Aliyeteuliwa Ubunge akiwa mahabusu kuhojiwa Mahakamani leo

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Jopo la mawakili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) linatarajiwa kuendelea kuwahoji wabunge wa viti maalumu waliovuliwa uanachama wa chama hicho, huku kesho wakitarajiwa kumhoji Nusurati Hanje.

Mawakili hao wa Chadema wanaendelea kuwahoji baadhi ya wabunge hao kuhusiana na ushahidi wao waliouwasilisha mahakamani kwa njia ya viapo, katika kesi yao waliyoifungua Mahakama Kuu Masjala Kuu, kupinga kuvuliwa uanachama.

Katika kesi hiyo wabunge hao wanapinga uamuzi wa Baraza Kuu la Chadema wa Mei 11, 2022, kutupilia mbali rufaa walizozikata wakipinga uamuzi wa Kamati Kuu wa Novemba 27, 2020 kuwafukuza uanachama kwa tuhuma za kuapishwa kuwa wabunge bila ridhaa ya chama.

==========================

Wabunge hao 19 wanapinga uamuzi huo kwa utaratibu wa Mapitio ya Mahakama (Judicial Review), wakidai kuwa walifukuzwa isivyo halali kwa kuwa hakwakupewa haki ya kusikilzwa, hivyo wanaiomba mahakama hiyo iutengue.

Kabla ya kuanza usikilizwaji, mawakili wa Chadema waliomba mahakama na ikaridhia na kuwaamuru wabunge wanane kati yao, akiwemo Hanje, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), wafike mahakamani wawafanyie mahojiano kuhusiana na ushahidi wao huo.

Wengine walioitwa kuhojiwa ni aliyekuwa mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee; aliyekuwa makamu mwenyekiti Bawacha, Hawa Mwaifunga, aliyekuwa Katibu Bawacha, Grace Tendega na aliyekuwa mweka hazina Bawacha, Ester Matiko; Ester Bulaya, Jesca Kishoa, na Cecila Pareso.

Jina la Hanje kuwa ndiye atafuata kuhojiwa kesho limetajwa mahakamani leo na kiongozi wa jopo la mawakili wao, Ipilinga Panya, baada ya Mwaifunga kumaliza kuhojiwa.

Viongozi wa Chadema wamekuwa wakidai kuwa hawakuwahi kupendekeza, kusaini na kuwasilisha katika Tume Taifa ya Uchaguzi (Nec) orodha ya majina ya wabunge hao kuteuliwa kuwa katika nafasi hiyo, kama sheria inavyoelekeza.

Badala yake wamekuwa wakiwatuhumu kuwa walijipendekeza wenyewe na jina la Hanje likitawala mjadala.

Mara kadhaa Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amekuwa akikaririwa na vyombo vya habari akidai kuwa Hanje aliyekuwa mahabusu akikabiliwa na kesi ya jinai, anayoiita ya kubambikiwa, alitolewa mahabusu Novemba 23, 2020 usiku ili kesho yake aende kuapishwa.

Alidai kuwa uteuzi wa Tume ulifanyika Novemba 20, 2020 lakini yeye Hanje alitolewa Novemba 23, huku akihoji kuwa fomu yake aliijaza lini na hakimu aliyemuapisha kama Sheria ianvyoelekeza alikuwa wapi, na kwamba inadhihirisha ni kazi ya mfumo.

Hata hivyo wakati akihojiwa, Tendega ambaye alikuwa wa kwanza kuhojiwa akifuatiwa na Mwaifunga, pamoja na mambo mengine alidai kuwa wakati walipokaa kupendekeza majina ya wagombea wa viti maalum, Mnyika aliwapelekea majina 10 kutoka Bavicha.

Alidai kuwa miongoni mwa majina hayo lilikuwemo jina la Hanje na kwamba aliwasisitiza kuwa jina la Hanje lisiachwe kupendekezwa kuteuliwa katika nafasi hiyo.

Bila shaka kuhojiwa kwake Hanje kesho ni jambo linalosubiriwa sana na wanachama, wafuasi wa Chadema na wadau wote wanaofuatilia kesi hiyo kutaka kujua ni maswali gani Hanje ataulizwa na atajibu nini.

Mbali na Chadema kupitia Bodi yake ya Wadhamini, wadaiwa wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambaye pia anasimama kwa niaba ya Bunge la Tanzania na Nec.
 
