mrisho shabani
Member
- Feb 11, 2008
- 14
- 0
Asante sana kwa uchangiaji wenu,unaoruhusu hoja pinzani nazo kujikita mahala,mie nauita ni "open minded thinking".
Kwenye ile taarifa ya kamati kuna mambo mengi sana na ndio maana waziri mkuu hata kaunda kamati nyingine kupitia yale mapendekezo na kuona ni jinsi gani yanatekelezeka bila kuathiri haki za watu au kuwaonea wengine. Kikubwa kilichobainika na kamati ya mwakyembe ni ukiukwaji wa wazi wa taratibu za tendering uliofanywa na wizara,maafisa wake na kitu kinachoonekana kama shinikizo la waziri mkuu. Ukiukwaji wa taratibu huo kwa wenyewe sio rushwa tena kisheria unafall katika administrative law,bali umebeba pia mambo mengine kibao yanayoibua masuala mengine ya kisheria. Point kubwa hapa ni ukiukwaji wa sheria ya tendering na kutofanya due diligence ambayo inategemewa kwa reasonable man wa calibre ya AG,na maafisa wa wizara.
Ukiukwaji kama huu kwa kawaida adhabu zake zipo administratively sio judiciary.Adhabu zao ni kama kushushwa vyeo,kuhamishwa vitengo kwani vile walivyopo sio competent n.k.Sasa HOSE yeye anakuja wapi? Kila mtu katika ile ripoti anasehemu yake aliyochangia kama ni nengligence tunasema contributory negligence.
Kama walivyo wengine HOSEA sehemu inayomgusa ni hii:
Ukisoma kifungu cha 6 cha sheria hiyo ya zamani kinasema kwamba
mtu yeyote ambaye kwa kujua atampa wakala, au wakala yeyote kwa kujua atatumia kwa lengo la kumdanganya mkuu wake, risiti,akaunti au hati au nyaraka yoyote inayohusiana na mambo au shughuli yoyote ya mkuu wake wa kazi na ambayo ina taarifa feki,za kughushi au zilizopotoshwa na kwa jinsi yoyote ile zina lengo la kumdanganya mkuu,atakuwa ametenda kosa.mwisho wa kunukuu.
Sawa Hosea hakuona rushwa,je hakuona pia kipengele hiki cha sheria? je katika mkatba wa richmond hakukuwa na nyaraka feki zenye lengo la kumpotosha mkuu,je kusema kwamba richmond ina ubia na kampuni ile waliyoitaja na kuthbitisha hilo kwa business kadi hakukuwa na lengo la kumpotosha mkuu?je,ukweli kwamba richmond haikuwa mtu kisheria yaani sio kapuni halali kwa kuwa inakosa usajili tanzania na huko USA haipo na kwamba hata kama ilisajiliwa hapa nchini usajili wake haukuwa halali kwa kuwa hatuna one man company kwa mujibu wa kifungu cha tatu,moja cha sheria ya makampuni.je,waliohusika hawakuwa na lengo la kumpotosha mkuu?
Hapa tu,akiclear hapa anapeta,mi ningekuwa wakili wake ningejikita kutafuta defense mahali hapa zaidi,kwani sehemu nyingine zote za sheria namba 16 yupo clean.Hatuna sheria ya harufu wala moshi wa rushwa.Neno harufu au moshi wa rushwa linatokana na sheria ya ushahidi ya ya mwaka 1967 nadhani THE LAW OF EVIDENCE ACT,kifungu cha 3 hadi 15 kinachozungumzia circumstancial evidence, Circumstancial evidence ndio inayounda mazingira au harufu ya tukio la rushwa. Ndio maana nikasema hata katika kesi ya balozi mahalu inayoendelea hakukuwa na rushwa ya moja kwa moja kesi imeenda mahakamani on circumstantial evidence.Na kesi za namna hii huwa ngumu sana kuliko zile za kumshika mtu papo kwa hapo.
Hayo yote ya kamati kuwataja watuhumiwa au la sioni kama ni msingi sana kwa mhe.Hosea ambaye namheshimu sana kama mwalimu wangu somewhere.Ila ni wazi wenzie hata kama wana hila mbaya naye wanataka kumkamatia hapa.Ningeomba mtu mwenye ripoti ya HOSEA atumwagie hapa ile tuweze kujadili vizuri zaidi kwa kuilinganisha na findings za mwakyembe.
Kwa mantiki hii mimi na wadau wengine ndio maana tunashawishika kukubali kuwa Mhe.HOSEA anawajibika katika sakata hili la Richmond unless aje na maelezo ya kuridhisha zaidi lakini sio kujibu wadau kwa jazba.

