Aliyetoroka karantini akamatwa Iringa

Aliyetoroka karantini akamatwa Iringa

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amesema alipigiwa simu na mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Dniale Chongolo na akamjulisha kuhusu mtu aliyetoroka karantini.

Mtu huyo baada ya kutoroka Dar alionekana yuko Iringa, uongozi wa wilaya walishirikiana na jeshi la polishi kujua anapokaa mtu huyo na wamempeleka kantini.

Mtu huyo inasemekana alitoka Norway, na ana siku nne tangu aingie hapa Tanzania. Alikaa karantini siku tatu na kuamua kutoroka.

Nyumba aliyokaa pia iko chini ya karantini na mganga mkuu wa wilaya atawapima wote wanaoishi katika nyumba hiyo.

Kasesela amesema kuna mwingine wiki iliyopita alitoroka karantini ya Tunduma na hadi sasa hawajui yuko wapi, lakini mtu huyo alikuwa Mmalawi.


Sent using Jamii Forums mobile app
NINA MASHAKA NA HIZI KESI ZA WATUHUMIWA WA ''COLONA'' KUTOROKA.
Mwisho tutakuja kuambiwa wale waliotoroka ndio wamesbabisha miambukizo yote hii wakati huo imeshafikia 500.
UMMY TICHA tuambie ukweli halihalisi ukoje. MFICHA UCHI.... MFICH UGONJWA? KIFO......
 
Changamoto ni aina ya karantini,endapo inawekwa watu zaidi ya mmoja kwenye chumba..
Mfano nimetoka Italia nikiwekwa Quarantine na mtu kutoka Sweden lazima atataka kutoroka maana hakuna imani juu ya yoyote, ata daktari anayepima huenda akawa na Corona..
 
Sawa mwanafunzi naona unajua kuandika sentensi kwa kiingereza.
Ni rahisi tu endapo wenye mamlaka wakiamua.Mm nimeshauri tu.
Kulikuwa na haja ya kuongeza hayo maneno mengine?

Haufahamu kama hili ni Taifa linaloendeshwa kwa misingi ya kisheria? Je kuna sheria yoyote inayosema anayetenda kosa hata la kufanya mauwaji ya halaiki apigwe risasi?

Come on you need to grow up a little bit 😟
 
Nani wa kulaumiwa katika hili?
Nani alaumiwe katika kutoroka kwa mtu aliyewekwa karantini ni mtorokaji mwenyewe. Tuwaache polisi wafanye kazi za maana zaidi. Watanzania tuelewe kwamba kuwekwa karantini ni kwa faida yako mwenyewe, na ndugu zako unaokutana nao, na Watanzania wengine kwa ujumla. Ndiyo maana unakuta nchi nyingine waziri mkuu au waziri anajiweka karantini mwenyewe baada ya kuhisi anaweza kuwa ameambukizwa. Baada ya siku husika kupita na hajaugua anatoka hadharani na kutangaza amemaliza karantini aliyojiwekea. Si aibu kwamba umekuwa karantini kwa kuhofia umeugua. Cha kuonea aibu ni kuwekwa lock-up kwa tuhuma ya kuhusika na jinai.
 
Kwahili Bora tuwataje tu majina, kumbe makonda alikuwa sahihi, mbowe asingetajwa angeendelea na maandamano yake
Ni sahihikabisa mtu katoka hapa mpakà Iringa kakutana na watu wangapi! Huko njiani kuchimba dawa mnakutana na watu gari tofauti, akimaliza hizo siku kama hajahadhirika ashitakiwe na kama atakuwa na maambukizi wampe chloroquine tu zakutafuta kenge huyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu aliyetoroka tunamlaum lakini hatujui kwa nini katoroka.. Mimi nahisi hakuwa na fedha za kutosha na hotelini unajihudumia kila kitu!. Ukikaa hotelini siku 14 bili utakayopewa hapo unaweza ukadondosha machozi. Mm nadhani serikali badala ya kuwaweka hotelini ingewatafutia sehemu ya gyarama ndogo in case ikitokea kuna raia wasio weza kumudu gharama za hotel


Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini wasitulie kusubilia janga lipite?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dogo nimesema wenye mamlaka wakiamua namaanisha wanaweza kupeleka muswada bungeni na kubadilisha sheria kisha ikawa kama nilivyoshauri na kuandika hapo juu.
Huwezi kusoma sentensi na ukaelewa kwa kina?
Kulikuwa na haja ya kuongeza hayo maneno mengine?

Haufahamu kama hili ni Taifa linaloendeshwa kwa misingi ya kisheria? Je kuna sheria yoyote inayosema anayetenda kosa hata la kufanya mauwaji ya halaiki apigwe risasi?

Come on you need to grow up a little bit 😟
 
Back
Top Bottom