Amani Karume: Nilishangaa wana-CCM wenzangu wanahofia wapinzani kushinda, Uchaguzi 2015 Zanzibar nilisikitika, niliwauliza hawa wenzetu si Watanzania?

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,311
2,000
Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume amesema miongoni mwa mambo yaliyowahi kumsikitisha ni kuitishwa kwa uchaguzi wa marudio mwaka 2015, wakati wakiwa kwenye kikao cha kujadili yaliyotokea katika uchaguzi huo akisema yeye alikuwa miongoni mwa wajumbe wa CCM waliokuwa wakifanya majadiliano na Maalim Seif baada ya uchaguzi ili kujua hatma ya Zanzibar.

Uchaguzi huo ulifutwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) wakati huo Mwenyekiti wake akiwa Jecha Salim Jecha aliyeamua kufuta matokeo yaliyokuwa yakiendelea kutangazwa kisha ukatangazwa uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 2016 ambao Maalim Seif aliususia.

"Nilishangaa hata wana CCM wenzangu wanahofia wapinzani kushinda, niliwauliza kwani hawa wenzetu si Watanzania? Hawataki haki na usawa? Niliwaambia Maalim Seif ni mtu muungwana kuliko hata walivyokuwa wakimuona na kumpa majina mabaya"-Karume.
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
112,186
2,000
Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume amesema miongoni mwa mambo yaliyowahi kumsikitisha ni kuitishwa kwa uchaguzi wa marudio mwaka 2015 ,wakati wakiwa kwenye kikao cha kujadili yaliyotokea katika uchaguzi huo akisema yeye alikuwa miongoni mwa wajumbe wa CCM waliokuwa wakifanya majadiliano na Maalim Seif baada ya uchaguzi ili kujua hatma ya Zanzibar.
:
Uchaguzi huo ulifutwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) wakati huo Mwenyekiti wake akiwa Jecha Salim Jecha aliyeamua kufuta matokeo yaliyokuwa yakiendelea kutangazwa kisha ukatangazwa uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 2016 ambao Maalim Seif aliususia.

"Nilishangaa hata wana CCM wenzangu wanahofia wapinzani kushinda, niliwauliza kwani hawa wenzetu si Watanzania? Hawataki haki na usawa? Niliwaambia Maalim Seif ni mtu muungwana kuliko hata walivyokuwa wakimuona na kumpa majina mabaya"-Karume.
Huyo tangu mwanzo alionyesha utofauti na maccm wenzake lkn hilo halimuondolei kuwa ni mwana ccm
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
12,679
2,000
Hivi wale wana-CUF ambao waliuawa kule ZNZ back in 2001, na wengine kukimbilia uhamishoni; ilikuwa ni awamu ya nani?!

Sawa, tutambebesha zigo la misumari Mkapa kwa hoja kwamba ndie alipeleka polisi ZNZ kwenda kuua wana-CUF, na pia Karume bado alikuwa mgeni kwenye kiti lakini miezi michache ambayo alishakuwa madarakani ingemwezesha kugomea ukatili ule!!

Hayo majadiliano yalikuja baada ya CUF kuwa wameshauawa, na baada ya hapo hali ya ZNZ ikasambaratikavibaya mno!!

Zanzibar watu wakawa hawazikani!!

Visima vya maji vikawa vinajazwa vinyesi!!

Hata ulipoitishwa uchaguzi mwingine wa Wabunge, CUF "wakasusia" na Maalim akahamasisha Wafuasi wake wakapige kura za Maruani!!

2005 JK alipoingia madarakani bado hali ilikuwa mbaya Zanzibar!

JK, bila shaka kwa kutumia uzoefu wake wa kidiplomasia, ndipo akaunda Tume ya Maridhiano na kuitishwa Kura ya Maoni!

Kupitia kura za maoni ndipo Mfumo wa Utawala ZNZ ukabadilishwa na kuleta mfumo wa Serikali ya Mseto!! Na ndipo pia muundo wa Tume ya Uchaguzi ZNZ nao ukabadilishwa (ingawaje haujaleta suluhu) ili Wajumbe wake wawe wanatoka kwenye chama tawala na upinzani!

Lakini pamoja na kubadilisha mfumo wa ZEC, bado CCM wameendelea kubananga chaguzi ZNZ!

Kwahiyo tusidanganyane.!!

Hakuna mwana-CCM anayependa upinzani waingie Ikulu unless kama kushinda wanakoweza kuvumilia wengine ni ule ushindi wa ubungeTU lakini linapokuja suala la urais... WOTE, HAWAPO TAYARI KUONA WAPINZANI WANASHINDA!!!
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
8,807
2,000
Haya maneno huwa wanayasema baada ya kustaafu, siwaamini, yale yale ya Mkapa kutaka Katiba Mpya kwenye kitabu chake baada ya kustaafu.

Hata Karume binafsi asingekubali kushindwa na Seif na angetumia njia yoyote kuhakikisha anashinda.
 
Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
21,474
2,000
Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume amesema miongoni mwa mambo yaliyowahi kumsikitisha ni kuitishwa kwa uchaguzi wa marudio mwaka 2015, wakati wakiwa kwenye kikao cha kujadili yaliyotokea katika uchaguzi huo akisema yeye alikuwa miongoni mwa wajumbe wa CCM waliokuwa wakifanya majadiliano na Maalim Seif baada ya uchaguzi ili kujua hatma ya Zanzibar.

Uchaguzi huo ulifutwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) wakati huo Mwenyekiti wake akiwa Jecha Salim Jecha aliyeamua kufuta matokeo yaliyokuwa yakiendelea kutangazwa kisha ukatangazwa uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 2016 ambao Maalim Seif aliususia.

"Nilishangaa hata wana CCM wenzangu wanahofia wapinzani kushinda, niliwauliza kwani hawa wenzetu si Watanzania? Hawataki haki na usawa? Niliwaambia Maalim Seif ni mtu muungwana kuliko hata walivyokuwa wakimuona na kumpa majina mabaya"-Karume.
Wao ndio watanzania wengine sio🤣🤣
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom