Internal nimesoma story vizuri,kwanza pole sana katika maisha kuna milima na mabonde,kuna nyakati za Giza na nyakati za mwanga na matumaini,hoja hapo niliyoielewa ni wewe kuwa na mahusiano hafifu au kutengwa na wazazi wako ndicho kitu ninachokuumiza na ambacho unataka Ku kisahihisha yaani kurudisha mahusiano vizuri na wazazi wako nadhani ni hilo,niweke sawa kama nitakuwa nimekosea.Kama ni hivyo kuna Dawa moja tu ambayo unaweza kuitumia haijawahi kushindwa kutibu kurejesha mahusiano yaliyoharibika.Dawa hiyo ni kuwa penda na kuwajali sana wazazi wako kuliko Jana na juzi,Upendo una nguvu kuliko kifo,wapende wazazi wako na usionyeshe kuwa wawo wanakuchukia au kukutenga,sijui una hali gani gani sasa lakini unaweza kutenga muda na pesa na kuaandaa matukio yatakayo onesha kuwa unawazajali,wasaalimu,watumie SMS za kuwapongeza kwa mambo mazuri waliyo Fanya,wanunulie zawadi,suti au vitenge,chukula,wakaribishe kwako,watembelee,huuu ni mfano tu vifunze kuwapenda kwa dhati na endelevu,kamwe usionyeshw hisia za kupambana nao,sahau yaliyotokea anza ukurasa mpya,hao ni wazazi wako wamebeba Baraka zako kutoka kwa Mungu,hamna namna wewe ni Mtoto na haukusababisha huo ugomvi,usifanye jambo la kumpendelea mama au baba kwa namna yoyote ile.kwa kusamalizi ni same wapende na wajali sana wazazi wako Upendo huo utaondoa hisia na mawazo yao mabaya kwako na mahusiano yatarudi tena mazuri kuliko mwanzo na kuhakikishia hili ndugu yangu,pole sana,Mungu atakusaidia.