MAZINGIRA YANAASHIRIA RUSHWA NA HUYU HOSEA NDIO ANGA ZAKE HIZO maana amefanya Ph.D Law: Mapambano dhidi ya Rushwa nchini Tanzania: Nguvu ya Ushahidi wa MazingiraKutumia madaraka yako kupata Tender ya serikali sio kosa wala Rushwa hata kidogo na sheria za Azimio zinawa protect zaidi..
Nashindwa kumuelewa HOSEA
Jamani wanajf humu ndani inaonesha kuna wanasheria wengi sana tena waliobobea ikibidi zaidi ya mwakyembe na Hosea,ndio maana hii mijadala labda haiishi,lakini pamoja na hayo siasa na misukumo binafsi nayo imetuelemea mno kiasi saa nyingine tunashindwa kutoa hoja na badala yake tunang'ang'ania misimamo yetu. Aliyemwanazuoni atakubaliana nami kuwa lazima akubali kupingwa na katika kufanya hivyo hoja yoyote anayoitoa anaitoa akiwa na open mind huku akielewa kuwa wapo watakaompinga wapo watakaomkubali na pia wapo watakaotaka kuelimishwa zaidi.Lakini katu hatowachukia wanaompinga kwani nao wanahoja zao shindani.
Baada ya kusema hayo,sasa narudi kwa HOSEA.Mhe. HOSEA wakati anachunguza sakata la Richmond alikuwa akitumia sheria namba 16 ya mwaka 1971 kadiri ilivyofanyiwa marekebisho kwa vipindi toauti.Vilevile wakati HOSEA nachunguza kuhusu sakata la balozi Mahalu vilevile alikuwa akitumia sheria hii hii. Makosa yote haya mawili yalihusisha viongozi wa serikali kwa upande mmoja na watu binafsi au makampuni yaliyoko nje ya nchi. Na katika makosa yote hayo mawili yaliyoiingoza hasara nchi yetu hakuna aliyewahi kushikwa red handed akiomba,au kupokea rushwa. Yote yanahusisha ushahidi wa kimazingira tu. Makosa yote mawili pia hayahusishi rushwa tu bali pia uhujumu uchumi.
Hivi karibuni Hosea amesikika kwenye vyombo vya habari akisema,yeye kazi yake ni rushwa na kwamba alifanya kazi kwa mujibu wa sheria ya rushwa ya mwaka 1971 ilivyokuwa,hivyo kazi yake si miktaba wala uhujumu uchumi. Jibu hili linafanana sana na alilolitoa mwanyika wakati anahojiwa na kamati ya mwakyembe. Swali hapa je,uhujumu uchumi na mikataba ni kazi ya nani? si makusudi yangu kujibu swali hili leo hapa,bali kuangalia uhalali wa kauli za HOSEA kuhusu wajibu wake kwa masuala yote hayo mawili hapo juu.
TAKURU ya zamani iliundwa kwa mujibu wa kifungu cha tatu cha sheria ya rushwa mwaka 1971 ikiwa na majukumbu yafuatayo,hapa nitanukuu
1.TO take necessary measures for the prevention of corruption in the public,parastatals and private sector.
2.To investigate and prosecute offences under the Act and other offences involving corrupt transactions.
3.Advise the governement and other parastatals organization on the ways and means to prevent corruption.
Sheria pia inaendelea kusema kuwa wakati wakitekeleza majukumu yao,watakuwa na mamlaka ya kipolisi sawa na askari mwenye cheo cha ASP.Hivyo kwa ufupi hizo ndizo kazi zao. Ukiangalia kwa haraka haraka tu utakuta kwa kauli za hosea,haguswi na richmondi kwani labda alishafanya kila jinsi kuzuia rushwa,pili alishachunguza akakuta hakuna rushwa ya moja kwa moja na tatu aliishauri serikali kwamba iendelee tu na richmond kwani hakua rushwa na haipati hasara yoyote.
Hivi kusema serikali inapata hasara au haipati ilikuwa ni kazi yake? hiyo kazi inafall wapi kati ya hizo kazi tatu kuu hapo juu? naam labda alisema kwakuwa hizo zilikuwa hadidu za rejea za uchunguzi wake. Lakini mimi naenda mbali zaidi.
Ukisoma kifungu cha 6 cha sheria hiyo ya zamani kinasema kwamba
mtu yeyote ambaye kwa kujua atampa wakala, au wakala yeyote kwa kujua atatumia kwa lengo la kumdanganya mkuu wake, risiti,akaunti au hati au nyaraka yoyote inayohusiana na mambo au shughuli yoyote ya mkuu wake wa kazi na ambayo ina taarifa feki,za kughushi au zilizopotoshwa na kwa jinsi yoyote ile zina lengo la kumdanganya mkuu,atakuwa ametenda kosa.mwisho wa kunukuu.
