Ifunda, Iringa: Moto ulioanzishwa na mpishi wa pombe wasababisha hasara ya zaidi Bilioni 1.5

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,454
3,417
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amesema Moto uliozuka Kijiji Cha Mfukulembe umeunguza zaidi ya nyumba 11 na mashamba ya miti yenye ukubwa wa zaidi ya ekari 811.

1.jpg

Aidha amebainisha kuwa hakuna mtu aliyepata madhara na chanzo cha moto huo isadikiwa kuwa mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Mama Ritha Kalinga alikuwa akipika pombe na moto ukaruka na kuingia kwenye mashamba na kusambaa.

2.jpg

Huku akionesha picha zake akiwa anatembelea kuangalia madhara ya moto na kuzungumza na wananchi wa kijiji Cha Mfukulembe kata ya Ifunda amesema hasara mpaka sasa kwa nyumba ni 7.4m na mashamba ya miti zaidi ya 1.5Billlion. 
Huyo mama mpika pombe ya kienyeji alipe hiyo hasara ya shilingi bilioni 1.5 upesi.Vinginevyo Hilo jumba lake na pipa lake la kupikia pombe lipigwe mnada.Yono Auction Mart jiandae kwenda kunadi. Mama Yono tenda hiyo ya kuuza hilo jumba la Mnyalu.
 
Huu moto sijui ulirukaje?

Sitasahau enzi hizo mama anapika pombe.

Ghafla pipa likaanza kujikunja (madhara ya atmospheric pressure) watabe wa physics mtaelewa hapa.

Then pipa likaruka kama bomu sema halikwenda mbali sana.

Fluid iliyokuwa ndani ikamwagika yote na pipa likajikunjakunja hovyo.

Nashukuru Mungu hatukupata madhara.
 
Changamoto kubwa ya biashara ya upandaji miti, ni hiyo ishu ya moto! Halafu ukutane na miti aina ya pines, hapo ni kama umemwagia tu mafuta ya petrol.
 
Huu moto sijui ulirukaje?

Sitasahau enzi hizo mama anapika pombe.

Ghafla pipa likaanza kujikunja (madhara ya atmospheric pressure) watabe wa physics mtaelewa hapa.

Then pipa likaruka kama bomu sema halikwenda mbali sana.

Fluid iliyokuwa ndani ikamwagika yote na pipa likajikunjakunja hovyo.

Nashukuru Mungu hatukupata madhara.
How!!!kwani lilikuwa limefungwa kila sehemu??
 
Back
Top Bottom