Aliyeokolewa mgodini baada ya siku 41, amuulizia Lowassa

Aliyeokolewa mgodini baada ya siku 41, amuulizia Lowassa

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,728
Reaction score
62,878
Kutoka Magazetini.

Watu watano waliookolewa kati sita waliokuwa wamefukiwa na kifusi kwa takriban siku 41 muda ambao tulikuwa kwenye mchakato wa uchaguzi Mkuu, wamehoji kwa nini Lowassa hakuwa rais.

Chanzo: Habari Leo na Tanzania Daima.

Aliyeokolewa mgodini, amuulizia Lowassa
​

lowassa..jpg

Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa
​

Kwa ufupi
Juhudi za kuwaokoa wachimbaji hao zilifanyika lakini zikasitishwa baada ya muda kutokana na kutokuwapo na dalili za mafanikio

Kahama
Mmoja wa watu waliokuwa wamefunikwa na kifusi chini ya ardhi kwa siku 41, juzi jioni alizinduka na muda mfupi baadaye akaulizia kama aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa ameshinda Uchaguzi Mkuu.

Joseph Bulule ni mmoja kati ya wachimbaji watano waliokuwa wamefukiwa na kifusi kwenye machimbo ya Nyangalata wilayani Kahama tangu Oktoba 5, siku tatu baada ya Lowassa kurejesha fomu za kuwania urais kwa tiketi ya CHADEMA.

Juhudi za kuwaokoa wachimbaji hao zilifanyika lakini zikasitishwa baada ya muda kutokana na kutokuwapo na dalili za mafanikio, kabla ya jitihada hizo kuanza tena baada ya wachimbaji wengine kusikia sauti za wenzao wakiomba msaada kutoka chini ardhi.

Bulule, ambaye amelazwa Hospitali ya Halmashauri ya Kahama, aliuliza swali hiyo mbele ya waandishi wa habari baada ya kupata fahamu.

"Nani alishinda kwenye uchaguzi wa Rais," aliuliza waandishi akiwa amelala kitandani. "Lowassa alishinda? Maana sisi tangu Oktoba 5, tulipofukiwa hatujui kinachoendelea. Uchaguzi umetukuta ndani ya mashimo na hatujui matokeo ya uchaguzi."

Uchaguzi wa Rais na wabunge ulifanyika siku ishirini baadaye wakati juhudi za kuwaokoa zikiwa zimeshasitishwa. Katika matokeo ya uchaguzi huo, mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli alishinda kwa kupata kura milioni 8.88, huku Lowassa, aliyekuwa anaungwa mkono na vyama vinne, akishika nafasi ya pili kwa kupata kura milioni 6.07
Baada ya waandishi wa habari kumueleza kuwa aliyeshinda ni Dk Magufuli, mchimbaji madini huyo mdogo alionekana kukosa raha.

Kwa mujibu wa mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Joseph Ngowi jana mchana watu hao watano walianza kupatiwa chakula chepesi, kama uji wenye maji mengi ambayo alisema yanasaidia utumbo kunyanyuka baada ya kukaa siku 41 bila kupata chakula.

Alisema baada ya hatua hiyo wataanza kupewa chakula laini na baada ya siku saba wataanzza kula chakula cha kawaida. Alisema wote watano wapo kwenye usimamizi wa madaktari pamoja na wataalamu.

Wakiwa kwenye mgodi Oktoba 5, kifusi kilikatika na kufunika mlango wa kutokea, hali iliyofanya waishi siku 41 kwa kunywa maji, kula mende, vyura na magamba ya miti hadi walipookolewa Jumapili iliyopita wakiwa hai.


CHANZO: Mwananchi
 
hii ndio africa, nkurunzinza burundi kapata 87% ila mpaka leo kuna vurugu na mauaji sasa sijui hao wanaompinga wako wapi hapo

chezea chaguzi za africa..............hah hah hahah hahah
 
da yawezekana Lowassa alishnda kweli uchaguzi
 
ha ha ha ha.
waambieni hii ndio democrisis ya africa. chaguo la wengi sio chaguo la wapiga dili.
ni viongozi wachache sana wenye busara ya kukubali kushindwa akiwemo Wade,Jonathan, Banda.
wengine wote ni wapiga dili za kuuza nchi zetu
 
Kama lowassa angekuwa rais,siku ile ile anaapishwa angeagiza kitendo cha maafa waje kuwaopoa dead or alive,wamerudi hawa hawa wa kijani waliowatelekeza mfie mashimoni mpaka iliporokea bahati wachimbaji wenzenu wakawasikia!
 
Nina uhakika hata kama angepiga kura, kura yake ingeibiwa tu.

Kwa hiyo nyie hata kura zenu hamuwezi kulinda. Itakuweje kulinda watz na mali zao. Au uhuru wao au utu wao au utamaduni wao. Au ardhi yao au madin yao
 
Huenda angekuwepo apige kura Lowassa angeshindq, bahati mbaya alikuwa shimoni!
 
Ni jambo la kusubiri kutimia tu. Lowasa ni Rais,muda utajibu.
 
Tanzania Daima hata siku ya kuapishwa magufuli halikuandika chochote kuhusu kuapishwa Raisi.
 
Lowassa ashinde kwa tume hii chini ya Lubuva?ajiulize kwanini mpk Leo Zanzibar haina Rais?
 
Kwa hiyo nyie hata kura zenu hamuwezi kulinda. Itakuweje kulinda watz na mali zao. Au uhuru wao au utu wao au utamaduni wao. Au ardhi yao au madin yao
Kwa hiyo wewe unawapongeza wezi kwa vile wameiba bila kukamatwa.
 
Hiyo ndio power ya upako wa 'mahaba' ya Lowassa huwafikia hata wale walio kufani chini ardhini🙂 Mahaba ya ajabu kabisa haya!
 
Kutoka Magazetini.

Watu watano waliookolewa kati sita waliokuwa wamefukiwa na kifusi kwa takriban siku 41 muda ambao tulikuwa kwenye mchakato wa uchaguzi Mkuu, wamehoji kwa nini Lowassa hakuwa rais.

Chanzo: Habari Leo na Tanzania Daima.

Tanzania Daima!! Harufu tupu!! kama kimba vile.
 
Back
Top Bottom