Ally Kiba, Diamond kuibeba Serengeti Boys

MZK

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
223
303
Wanamuziki Ally Kiba na Diamond Platnumz ni miongoni wa wajumbe wa kamati ya watu 10 wa kusaidia maandalizi ya timu ya taifa ya vijana ya Tanzania 'Serengeti Boys'<Akitangaza kamati hiyo inayoundwa na wanahabari, viongozi wa kampuni na wasanii Waziri wa Habari, Utamaduni Sana'a na Michezo Nape Nnauye amesema jukumu kubwa la kamati hiyo ni kuhakikisha wananchi wanashirikishwa kwenye maandalizi ya timu hiyo."Tumeshamiria kuona timu hii inafanya maandalizi makubwa na nimeongea na Malinzi asubuhi hii yuko Morocco akiweka sawa masuala ya kambi ya vijana,"amesema.Kamati hiyo itakuwa chini ya uenyekiti wa mwanahabari mkongwe Charles Hillary na katibu ni katibu mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine.Wajumbe wa kamati hiyo ni wanamuziki Ally Kiba na Diamond Platnumz wengine ni Beatrice Singano, Ruge Mutahaba, Maulid Kitenge, Erick Shigongo, Hassan Abbas na mwanamitindo Hoyce Temu.Serengeti Boys imefuzu kucheza fainali za vijana Afrika nchini Gabon Mei 24- Juni 5, baada ya kushinda rufani yake dhidi ya Congo-Brazzaville iliyomchezesha mchezaji Langa Lesse Bercy ambaye umri wake ulizidi miaka 17
 
Mchungu wa kupiga maela maana kwa kamati hiyo lazima michango imiminike sasa tff sasa nawaona wanavyo subiria michango hiyoo
 
Bonge la mseto wakitulia hao jamaa wana ushawishi kwa watu wengi wanaweza kusaidia kwa namna moja au nyingine.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom