
757
1,000
View attachment 2002168

Rais huyo Mstaafu wa Zanzibar amedai kwamba miongoni mwa mambo ambayo yamemsononesha na ambayo hatokuja kuyasahau kamwe ni hili la Jecha Salum Jecha kufuta matokeo halali ya uchaguzi wa 2015 , huku wao wakiwa kwenye vikao na Maalim Seif vya kujadili hatima ya Zanzibar .

Amewashangaa wanaccm kuogopa kuongozwa na Wapinzani .
Hivi huyu mzee kasahau yeye ndio sababu wazanzibar kuwawa kule pemba mwaka 2001. Atulie nae dawa imungie
 

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
11,111
2,000
Huu unafiki tu. Kwanini yeye hakupave hizo political roads wakati alipokuwa Rais?
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
30,382
2,000
Umerudia mara nyingi sana kusema "Waarabu Wapemba..."

Hao "Waarabu Wapemba" ni Waarabu wa aina gani, na wanatofautiana vipi na Waarabu wengine?

Btw, kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa inawezekana tu pale madarakani anapokuwa Mwarabu... kwani hiyo Serikali ya Umoja wa Kitaifa ilianza wakati madarakani akiwa Mwarabu yupi, na ikafa wakati yupo Mswahili Mweusi yupi?!

Hivi unaijua historia ya ZNZ kweli wewe?!

Karume aliuawa na Waarabu au aliuawa kutokana na utawala wake wa kidikteta?!

Au unata ukumbushwe ni namna gani alivyokuwa na hofu dhidi ya wanachama wa Umma Party kwa sababu tu, miongoni mwao walikuwa wasomi waliotukuka kuliko yeye, na pia wenye mitazamo ya kikomunisti!!

Yaani tuanze kukumbushana jinsi alivyokuwa anawaweka ndani wale aliokuwa anawaona threat kwake, na wengine kuwapeleka bara?!

Au nianze kukupa darasa hapa kwamba, watu wa mwanzo kabisa kuleta mgawanyiko ni Wanazi wa ASP ambao walikuwa Waafrika Weusi?

Hao uliowataja walisumbuliwa na Waarabu gani?! Usitolee mfano wa akina Maalim Seif ambao walifikia hadi kutimuliwa kwa sababu hata Jumbe, native African nae alitimuliwa kwa sababu zile zile ambazo zilipelekea Maalim Seif kutimuliwa!

Yaani Othman Masoud hana lolote?! Hivi unawajua vizuri hawa watu wewe?

Mauaji ya kutisha kule Pemba yalitokea wakati rais akiwa nani? Alikuwa hao unaowaita Waswahili Weusi "wanaouchukiwa na waarabu wa Pemba" au alikuwa hao unaowaita Waarabu?!
Jumbe alitimuliwa sababu ya fitna ya Mwarabu Mpemba Maalim Seif aliyemfitini ili ashike yeye baadaye CCM wakagundua Maalim Seif nyoka ndie anasababisha waswahili ngozi nyeusi wasitawale kwa amani Zanzibar wakamtumua
 

Jagina

JF-Expert Member
Jan 29, 2019
999
500
Jumbe alitimuliwa sababu ya fitna ya Mwarabu Mpemba Maalim Seif aliyemfitini ili ashike yeye baadaye CCM wakagundua Maalim Seif nyoka ndie anasababisha waswahili ngozi nyeusi wasitawale kwa amani Zanzibar wakamtumuaInaelekea


Huo uarabu ulimpa wewe ???, ulikuwepo alipomfitini ?? Sikushangai labda wapemba walikupa ile kitu mbaya ambayo kwako ni nzuri

wjd-billboard-born-gay.jpg

1636436590631.jpeg
 

Kamakabuzi

JF-Expert Member
Dec 3, 2007
2,451
2,000
Wakiwa madarakani wanakuwa vipofu wa akili? au wakishatoka hawataki wenzao nao wafaidi?
Kwa madaraka aliyo kuwa nayo wakati ule, angesimama kidete kutetea msimamo wake huu wa sasa, kweli Zanzibar ingekuwa mbali, na Tanganyika nayo labda ingesalimika
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
12,679
2,000
Jumbe alitimuliwa sababu ya fitna ya Mwarabu Mpemba Maalim Seif aliyemfitini ili ashike yeye baadaye CCM wakagundua Maalim Seif nyoka ndie anasababisha waswahili ngozi nyeusi wasitawale kwa amani Zanzibar wakamtumua
Kuna maswali kadhaa ya msingi nimekuuliza lakini umeyakwepa...

Na umeyakwepa kwa sababu allegation zako hazina msingi wowote!!

Na tukija hilo la "kumfitini", je alegations dhidi ya Jumbe zilikuwa za kupikwa au sahihi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom