Alphonce Mawazo mwanasiasa wa kuigwa CHADEMA

Alphonce Mawazo mwanasiasa wa kuigwa CHADEMA

mchambuzixx

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2011
Posts
1,292
Reaction score
946
jamani huyu kamanda muacheni aitwe Mawazo wakipatikana kama hawa sita CCM sijui atatokea upande upi.....je chama kinafadhili hizi ziara anazozifanya au ni wananchi wa maeneo ndio wanaomwita au vipi naomba kiongozi yeyote wa chama aje ajibu hapa tuelewe.

Ikumbukwe MAGU ni sehemu ambayo ina mizizi ya upinzani sema chama ambacho kilikita mizizi hapo magu NI UDP na walikua hawana strateg za ushindi kila uchaguzi wao hua wanashinda lakini wanaporwa kutokana na viongozi wao wakuu kua CCM B.

Ikumbukwe CHADEMA hawakua hata na mwenyekiti wa kitongoji Magu lakini ziara alizofanya bila kuchoka kamanda huyu zimeonesha kuwafungua watu macho leo hii tunashuhudia Magu CHADEMA ikianza kuchonga mzinga na ikumbukwe alikua kule Bukoba ambako nako pia matunda yameonekana,kila anapokwenda mabadiliko tunayaona naomba viongozi wengine huko msikae ofisini kupigwa viyoyozi nendeni vijijini mkapige kazi.

Toka ameachia udiwani huyu mtu sijawai ona amepumzika
Alphonce Mawazo alipojitoa CCM mwaka jana na kuingia CHADEMA wengi hawakumwelewa! Wengine walidhani kafuata madaraka tu,lakini Mawazo tayari alikuwa na madaraka makubwa tu CCM tena ya kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Sombetini Arusha.Alipojitoa CCM na udiwani ukaishia palepale.

Alphonce Mawazo kwa sasa jina lake linavuma kama moto wa Kiangazi huku Kanda ya ziwa.Ni mwanasiasa ambaye tangia ajitoe CCM na kujiunga Chadema ameamua kujikita vijijini huku Kanda ya ziwa kutoa elimu ya uraia na kueneza sera za Chadema.Anasimamia kwa vitendo operesheni ya chama sasa hivi ijulikanayo kama Chadema ni Msingi.

Kwa mwaka huu pekee Mwanasiasa huyu kijana ameweza kuzunguka kata na vijiji mbalimbali katika majimbo 30 ya Kanda ya ziwa.Katika majimbo hayo amefanikiwa kufanya mikutano ya hadhara 300.

Isitoshe kwa harakati zake hizi ameiwezesha Chadema kushinda vijiji na vitongoji mbalimbali katika chaguzi ndogo zilizofanyika mwaka huu Kanda ya ziwa.

Ninapoandika habari hii yuko katika jimbo la Ngara akiendeleza harakati za Chadema ni Msingi.

Hongera sana Alphonce Mawazo kwa kazi kubwa uliyofanya mwaka huu na Mungu azidi kukusimamia katika mwaka mpya wa 2014.

Makala hii Fupi ni kuonyesha mchango wako mkubwa ndani ya Chadema uathaminiwa na hauwezi kupita bure.
 
Huyu ni noma ulikuwa humjui? Huku Arusha anafahamika sana, ni kichwa balaa ni sawa na Magamba 1,000,000
 
Mungu amjalie afya njema kamanda Mawazo,huyu jamaa ni hatari kwa uhai wa ccm
 
Itafika wakati kila kitu kitakuwa sawa na viongozi wa ukombozi wataenziwa siku hiyo. Twende sasa ukombozi ni mgumu.
 
Huyu jamaa ni mpambanaji, ingekuwa vizuri watu wa aina hii mishahara yao ikawa minono ili kumfanya a focus kwenye kazi yake hii badala ya kufikiria watoto nyumbani
 
Katika hili chama changu chadema hawanifurahishi.. Huyu kamanda ziara zake zote anafanya bila kuwa na msaada kutoka makao makuu,yeye anachofanya ni kutoa taarifa leo ninafnya nini na nitakuwa wapi kama ni fedha anagenerate hukohuko field (aina ya siasa za huyu mkuu kwa kweli hata mimi nashindwa kuzielewa). Hata kama ni mtu ameanza siasa za one man army tayari ameonekana kuwa na uwezo mkubwa tafaadhali makao tunaomba mumwangalie huyu kamanda! Otherwise chadema ina hazina ya wapiganaji.
 
Safi sana..Tuntaka MAKAMANDA wa style hii...safi sana KAMANDA MAWAZO.....
 
