Internal
JF-Expert Member
- Feb 23, 2017
- 3,579
- 3,913
Mm ni mzaliwawa kwanza(First born) kwenye familia yetu yenye watoto watano.
Wazazi kabla ya kunileta duniani sikujua hali ya aman kipindi hicho ilikuwaje ila naamini walikuwa wawili wapendanao ndio maana wakakusudia kuanzisha familia pamoja.
Uzi huu sio kwaajil ya kuwalaumu wazaz wangu *hapana* Nawapenda sana mpaka mwisho wa uhai wangu pia nawaombea kher kila uchwao.
Wawili hawa walianza kupishana kauli na kupelekea kurudishana mara kwa mara nyumbani pindi mimi nikiwa darasa lasaba mwaka 2008.
Kipindi hicho bado akili za darasani zipo ila zile zingne bado zilikuwa likizo.
Mtoto wawatu nikafaulu uzur kwenda sekondar lakini wakat napokea matokeo hayo familia yangu haikuwa pamoja, na hapo mother yupo kwao tumebaki na baba ambae ametuacha kwa baba yake yan Babu yetu.
Nilipompelekea baba taarifa ya mimi kufaulu aliniambia sawa nimekusikia tutalifanyia kazi.... . sikuishia hapo nikapeleka taarifa pia kwa mother alichonijibu nikwamba nikamueleze baba maana yeye tayar hawezi kufanya maamuzi zaid ya kunishaur na kutoa msaada pale nitakapoanza sekondari.
Sasa kwenye sakata la mimi kwenda shule baba akaenda kwa mzazi mwenzake ( mama) ili kufanya majadiliano kidogo kuhusu mimi kwenda shule.
Kama unavyojua wanandoa waliogombana kumbukumbu zao zote zinakumbuka ugomvi tu wakapishana kauli tena wakarushiana maneno mazito.
Mama akaamua kumshitaki mume wake kwa kosa la kuja kwake na kumtishia maisha na kumtukana.
Ukweli siku hio nilikuepo wakat wanagombana mbele yangu.
Utata unakuja mahakaman ambapo mama amefungua kesi nzito ya kutishiwa kuuawa na shahidi ni mimi mtoto wao ambae nilkuwepo mwanzo mwisho.
Duh siku ikapangwa ya kuendesha kesi........kabla ya kwenda nikawa napewa mafunzo namna ya kwenda kusema mahakamani.
Upande wa baba wananipa yakwao.....upande wa mama wananipa yakwao. Dah kila upande unahitaji niutetee..
Mimi mambo yasheria sijui.... Kuendesha makesi ndio kilaza kama babashite....dahhhhh ilikuwa ngumu sana kwangu.
Shule ikafutika kichwani nikawaza nijiuwe wote wanikose siku ya ushahidi kakin mhhhhh kweli nife mm kijana mdogo kwa kujiua nikamkumbuka dem wangu nikasema sitajiuwaa.
Nilikuwa kama mfungwa huru yani kila aliekuwa anakuja nyumban hakuwa na mada tofauti na ile iliokuwa inausumbua moyo wangu.
Kichwa kilikuwa hakiwezi tatua hesabu ya 1+1 ukiniuliza hio najiangalia tu chozi linaenda ardhini.
Wazaz wangu wote nawapenda istoshe wote wananitegemea mm.
Itakuwaje ushahidi nitakaotoa ukasababisha mzazi mmoja akapelekwa jela?????? Si nitakuwa nimejenga ukuta na mzazi huyoo????
Maswali yalikuwa mengi kuliko majibu.......
Siku ilipofika nikasimamishwa kutoa ushahid pembeni yuko baba mbele hakimu pembeni mama wazee wawili(masesa) nawaona kwa mbele..
Kutizama dirishana wasikilizaji wapo wakutosha wametega masikio kunisikia naamua nan aende jela na arud nyumbani.
Eneo lile kulitulia ghafla kias kwamba ukihema kwa nguvu utaonekana umepiga yowe kwa ukimya huo.
Nilisita kuongea mdomo ulitikisika tu bila kutoa sauti yoyote wazee wawili wakaanza sema ukweli usitucheleweshe.
Na hapo nishakula kiapo cha biblia kuwa nitakachosema nichakweli kabsa mbele ya mahakama.
Mwisho wasiku nikasema nilikuepo siku hio wakati baba anakuja kwa mama lakn ugomvi sikushuhudia huenda baada ya mimi kuondoka walirushiana maneno huko nyuma.
Nikahitimisha mzigo ulionisumbua takribani wiki mbili kasoro.
Hakimu akanikazia jicho chozi likanidondoka ....
Siku hio ushahidi haukutosha ikapangwa siku nyingne shahidi ni mdgo mtu wa mwisho
Balaa kubwa kwangu dogo akafunguka ukweli wote mzee akapewa haki yake miaka miwili jela ila akalipa faini skarud nyumbani.
Maamuz yangu ya kipindi hicho yananifanya niishi bila ukaribu na wazazi wangu leo.
Kila mmoja ananitenga kiana flani japo najitahid kuwaweka karbu lakini kila mmoja anasukumia kwa mwenzake, wanadhani nitawasaliti tena kulingana na kile kilichotokea miaka tisa iliopita.
Nawaza kila siku ni njia ipi ningetumia ili kusolve bila kumkwaza yeyote??????????????????
Kwa staili kama hio ndugu zangu wana JF ningefanyeje??????.??...????????????????
Limepita lkn naitaji uzoefu wenu ili nijue je nilikosea kwa maamuzi niliochukua au la!!!
Karbuni