MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 20,897
- 63,784
Namaanisha nini?
Ni kweli Historia ya Wayahudi inakuwa traced kuanzia Adam hadi yakobo katika bibilia. Na hapo walipo sasa ni kweli palinunuliwa na Babu yao kwa mujibu wa kifungu cha bibilia., Na hata safari yao kutoka Misri walikuwa wanakwenda hapo walipo sasa. hata baada ya yesu kupigwa kwa yerusalem na wao kusambaratika na kukimbilia sehemu mbalimbali ulaya na afrika na baadae baadhi yao wakajikusanya na kurudi hao wachache tu maana wengi karibu3/4 wamesambaa dunia nzima.
Mimi naanini Hapo walipo ni sahihi na ni sehemu yao wanapaswa kuwa. Ila hao waliopo kuna watu wanawanyenyekea kama wana upendeleo flani wa kidini. Sioni kama ni sahihi. Ikija suala la Mungu kila mmoja anawajibika kufuata utaratibu wake sio Muisrael wala Msukuma. They are all equal before God.Kwa kusema hivyo nikimaanisha hao waliopo ni taifa tu kama Tanzania na wanapaswa kufuata utaratibu wa Mungu na kuacha mambo yao kama kuwauwa waparestine, etc
Walirudi vipi,kwa mbinu zipi,kwa nini walikataa walipopewa ardhi na UN kati ya Uganda na Kenya au ethiopia wakaamua kwenda eneo lenye jangwa,madimbwi yaliyojaa mbu. etc hapo sioni Dini ni mikakati yao ya kisiasa ila Ndio hao hao wala sio kweli ni watoto wa hesau.
Mkuu uko sawa kabisa.
Wale pale ni pao hata ufanyaje na Wayahudi hawa ni watu wa kawaida kama walivyo watu wa mataifa mengine.
Hakuna haja ya (special treatment) kama ambavyo American Evangelicals wanataka kuiaminisha dunia.
Hapo nyumba nakumbuka kabla ya U.N kutaka kuwapa maeneo ni serikali ya Uingereza ilitaka iwape Uganda kwasababu lilikuwa ni koloni lake wao wakakataa.
Tena ukisoma sana utakuja kwamba walipewa hadi kisiwa cha MADAGASCAR wakakataa.
Muhimu ni kukumbuka kwamba uwepo wa Taifa la ISRAEL ni Strategy kubwa ambayo mtu ukiangali vizuri utaelewa kabisa. Kwanza it is an ATHEISTIC and IMPERIALISTIC nation serving the interests of the global elites in the middle east. Kipindi Zionism inazaliwa Orthodox Jews walipinga sana na hadi sasa wanapinga.
Kuwafukuza wayahudi kama baadhi ya wachangiaji wanavyosema si sahihi hata kidogo.
Ila TWO STATE SOLUTION ndiyo Mwarobaini. Ukiwarudisha Ulaya hakuna nchi itakayowapokea.
Na ikumbukwe leo ukitaka kuwafukuza Wayahudi pale Mashariki ya kati basi utakuja kukuta kwamba dunia nzima kutakuwa na Migration. Uelewa butu na chuki zisituzuie kuona uhalisia.
Ukifukuza Wayahudi Mashariki ya kati kwa minajili ya kusema siyo pao basi ni sawa sawa unasema,
- Washirazi wafukuzwe Zanzibari ile ni sehemu ya Weusi tu.
- Wazungu wafukuzwe South Africa ile ni sehemu ya Weusi tu.
Israel inaua Wapalestina kwasababu ni Marekani na Mataifa ya magharibi yananufaika. Pindi hayo Mataifa yanacha kuisaidia Isreal basi lazima amani irudi pale Mashariki ya kati.
Lakini hizi blah blah za kusema eti wataifuta kwenye ramani ya dunia ni maneno ambayo huwa siyaafiki hata kidogo.
Hakuna mwanadamu mwenye dhamana ya kutoa uhai wa wanadamu wengine kwasababu zake zisizo za msingi.