Hivi kwa nini CHADEMA wanahangaika na hii kesi? Mimi naona ingetosha kwa wao kuwafuta uanachama wale na kumwandikia speaker kuwa hao si wanachama wao. Then wakanyamaza.

Naona kwa kwenda kwao mahakani wanafanya kazi ambayo si ya kwao...wala haiwahusu ila mbaya zaidi wanamsaidia speaker na ma serikali kutimiza agenda zao kirahisi.
 
Hamna kitu hapo, mnapoteza muda tuu.
JamiiForums-900505565.jpg
 
Hivi kwa nini CHADEMA wanahangaika na hii kesi? Mimi naona ingetosha kwa wao kuwafuta uanachama wale na kumwandikia speaker kuwa hao si wanachama wao. Then wakanyamaza.

Naona kwa kwenda kwao mahakani wanafanya kazi ambayo si ya kwao...wala haiwahusu ila mbaya zaidi wanamsaidia speaker na ma serikali kutimiza agenda zao kirahisi.
Mkuu hao vicheche 19 ndiyo waliofungua kesi siyo Chadema na Chadema wanakwenda kuitikia wito wa Mahakama. Hao vicheche walishafukuzwa uanachama na Spika anayo taarifa rasmi. Ngoja kesi iendelee ili dunia ijue kuwa Serikali yetu inaendeshwa kihuni na Watanzania waone jinsi kodi zao zinavyotumika kiboya.
 
Hivi kwa nini CHADEMA wanahangaika na hii kesi? Mimi naona ingetosha kwa wao kuwafuta uanachama wale na kumwandikia speaker kuwa hao si wanachama wao. Then wakanyamaza.

Naona kwa kwenda kwao mahakani wanafanya kazi ambayo si ya kwao...wala haiwahusu ila mbaya zaidi wanamsaidia speaker na ma serikali kutimiza agenda zao kirahisi.
Unajua kinachoendelea kweli? Sio Chadema waliopeleka shauri mahakamani. Chadema ni walalamikiwa (respondents?
 
Jopo la mawakili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) linatarajiwa kuendelea kuwahoji wabunge wa viti maalumu waliovuliwa uanachama wa chama hicho, huku kesho wakitarajiwa kumhoji Nusurati Hanje.

Mawakili hao wa Chadema wanaendelea kuwahoji baadhi ya wabunge hao kuhusiana na ushahidi wao waliouwasilisha mahakamani kwa njia ya viapo, katika kesi yao waliyoifungua Mahakama Kuu Masjala Kuu, kupinga kuvuliwa uanachama.

Katika kesi hiyo wabunge hao wanapinga uamuzi wa Baraza Kuu la Chadema wa Mei 11, 2022, kutupilia mbali rufaa walizozikata wakipinga uamuzi wa Kamati Kuu wa Novemba 27, 2020 kuwafukuza uanachama kwa tuhuma za kuapishwa kuwa wabunge bila ridhaa ya chama.

==========================

Wabunge hao 19 wanapinga uamuzi huo kwa utaratibu wa Mapitio ya Mahakama (Judicial Review), wakidai kuwa walifukuzwa isivyo halali kwa kuwa hakwakupewa haki ya kusikilzwa, hivyo wanaiomba mahakama hiyo iutengue.

Kabla ya kuanza usikilizwaji, mawakili wa Chadema waliomba mahakama na ikaridhia na kuwaamuru wabunge wanane kati yao, akiwemo Hanje, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), wafike mahakamani wawafanyie mahojiano kuhusiana na ushahidi wao huo.

Wengine walioitwa kuhojiwa ni aliyekuwa mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee; aliyekuwa makamu mwenyekiti Bawacha, Hawa Mwaifunga, aliyekuwa Katibu Bawacha, Grace Tendega na aliyekuwa mweka hazina Bawacha, Ester Matiko; Ester Bulaya, Jesca Kishoa, na Cecila Pareso.

Jina la Hanje kuwa ndiye atafuata kuhojiwa kesho limetajwa mahakamani leo na kiongozi wa jopo la mawakili wao, Ipilinga Panya, baada ya Mwaifunga kumaliza kuhojiwa.

Viongozi wa Chadema wamekuwa wakidai kuwa hawakuwahi kupendekeza, kusaini na kuwasilisha katika Tume Taifa ya Uchaguzi (Nec) orodha ya majina ya wabunge hao kuteuliwa kuwa katika nafasi hiyo, kama sheria inavyoelekeza.

