Ama kweli Duniani kuna magumu ya kuamua

Ama kweli Duniani kuna magumu ya kuamua

kwa wakati ule ulifanya vyema hukutaka kumuumiza yeyote japo mama alitegemea ungemtetea yeye zaidi. mkuu isha kuwa historia haina haja ya kuumiza kichwa fanya nafasi yako ya kuwaheshimu na kuwapenda na kuwahudumia pale inapobidi pia usisahahu kuwaombea Mungu awafungue macho.. mkuu ni swala la mda tu soon wataelewa hakuna haja ya kujipendekeza .
Nimekuelewa miss chaga mtani wangu bila kupepesa macho.

Ishakuwa historia ndio but ni kama ile ya walioshiriki(nchi) vita vya Dunia wengine until now wanamadeni duhh
 
Nimekuelewa miss chaga mtani wangu bila kupepesa macho.

Ishakuwa historia ndio but ni kama ile ya walioshiriki(nchi) vita vya Dunia wengine until now wanamadeni duhh
hilo haliwafanyi wao kuendelea na maisha yao mkuu
 
Mkuu, binafsi naona kunakitu ulikifanya ambacho ndo chanzo cha yote...

KUSALITI kiapo, ukwel uliujua Na uliapa kusema ukwel lakin hukufanya hivyo, Kama ungesema ukweli hata mkosaji ingefikia hatua akakubali kuwa alikosea Na Maisha yangeendelea..

Sasa hapo unatafunwa Na dhambi ya usaliti..!
Unahukumiwa Na nafsi

Uliapa kwa bible so hapo tayar ulihusisha imani hivyo jaribu kuwatafuta wataalam wa imani uliyonayo wakusaidie jins ya kufuta dhambi hiyo..!
 
2008 umemaliza la saba na una demu, na uandishi wako huu!!!mbona kama mzee zaidi ya hapo???

Sasa nawe kwa akili yako ukamning'iniza faza ako???.pale ungeweka mpira kati,bila kufungamana na upande wowote.maana mpaka sasa sjui nani alikusomesha.
Ukisoma vzt post ya jamaa,nna uhakika utaedit hii post yako.

Soma vzr kabla hujapost mkuu.
 
Mbona hapo kulikuwa hamna shida sema inaonekana ulikuwa na mahaba kwa mama-wewe ungesema ukweli tu,na kama msma ndio mwenye makosa ushahidi usingejitosheleza na kesu ingefutwa kiufupi ww ndio umesababisha baba yako afungwe ndio maana hadi leo unajisitukia kwa kutotenda haki
 
Mkuu, binafsi naona kunakitu ulikifanya ambacho ndo chanzo cha yote...

KUSALITI kiapo, ukwel uliujua Na uliapa kusema ukwel lakin hukufanya hivyo, Kama ungesema ukweli hata mkosaji ingefikia hatua skakubali kuwa alikosea Na Maisha yangeendelea..

Sasa hapo unatafunwa Na dhambi ya usaliti..!
Unahukumiwa Na nafsi

Uliapa kwa bible so hapo tayar ulihusisha imani hivyo jaribu kuwatafuta wataalam wa imani uliyonayo wakusaidie jins ya kufuta dhambi hiyo..!
Somo jipya tena hapa naibuka nalo dah......

Kweli wakat naapa roho ilinikandamiza kweli kusema uhalisia ilaa mhhhhhh ilikuwa ngumu kumeza kama ya clauds fm michezo.

.Aysee ngoja kwanza nitafte watumishi nipate ujuz wao.

Au kma wapo humu wanisaidie.
 
Mbona hapo kulikuwa hamna shida sema inaonekana ulikuwa na mahaba kwa mama-wewe ungesema ukweli tu,na kama msma ndio mwenye makosa ushahidi usingejitosheleza na kesu ingefutwa kiufupi ww ndio umesababisha baba yako afungwe ndio maana hadi leo unajisitukia kwa kutotenda haki
Mkuu ukwel nikwamba mzee alikuja kweli nikiwepo ila kwaamani sio kwa shar lkn katkat ya maongezi yao wakapishana kauli ugomvi ukaazia hapo..

Maneno yakawa mengi unavyojua tena mama zetu akaamua kutafts haki kwa sheria mkasa ukawa mkubwa.....
 
Mm ni mzaliwawa kwanza(First born) kwenye familia yetu yenye watoto watano.

Wazazi kabla ya kunileta duniani sikujua hali ya aman kipindi hicho ilikuwaje ila naamini walikuwa wawili wapendanao ndio maana wakakusudia kuanzisha familia pamoja.

Uzi huu sio kwaajil ya kuwalaumu wazaz wangu *hapana* Nawapenda sana mpaka mwisho wa uhai wangu pia nawaombea kher kila uchwao.

Wawili hawa walianza kupishana kauli na kupelekea kurudishana mara kwa mara nyumbani pindi mimi nikiwa darasa lasaba mwaka 2008.

Kipindi hicho bado akili za darasani zipo ila zile zingne bado zilikuwa likizo.

Mtoto wawatu nikafaulu uzur kwenda sekondar lakini wakat napokea matokeo hayo familia yangu haikuwa pamoja, na hapo mother yupo kwao tumebaki na baba ambae ametuacha kwa baba yake yan Babu yetu.

Nilipompelekea baba taarifa ya mimi kufaulu aliniambia sawa nimekusikia tutalifanyia kazi.... . sikuishia hapo nikapeleka taarifa pia kwa mother alichonijibu nikwamba nikamueleze baba maana yeye tayar hawezi kufanya maamuzi zaid ya kunishaur na kutoa msaada pale nitakapoanza sekondari.

