eden kimario
JF-Expert Member
- Jun 13, 2015
- 10,233
- 16,202
Izrael ilianzishwa na waizraeli waliotoka nchini misri chini ya uongozi wa musa na yoshua ambae alivamia kanaani mnamo mwaka wa 1200 kk.
Muungano wa vikundi na makabila mbalimbali yasemekana ndio chanzo cha kuundwa kwa taifa moja teule chini ya sauli na baadae daudi na Solomoni mwanae Daudi.
Baada ya kifo cha solomoni mfalme mtafaruku uliibuka kiasi kwamba izrael ilipasuka vipande viwili yaani ufalme wa kazkazini ulioendelea kujiita izraeli. Na ufalme wa Yuda ambao mji mkuu wake ukikua Yerusalemu.
Kutokana na kujitenga huku falme hizi zilikosa nguvu ya kushinda vita. Na hivyo kujikuta zikiwa chini ya falme mbalimbali za babiloni uajemi na ugiriki ya kale na hii ilikua ni kuanzia mwaka 587 kk.
Lakini kuliibuka kikundi kilichojiita wamakabayo kilichoanzisha harakati za kurudisha uhuru na waliweza kuwafukuza wagiriki waliokua wakiwatawala kwa kipindi hicho na kuanzisha ufalme na kuanzisha ufalme wa kiyahudi kati ya mwaka 140 kk.
Pamoja na hilo ufalme huo uliwekwa chini ya dola la kirumi mwaka 63kk. Na hatimae kua jimbo la kiroma mwaka 70 bk.
Maangamizi ya yerusalemu mwaka 70bk yanahesabiwa kama mwisho wa Israeli ya kale
Nikukumbushe tu wakati wa ujio wa yesu izraeli na palestina zilikua chini ya dola la kirumi ambao walitawala maeneo yote ya bahari ya mediterenian.
Nimalizie tu kwa kusema izraeli ya sasa sio ile ya taifa teule la mungu. Bali ni uzao wa ashkenazi ambae ni kizazi cha uzao wa Esau. Kama unaelewa zaidi kuhusu Israel ya kale karibu uongezee ili wengine na mimi tuelewe zaidi.