Sawa Hosea hakuona rushwa,je hakuona pia kipengele hiki cha sheria? je katika mkatba wa richmond hakukuwa na nyaraka feki zenye lengo la kumpotosha mkuu,je kusema kwamba richmond ina ubia na kampuni ile waliyoitaja na kuthbitisha hilo kwa business kadi hakukuwa na lengo la kumpotosha mkuu?je,ukweli kwamba richmond haikuwa mtu kisheria yaani sio kapuni halali kwa kuwa inakosa usajili tanzania na huko USA haipo na kwamba hata kama ilisajiliwa hapa nchini usajili wake haukuwa halali kwa kuwa hatuna one man company kwa mujibu wa kifungu cha tatu,moja cha sheria ya makampuni.je,waliohusika hawakuwa na lengo la kumpotosha mkuu?
Watu wote waliokuwa wakideal na richmond walikuwa wanajua nini kinachoendelea toka mwanzo hadi mwisho,na ukweli wote hapo juu walikuwa wanaujua je,hakuwa na nia ya dhati ya kumpotosha mkuu? ili aingie mkataba na mtu asiyekuwepo(yaani fictitious person?) Hosea hili hakuliona kabisa? Kama hakuliona anatofautiana vipi na sisi walei(laymen) wa taaluma ya kuchunguza rushwa? basi ameprove incomptence kwenye taasisi yake iwapo atashindwa kuthibitisha hili.Basi uchunguzi wake ulijikita kwenye nini? yaani ni vitu gani alivyoviangalia hadi akaandika ripoti?
Je,kama vigezo hivyo hapo juu havikwepo kwa maana kwamba kampuni ilitoa nyaraka feki juu ya uwepo wake kisheria na maafisa wetu wakavipokea na kumwaminisha mkuu ili anendelee kuingia mkataba je,hakukuwa na harufu ya rushwa iliyowapofusha maafisa wetu wasiweze kuchunguza zaidi juu ya uwezo wa richmond kisheria na kama je,imetimiza masharti yote ya sheria za tanzania?Mbona ukisoma mkataba wa richmodn maafisa wetu wanasaini kabisa kauli zao kwamba wameridhika richmondi ni kampuni halali kisheria na haijavunja sheria yoyote ya tanzania,wakati kwa hakika imevunja sheria ya makampuni na sheria ya mikataba ya mwaka 1961.
Sawa Hosea atasema yote haya si kazi yake na hayakuwamo Richmondi. Ok,si kazi yake ndiyo lakini jaji mmoja kwenye kesi ya Donoghue v,stevenson[1932]QB aliwahi kusema "....iwapo tutakwenda hatua moja kwanini isiwe hamsini?" HOSEA alifikiaje uamuzi wa kumshitaki balozi mahalu? alijuaje kuwa pale kuna mkono wa rushwa wakti mazingira yake yalikuwa swa na richmond? Ni kwanini HOSEA alitumia kifungu cha sita katika suala la mahalu kumtia mahalu hatiani wakti kwenye richmond hakukitumia?ilikuwaje katika mashtaka ya mahalu Hosea huyohuyo akamchaji pia balozi mahalu na uhujumu uchumi pamoja na wizi kama mtumishi wa umma kwa mujibu wa sheria ya kanuni ya adhabu(pena code cap16) na pia sheria ya rushwa 1971,wakati kwa mujibu wa sheria ya mwaka 1971 hakuwa na mamlaka ya kuestablish makosa hayo?
Mamlaka ya kuchaji mahalu kwa kutumia penal code na Economic and organised crimes control Act aliyapata wapi.Hivyo basi kama aliweza kwenye hili la mahalu tultegemea aweze pia kwenye richmond kwani kanuni za haki zinasema "justice must not only be done but must be seen to be done" na katiba yetu intambua equality before the law. Ni kutokana na mashaka haya niliyoataja hapo juu ndio maana mhe. Hosea anatuhumiwa kuhusika kwa namna moja au nyingine kwenye sakata la richmond kwa kuufumbia macho uovu wa wazi.