Badala yake wamekuwa wakiwatuhumu kuwa walijipendekeza wenyewe na jina la Hanje likitawala mjadala.

Mara kadhaa Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amekuwa akikaririwa na vyombo vya habari akidai kuwa Hanje aliyekuwa mahabusu akikabiliwa na kesi ya jinai, anayoiita ya kubambikiwa, alitolewa mahabusu Novemba 23, 2020 usiku ili kesho yake aende kuapishwa.

Alidai kuwa uteuzi wa Tume ulifanyika Novemba 20, 2020 lakini yeye Hanje alitolewa Novemba 23, huku akihoji kuwa fomu yake aliijaza lini na hakimu aliyemuapisha kama Sheria ianvyoelekeza alikuwa wapi, na kwamba inadhihirisha ni kazi ya mfumo.

Hata hivyo wakati akihojiwa, Tendega ambaye alikuwa wa kwanza kuhojiwa akifuatiwa na Mwaifunga, pamoja na mambo mengine alidai kuwa wakati walipokaa kupendekeza majina ya wagombea wa viti maalum, Mnyika aliwapelekea majina 10 kutoka Bavicha.

Alidai kuwa miongoni mwa majina hayo lilikuwemo jina la Hanje na kwamba aliwasisitiza kuwa jina la Hanje lisiachwe kupendekezwa kuteuliwa katika nafasi hiyo.

Bila shaka kuhojiwa kwake Hanje kesho ni jambo linalosubiriwa sana na wanachama, wafuasi wa Chadema na wadau wote wanaofuatilia kesi hiyo kutaka kujua ni maswali gani Hanje ataulizwa na atajibu nini.

Mbali na Chadema kupitia Bodi yake ya Wadhamini, wadaiwa wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambaye pia anasimama kwa niaba ya Bunge la Tanzania na Nec.
MNYIKA HAWEZI KUFANYA UPUMBAVU HUO hawana Hoja zaidi ya kutaja taja Watu kuhusika lakini Uongo una Mwisho wake FOMU husika zitawekwa Hadharani
 
Hivi kwa nini CHADEMA wanahangaika na hii kesi? Mimi naona ingetosha kwa wao kuwafuta uanachama wale na kumwandikia speaker kuwa hao si wanachama wao. Then wakanyamaza.

Naona kwa kwenda kwao mahakani wanafanya kazi ambayo si ya kwao...wala haiwahusu ila mbaya zaidi wanamsaidia speaker na ma serikali kutimiza agenda zao kirahisi.
Wao waliofukubmzwa ndio wakioishitaki Chadema sio chadema kuwashtaki.
 
Hivi kwa nini CHADEMA wanahangaika na hii kesi? Mimi naona ingetosha kwa wao kuwafuta uanachama wale na kumwandikia speaker kuwa hao si wanachama wao. Then wakanyamaza.

Naona kwa kwenda kwao mahakani wanafanya kazi ambayo si ya kwao...wala haiwahusu ila mbaya zaidi wanamsaidia speaker na ma serikali kutimiza agenda zao kirahisi.
Itakuwa hili sakata hujalifuatilia vizuri tangia mwanzo wa uteuzi wa Nov 20,2020 na maamuzi yaliyochukuliwa na kamati kuu ya CHADEMA. Chama kilishamalizana nao kitambo, wao ndio waliofungua case wakiongozwa na Halima Mdee kupinga kufukuzwa kwao chamani bila rufaa zao kusikilizwa.
 
Hivi kwa nini CHADEMA wanahangaika na hii kesi? Mimi naona ingetosha kwa wao kuwafuta uanachama wale na kumwandikia speaker kuwa hao si wanachama wao. Then wakanyamaza.

Naona kwa kwenda kwao mahakani wanafanya kazi ambayo si ya kwao...wala haiwahusu ila mbaya zaidi wanamsaidia speaker na ma serikali kutimiza agenda zao kirahisi.

Wao ndiowameenda mahakamani sio CHADEMA. Halafu CHADEMA haina nia ya kuteua wabunge wengine.
 
Documents zimeshafojiwa kuonyesha kuwa alikuwa tayari ameshasamehewa/ achiwa kutoka gerezani
 
Back
Top Bottom