Abunwasi
JF-Expert Member
- Jun 25, 2009
- 5,486
- 3,468
Inna lilahi wainaila rajiunView attachment 1204473chanzo:mwananchi facebook
Inna lilahi wainaila rajiunView attachment 1204473chanzo:mwananchi facebook
Kama ndiko huko sidhani hata kama mwaka mmoja kafikisha. May his soul RIP.nadhani alikuwa mwenyekiti wa bodi ttcl kama sijakosea
Hivi wewe uko dunia gani????Huyu ndie aliyetudanganya na kutuaaminisha kuwa Airtel ni mali ya Serikali kumbe muongo mkubwa. Walikuja wahindi wenye kampuni yao, sijui porojo zake ziliishia wapi?
Aliwahi kuwa mkuu wa mkoa wa tanga miaka ya 2010
Hayupo hapa.!
Kweli mawazo ya kuwa AIRTEL ni mali ya Serikali na toka 2017 ameshindwa kuprove hivyo yanaweza kuwa yalimletea sonona (depression). RIP NunduHuyu ndie aliyetudanganya na kutuaaminisha kuwa Airtel ni mali ya Serikali kumbe muongo mkubwa. Walikuja wahindi wenye kampuni yao, sijui porojo zake ziliishia wapi?
Apumzike kwa amani Mzee wetu Omary ibn Nundu. Namkumbuka wakati akiwa Waziri wa Uchukuzi na jinsi alivyopambana na Naibu Waziri wake Eng. Mfutakamba baada ya kuwa Naibu Waziri anamzunguka mkuu wake. Mzee alitoka hadharani na kukemea; alithubutuWaziri wa zamani nchini Tanzania, Omary Nundu amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Hospitali hiyo imethibitisha.
> Mnamo tarehe 27 February 2017 Rais Magufuli alimteua Omary Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la TTCL.
> Nundu aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tanga kuanzia mwaka 2010 hadi 2015
Historia Ya Marehemu, Omary Nundu
Omari Rashid Nundu, alizaliwa Tanga, Tanzania mwaka 1948 na huko ndiko alikopata elimu yake ya shule kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Glasgow, Scotland mwaka 1971 kusomea uhandisi na sayansi ya vyombo vya anga (Aeronautical Engineering); na baadaye kuendelea na shahada za juu na utafiti vyuo vikuu vya Cranfield, England na Concordia, Canada.
Omari amebahatika kufanya kazi kwenye taasisi mbalimbali duniani katika kuitendea haki taaluma hiyo aliyoisomea na anayoipenda. Kwa nyakati mbalimbali alikuwa mhandisi na mkurugenzi kwenye mashirika ya ndege, alikuwa mshauri na mhadhiri kwenye vyuo vya kimataifa, na pia alikuwa mkuu wa vitengo vya usafiri wa anga katika jumuia za kimataifa.
Kabla ya kurejea Tanzania na kuwa mbunge wa Tanga na pia Waziri wa Uchukuzi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa Rais wa jopo la kimataifa la magwiji wa taaluma ya Usafiri wa Anga Duniani (Air Navigation Commission) kwa miaka miwili mfululizo
Ingawa ni mhandisi na mwana sayansi aliyebobea, Omari anapenda kuongea lugha mbalimbali lakini ana mapenzi ya dhati kwa lugha ya Kiswahili ambayo ndiyo iliyomkuza. Hivyo basi kuwa yeye ni malenga wa mashairi halishangazi. Utenzi uliomo mwenye kitabu hiki unajaribu kusimulia maisha na mwenendo wa Dunia kwa kadri alivyoyashuhudia mhandisi huyu hadi mwaka 2015.
Comment ya kikuda sana mkuu hujawahi kufiwa na mtu wako wa karibu?Apumzike mahali alipochagua wakati akiwa hai
Alikuwa waziri wa nini miaka hiyo? RIP
Inna illay wa rajuni