Na kama mwanazuoni? utafiti wowote unasehemu ya hitimisho na mapendekezo,ambayo tulitegemea hosea aseme,pamoja na kuwa kazi yangu si kuangaliwa mikataba na masuala ya uhujumu uchumi,lakini katika utafiti wangu au uchunguzi nimegundua mapungufu yafutayo kwenye mkataba wenyewe na kwenye uhalali wa kampuni ya richmond kisheria ambao napendekeza ziundwe tume maalumu zenye mamlka ya kuchunguza uhalali wa mkataba huu nk.ili kujiridhisha zaidi. Hapa angekuwa safe,lakini yeye alikana kabisa na kusema mchakato wote ulizingatia sheria na ulienda kwa kufuata vipengele vyote wala hakuna harufu ya rushwa na wala hatupati hasara.mmh HOSEA ulienda mbali mno uliposema vipengele vyote vya sheria vilifuatwa je,na kanuni za manunuzi zinazosema tenda itangazwe siku 45 na wao wakatangaza siku kumi je,huko kulikuwa ni kufuata sheria? au ripoti ya PPRA hakuiona?
Kwa mantiki hii mimi na wadau wengine ndio maana tunashawishika kukubali kuwa Mhe.HOSE anawajibika katika sakata hili la Richmond unless aje na maelezo ya kuridhisha zaidi lakini sio kujibu wadau kwa jazba.
Wadau naomba niwakumbushe kitu,katika kufanya huu mjadala pia hebu tusisite kujiuliza kwamba mbali ya hseria ya kutangaza tenda siku 45 kukiukwa na utaratibu mzima wa tendering,je,ni kwa nini labda kampuni ambayo kila iliposhindanishwa na kampuni nyingine ilionekana ya mwisho ndiyo ikapewa tenda ya kuzalisha umeme?mmh yaani mnapiga pepa halafu wa mwisho au wale watu wa tatu mwishoni ndio wanaingizwa kwenye mchakato kwa kuchaguliwa kuingia kidato cha tano wale wenye division one au two wanaachwa kwamba hawafai?Ipi ni tafsiri ya jambo hili? jamani mambo mengine magumu,lakini wadau wa jf nawaaminia mnaweza kudadavua.Kwa uelewa wa kinadharia kamati zote mbili ya HOSEA NA MWAKYEMBE hazikuweza kugundua waziwazi uwepo wa rushwa na kwa sheria ya mwaka 1971 hakuna rushwa.Swali gumu pale ni je,ipi tafsiri ya ukiukwaji ule wa sheria?ni kwa nini mtu anayefeli ndio apewe tenda,ni kwa nini siku 10 badala ya 45,ni kwa nini baadhi ya watu walikuwa concerned sana hata kama hawahusiki,tafsiri yake ni nini?mimi na wewe hatujui hapa hasa ndipo panahitajika utafiti zaidi.
Kwa uanazuoni wangu naona makosa mengi hapa ni ya kutowajibika zaidi kuliko rushwa.Watu hawakuwa responsible kwenye vitengo vyao,walizembea mno,walipuuzia majukumu yao hata kama hawakupokea senti tano ya mtu. Mtu unapokosa kutimiza wajibu wako kisheria mf.polisi aliyepewa kazi ya kulinda benki,yeye akasimama tu pale mbele ya benki,wezi wakapitia upande wa nyuma wakavunja benki na kuiba bila yeye kujua,anawajibika kisheria japo usiku mzima alikuwa macho hakulala wala kusinzia hata tone. .
Kwa kuwa wajibu wake kisheria unamtaka asiishie tu kuwa macho na kushika silaha bali atumie uwezo wake wote na ujuzi aliosomea kuhakikisha anashtuka hata kudondoka kwa jani la mti tu,asipuuze kwani hicho chaweza kuwa kishindo cha mruka ukuta.Hosea hakukuta rushwa hata ningekuwa mimi nisingeona rushwa pale labda,kinachomning'iniza huyu ni conclusion zake.Au kama kweli wabunge wanavyosema ripoti aliyoitoa kwa umma haikuwa hata na tarehe na kwamba haikuwa yenyewe,original aliificha hilo suala ni gumu sana,ndio maana naomba sana wadau hebu tupatieni hiyo ripoti aliyoitoa hosea hapa tuidadavue ili tuone kama twaweza kumsulubu kiasi gani au kumclear.Na tutafanya hivyo tu kwa kuangalia hadidu zake za rejea na wajibu wake kisheria.
TAKUKURU haiko usingizini- Hosea
2008-04-29 10:10:56
Na Onesmo Kapinga
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuizua Rushwa Nchini, (TAKUKURU), Dk. Edward Hosea, amesema uchunguzi wa kesi kubwa 10 za rushwa utatangazwa mwaka huu.
Alisema kuwa kati ya kesi tano matokeo yake yanatarajiwa kutangazwa baada ya mwaka wa fedha wa serikali ambao unamalizika Juni 30, na zingine ifikapo Desemba, mwaka huu.
SOURCE: Nipashe