ALFONCE Mawazo ni noooma!. kama kuna mtu anabisha aende Kwimba akaone alivyoivuruga Kata nzima kwa kuhamisha viongozi wa CCM kwenda CHADEMA. Jamaa namkubali sana....alimshukia Diwani mmoja wa CCM pale Hungumalwa Ngudu Kwimba hadi huyo diwani akakimbia mkutanoni.
 
Wekeni picha yake ili wengine waweze kuandika kumbukumbu kwa usahihi!
 
Hakika huyu jamaa ni noma,cdm tunatakiwa kumwandalia package maana magamba hawakawii kumshonza na kumwampamba kipindi wakiona katelekezwa
 
Wekeni picha yake ili wengine waweze kuandika kumbukumbu kwa usahihi!
nakumbuka huyu jamaa mara ya kwanza kumuona ilikuwa Arusha kwenye uwanja wa NMC tareh 5 January, jamaa alikuwa Diwani wa CCM na siku hiyo alipandishwa jukwaani na wafuasi wa CHADEMA.
 
siku niliposikia ndg.mawazo ameamia chadema nilifurai sana kwani nilimjua kamanda huyu tangu alipokua tlp.akahamia ccm.huyu bwana ni jembe kweli kweli.huyu bwana anauchungu kweli na nchii kuamua kuacha ugali wa udiwani tena kwa chama cha kupiga dili ccm ni ushujaa tena nikitendo cha kupongezwa sana.naiini picha nzuri sana na mfano wa kuigwa na viongozi wa cdm.sio kukaatu na kutangaza ntagombea urais.huku wengine wakivuja jasho huku na huko kupiga m4c nakuleta matunda makubwa kwa chama.wote wanaotaka urais kupitia cdm wapige kazi.na cctutawapima kwa kazi walizofanya na matunda walio yaletea chama.bg up.ndg mawazo piga kazi tupo nyuma yako.
 
BaCzsJpL61YdAAAAAElFTkSuQmCC
 
Safari ya ukombozi,ni ngumu sana na unapoamua kuianza,huna budi kupambana na kila hari,juhudi zako kamanda mawazo zinaonekana,jasho lako litaleta faraja,na ukombozi kwa Watanzania waliokandamizwa na udhalimu wa ccm,pambana kamanda usirudi nyuma wala usichoke,tuna siku chache sana zinazohesabika CDM kurudisha nchi kwa wananchi wake.
 
Hakika huyu jamaa ni noma,cdm tunatakiwa kumwandalia package maana magamba hawakawii kumshonza na kumwampamba kipindi wakiona katelekezwa

Hawamuwezi kwani kaachia udiwani aliokuwa nao akiwa umagambani na kuwa mtu wa kawaida kabisa, hivyo kumrubuni hawawezi hawa. Angekuwa na tamaa asikuwa tayari kuachia udiwani aliokuwa nao.
 
ana stahili yake akiwa jukwaani utatamani kumuangalia muda wote
 
Alphonce Mawazo alipojitoa CCM mwaka jana na kuingia CHADEMA wengi hawakumwelewa! Wengine walidhani kafuata madaraka tu,lakini Mawazo tayari alikuwa na madaraka makubwa tu CCM tena ya kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Sombetini Arusha.Alipojitoa CCM na udiwani ukaishia palepale.

Alphonce Mawazo kwa sasa jina lake linavuma kama moto wa Kiangazi huku Kanda ya ziwa.Ni mwanasiasa ambaye tangia ajitoe CCM na kujiunga Chadema ameamua kujikita vijijini huku Kanda ya ziwa kutoa elimu ya uraia na kueneza sera za Chadema.Anasimamia kwa vitendo operesheni ya chama sasa hivi ijulikanayo kama Chadema ni Msingi.

Kwa mwaka huu pekee Mwanasiasa huyu kijana ameweza kuzunguka kata na vijiji mbalimbali katika majimbo 30 ya Kanda ya ziwa.Katika majimbo hayo amefanikiwa kufanya mikutano ya hadhara 300.

Isitoshe kwa harakati zake hizi ameiwezesha Chadema kushinda vijiji na vitongoji mbalimbali katika chaguzi ndogo zilizofanyika mwaka huu Kanda ya ziwa.

Ninapoandika habari hii yuko katika jimbo la Ngara akiendeleza harakati za Chadema ni Msingi.

Hongera sana Alphonce Mawazo kwa kazi kubwa uliyofanya mwaka huu na Mungu azidi kukusimamia katika mwaka mpya wa 2014.

Makala hii Fupi ni kuonyesha mchango wako mkubwa ndani ya Chadema uathaminiwa na hauwezi kupita bure.
 
Katika watu ambao wako makini na ni wana siasa hasa tuliowapata kutoka CCM ni pamoja na Mawazo...
 
Back
Top Bottom