Sasa kwenye sakata la mimi kwenda shule baba akaenda kwa mzazi mwenzake ( mama) ili kufanya majadiliano kidogo kuhusu mimi kwenda shule.

Kama unavyojua wanandoa waliogombana kumbukumbu zao zote zinakumbuka ugomvi tu wakapishana kauli tena wakarushiana maneno mazito.

Mama akaamua kumshitaki mume wake kwa kosa la kuja kwake na kumtishia maisha na kumtukana.

Ukweli siku hio nilikuepo wakat wanagombana mbele yangu.

Utata unakuja mahakaman ambapo mama amefungua kesi nzito ya kutishiwa kuuawa na shahidi ni mimi mtoto wao ambae nilkuwepo mwanzo mwisho.

Duh siku ikapangwa ya kuendesha kesi........kabla ya kwenda nikawa napewa mafunzo namna ya kwenda kusema mahakamani.

Upande wa baba wananipa yakwao.....upande wa mama wananipa yakwao. Dah kila upande unahitaji niutetee..

Mimi mambo yasheria sijui.... Kuendesha makesi ndio kilaza kama babashite....dahhhhh ilikuwa ngumu sana kwangu.

Shule ikafutika kichwani nikawaza nijiuwe wote wanikose siku ya ushahidi kakin mhhhhh kweli nife mm kijana mdogo kwa kujiua nikamkumbuka dem wangu nikasema sitajiuwaa.

Nilikuwa kama mfungwa huru yani kila aliekuwa anakuja nyumban hakuwa na mada tofauti na ile iliokuwa inausumbua moyo wangu.

Kichwa kilikuwa hakiwezi tatua hesabu ya 1+1 ukiniuliza hio najiangalia tu chozi linaenda ardhini.

Wazaz wangu wote nawapenda istoshe wote wananitegemea mm.

Itakuwaje ushahidi nitakaotoa ukasababisha mzazi mmoja akapelekwa jela?????? Si nitakuwa nimejenga ukuta na mzazi huyoo????

Maswali yalikuwa mengi kuliko majibu.......

Siku ilipofika nikasimamishwa kutoa ushahid pembeni yuko baba mbele hakimu pembeni mama wazee wawili(masesa) nawaona kwa mbele..

Kutizama dirishana wasikilizaji wapo wakutosha wametega masikio kunisikia naamua nan aende jela na arud nyumbani.

Eneo lile kulitulia ghafla kias kwamba ukihema kwa nguvu utaonekana umepiga yowe kwa ukimya huo.

Nilisita kuongea mdomo ulitikisika tu bila kutoa sauti yoyote wazee wawili wakaanza sema ukweli usitucheleweshe.

Na hapo nishakula kiapo cha biblia kuwa nitakachosema nichakweli kabsa mbele ya mahakama.

Mwisho wasiku nikasema nilikuepo siku hio wakati baba anakuja kwa mama lakn ugomvi sikushuhudia huenda baada ya mimi kuondoka walirushiana maneno huko nyuma.

Nikahitimisha mzigo ulionisumbua takribani wiki mbili kasoro.

Hakimu akanikazia jicho chozi likanidondoka ....

Siku hio ushahidi haukutosha ikapangwa siku nyingne shahidi ni mdgo mtu wa mwisho

Balaa kubwa kwangu dogo akafunguka ukweli wote mzee akapewa haki yake miaka miwili jela ila akalipa faini skarud nyumbani.

Maamuz yangu ya kipindi hicho yananifanya niishi bila ukaribu na wazazi wangu leo.

Kila mmoja ananitenga kiana flani japo najitahid kuwaweka karbu lakini kila mmoja anasukumia kwa mwenzake, wanadhani nitawasaliti tena kulingana na kile kilichotokea miaka tisa iliopita.

Nawaza kila siku ni njia ipi ningetumia ili kusolve bila kumkwaza yeyote??????????????????

Kwa staili kama hio ndugu zangu wana JF ningefanyeje??????.??...????????????????
Limepita lkn naitaji uzoefu wenu ili nijue je nilikosea kwa maamuzi niliochukua au la!!!

Karbuni
.you can never go back and make a new beginning but you can always begin and make a new ending..
 
.you can never go back and make a new beginning but you can always begin and make a new ending..
 
2008 umemaliza la saba na una demu, na uandishi wako huu!!!mbona kama mzee zaidi ya hapo???

Sasa nawe kwa akili yako ukamning'iniza faza ako???.pale ungeweka mpira kati,bila kufungamana na upande wowote.maana mpaka sasa sjui nani alikusomesha.

Hivi mkuu umesoma mada au umejibu tu? Si kasema alijitoa kuwa yeye hakusikia chochote??? Huku kukosa umakini ndio kunatuponza watanzania wengi.

Tukirudi kwa mtoa mada. Kwa maana hiyo ulidanganya mahakama? Maana kama ni kweli mshua alitishia maisha ungesimamia ukweli huo hata kama utakuponza. Na kitu cha pili ulifanya maamuzi sahihi pia kwa wakati huo na inakubidi usimamie maamuzi yako. Ndo ukubwa huo kila kitu tunachofanya duniani kina consequences na unapoamua kitu kiwe kizuri au kibaya uwe tayari kwa matokeo yake. Aidha mazuri au mabaya pia,ishi kwa amani kubali ukweli tengeneza ya kesho hayo ya miaka 9 iliyopita achana nayo huwezi kuyabadili
 
Ndio maana nimeshangaa,anasema alijitetea kwamba hakusikia chochote, baba yake alifungwa kwa ushahidi wa nani???

Vipi anauliza tungefanyaje kama ni sisi??
 
Back
Top Bottom