TANZIA Aliyewahi kuwa Waziri na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Omary Nundu amefariki dunia

Pumzika kwa Amani. Ameisaidia sana Shirika la Posta hasa alipokuwa Mwenyekkiti.
 
RIP comrade
Waziri wa zamani nchini Tanzania, Omary Nundu amefariki dunia na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), imethibitisha.

> Mnamo tarehe 27 February 2017 Rais Magufuli alimteua Omary Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la TTCL.

> Nundu aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tanga kuanzia mwaka 2010 hadi 2015
******

Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, Dk Omary Nundu (71) amefariki dunia.

Taarifa iliyotolewa leo mchana Jumatano Septemba 11, 2019 na Kitengo cha Mawasiliano cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dar es Salaam kimesema, “Waziri wa zamani Omary Nundu alifikishwa leo MNH, akitokea nyumbani kwa gari binafsi la wagonjwa akiwa tayari ameshafariki.”

“Hivyo waliomleta waliamua wakahifadhi mwili wake katika hospitali ya rufaa ya Jeshi Lugalo,” imeeleza taarifa hiyo
Dk Nundu enzi za uhai wake aliwahi kuwa mbunge wa Tanga na Waziri wa Uchukuzi katika Serikali ya awamu ya nne ya Tanzania.

Juni 12, 2019, Rais wa Tanzania, John Magufuli alimteua Dk Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania ikiwa ni utekelezaji wa makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya Bharti Airtel International.

Katika makubaliano hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania pamoja na ofisa mkuu wa ufundi wanapaswa kuteuliwa na Serikali.

Historia Ya Marehemu, Omary Nundu

Omari Rashid Nundu, alizaliwa Tanga, Tanzania mwaka 1948 na huko ndiko alikopata elimu yake ya shule kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Glasgow, Scotland mwaka 1971 kusomea uhandisi na sayansi ya vyombo vya anga (Aeronautical Engineering); na baadaye kuendelea na shahada za juu na utafiti vyuo vikuu vya Cranfield, England na Concordia, Canada.

Omari amebahatika kufanya kazi kwenye taasisi mbalimbali duniani katika kuitendea haki taaluma hiyo aliyoisomea na anayoipenda. Kwa nyakati mbalimbali alikuwa mhandisi na mkurugenzi kwenye mashirika ya ndege, alikuwa mshauri na mhadhiri kwenye vyuo vya kimataifa, na pia alikuwa mkuu wa vitengo vya usafiri wa anga katika jumuia za kimataifa.

Kabla ya kurejea Tanzania na kuwa mbunge wa Tanga na pia Waziri wa Uchukuzi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa Rais wa jopo la kimataifa la magwiji wa taaluma ya Usafiri wa Anga Duniani (Air Navigation Commission) kwa miaka miwili mfululizo

Ingawa ni mhandisi na mwana sayansi aliyebobea, Omari anapenda kuongea lugha mbalimbali lakini ana mapenzi ya dhati kwa lugha ya Kiswahili ambayo ndiyo iliyomkuza. Hivyo basi kuwa yeye ni malenga wa mashairi halishangazi. Utenzi uliomo mwenye kitabu hiki unajaribu kusimulia maisha na mwenendo wa Dunia kwa kadri alivyoyashuhudia mhandisi huyu hadi mwaka 2015.
 
Rest in peace Mh Nundu.

Daby unakumbuka kile kipindi cha kampeni pale shulen..... Yule mgombea wa udiwan kwenye ile kata pamoja na marehem walituletea mihogo shule?? Na ahadi kedekede....
 
Pumzika Mzee Omary Mungu akurehemu
 
RIP

Ingawa ni mhandisi na mwana sayansi aliyebobea,
Ungetoa taarifa za kifo tu hapa ingetosha sana kwa wakati huu.

Haya mengine yoote ya ubobezi na usomi wake tukiyachambua hapa tutakuwa tunaharibu na kumkosea heshima marehemu.
Kwani wasifu kama ulivyowekwa hapa hauna kichwa wala miguu.

Inawezekana, na inaelekea marehemu alikuwa mtendaji mzuri kwenye maeneo aliyoyasimamia. Lakini ukitaka kweli tuchambue "Ubobezi" kwenye sayansi na uhandisi...utataka kumkosea heshima marehemu.

Tuachane na haya mambo ya "ubobezi" pembeni.
 
Ndugu siasa zisitufikishe hapo ulipofika. Utu ni kitu muhimu sana,mengine ni ya kupita tu.
Umeyawaza vizuri haya uliyoandika hapa?
"utu ni kitu mhimu sana---" Ndugai ana "utu" ?

Unaposema "siasa zisitufikishe hapa", kweli una maana ya kusema anayofanya Ndugai ni 'siasa'?

Pengine maana ya maneno 'siasa' na 'utu' inakupa shida kuzitambua.
 
Nilijua hatakuwa na furaha na all in all lazima msongo ungemtesa maana alirudishwa kupewa ubunge na uwaziri ili atumie taaluma yake kuleta maendeleo nchini, tatizo sisi tunapenda siasa kuliko maendeleo ya aina yoyote iwe kiuchumi kijamii kimichezo mpaka kielimu. Kiteknolojia ndo usiseme kabisa ukivumbua kitu ni hatari kwako kuliko kawaida ya kwamba utakuwa umetoka kimaisha.
 
Back
Top Bottom