Aliyekudhuru ndo akuhudumie?

Aliyekudhuru ndo akuhudumie?

haujaeleweka mkuu!!

unasema serikali ya magufuli inahusika, kisha unalalmika hawajakuhudumia na unataka wachunguze??

does that makes sense?? naona umeenda mbali sana

assumption ni kuwa serikali inahusika!!! sasa anacholalamika Lissu ni nini ??

..na serekali nayo inasema haihusiki.

..lakini inamnyima huduma.

..na pia haichunguzi.

..halafu tunashangaa ikilaumiwa!!

Nyani Ngabu
 
Binafsi nacho-DHANI ni kuwa kulalamika huko kwa namna mbili ni kucheza karata mbili kwa mpigo.
Karata ya kwanza:
Kumtuhumu mkuu na serikali yake ina impact yake. (iwe ni kweli au la)
Karata ya pili:
Kulalamika serikali na bunge kiujumla hazijamuhudumia ni namna ya kutaka kuthibitisha madai ya karata ya kwanza. Na pia kuuboresha mtego.

Ni mchezo tu wa kuhakikisha kwamba kete lazima iliwe.

Pamoja na yaliyomtokea Lissu, naamini kuna part yake na ya watu wa karibu yake ambayo inachukua hii kama political opportunity.

I think we should just sit back and enjoy the game...
Only couple of pawns are left...
Soon, the Kings will move.
 
Ukituhumiwa huwezi kujichunguza mwenyewe. Baada ya Lissu kusema aliyosema ni wazi sasa serikali haipaswi kutumia vyombo vyake kufanya upelelezi juu ya nani kahusika.

Ni muda muafaka sasa wa kuleta wachunguzi huru ili watoe majibu huru.
 
Kama wenye akili wengi nawe ni mmoja wapo basi hilo kundi la "wenye akili" hilo sio jina sahihi la kuwaita bali "wenye upumbavu" wengi.
Kama washambuliaji lilikuwa kundi la wahuni ilikuwaje waingie kwenye makazi ya viongozi bila hofu na walinzi wawe hawapo siku hiyo? CCTV ziko wapi na nani kazing'oa? Lazima uwe kwenye kundi hilo la "wenye upumbavu" wengi ndio huwezi kujiuliza maswali kama hayo.
Wenye akili nyingi huwa hawafikiri in a simple way kama ulivyofanya. They think in a complex way wakiangalia all possible circumstances. Kwa mfano:
1. Saa hizo wabunge wengi walikuwa wanarejea kwenye eneo hilo walilopanga kwenda kupata chakula cha mchana kwenye nyumba zao. Eneo lina nyumba nyingi ila geti la kuingilia eneo hilo ni moja likiwa na mlinzi mmoja (armed or unarmed). Magari yaliyobeba hao waheshimiwa yanaingia kila baada ya muda wa dakika tano au kumi. Gari la Mh Lissu linakuja likiwa limeongozana na gari la waheshimiwa wengine (Nissan nyeupe). Kwa mazoea yetu waheshimiwa hawa wabunge na wengine huwa hawapendi mlinzi wa geti asimamishe magari yao getini na kuanza kukagua waliomo ndani na kuwahoji wao ni akina nani. Kwetu tendo hilo la kudodosa waheshimiwa ni ukosefu wa nidhamu kwa mlinzi mwenye tabia kama hiyo. Kwetu nidhamu ya mlinzi ni kufungua geti mara moja anapoona gari la mheshimiwa linapokuja ili mheshimiwa na alioambatana nao waweze kuingia bila bughudha ya kufanyiwa thorough search! Ndivyo watanaznia tulivyo, tumelemazwa na amani. Kwa kutumia mwanya huo 'waheshimiwa' waliokuwa kwenye shangingi nyeupe iliyoongozana na shangingi nyeusi ya Mh Lisu waliingia kwa pamoja ndani ya eneo hilo na kusimamisha magari yao. Then in seconds mmoja wa waliokuwemo kwenye lile gari jeupe alitoka na kuanza ku spray bullets from a heavy automatic gun!! Wenye akili wanaona scnerio ilivyokuwa kihalisia na reaction ya huyo au hao walinzi wa geti la waheshimiwa kama alikuwa au walikuwa karibu na risasi zilipokuwa zinamiminwa. Reflex reaction kwa askari yo yote kwenye such a situation ni kulala chini and craw fast to a nearet cover to save his life. Hayo mambo yalitokea in seconds na hao assillants kutokomea, geti likiwa bado liko wazi na magari mengine ya waheshimiwa wabunge hayajafika kwenye eneo hilo kuja kupata chakula cha mchana.

Ni ujinga kuamini kuwa walinzi waliokuwapo eneo hilo la geti na sehemu zingine hawakuhojiwa na polisi. Pia ni upumbafu kufikiri kuwa mlinzi au walinzi waliokuwepo getini wangaliweza kujibu mapigo hayo ya risasi. Vita ya risasi si lelemama, adui yako akikuwahi unachoweza kufanya kama una bahati ni ku take cover. Pia ni ujinga kuamini kuwa kwa sababu eneo hilo linalindwa na askari basi ni salama kwa asilimia 100%. Hata kambi za jeshi na vituo vya polisi vimewahi kumiminiwa risasi na askari kuuawa mara nyingi tu, sasa sembuse hilo eneo na kwa mazingira yetu kama hayo.

Pia ni upumbafu kuamini kuwa uwepo wa CCTV kwenye eneo hilo ndiyo solution ya kuwezesha kuonekana sura za wahalifu hao. Even the most expensive high quality high definition external rotating CCTV cameras hazina uwezo wa kutoa clear images at all 360 degrees anytime and at all distances from object. When the object is more than 3m from camera huwezi pata clear images za kuweza kutambua sura za hao wahalifu. Wenye akili wanajua kwamba the effectiveness as a security tool kwa kunasa sura za wahalifu wa aina hii is almost zero. Tumeshudia huko ulaya magaidi yanavyamia na kushambulia kwa risasi kumbi za burudani na kuua watu, cctvs zao hazikuwa na msaada wa maana katika kuwatambua wahalifu hao. Hapa kwetu ambapo tulizoea madili hiyo kampuni iliyolipwa mabillion kufunga hizo CCTV kwenye eneo hilo la serikali si ajabu kuwa quality ya hizo cameras zilizofungwa ni za quality ya lugumi, hivyo aidha no images or just blurred images.

Isitoshe siku hizi ili kukwepa kuonekana sura zao kwenye ma cctv au kwa watu wengine, wahalifu wa aina hii huvaa masks au miwani myeusi + kofia zilizoshushwa chini kuficha sura zao. Mtu pekee anayejua sura za assaillants hawa pamoja na gari yao ni dereva wa Lissu. Yeye kwa maneno yake alishasema hata kabla ya hitimisho la tukio kwamba ameshawaona mara nyingi tu kuanzia Dar. Wameshawahi hata kukaa kwenye bustani moja ya hoteli fulani huko Dar na wahalifu hao wakiwa kwenye mishe mishe hiyo ya kutaka kumzuru Lissu. Bahati nzuri siku hiyo wakaweza kuwakwepa watu hao na wakatoa majigambo kwenye vyombo vya habari kwa mafanikio hayo.
Dreva wa Lissu anawafahamu vizuri sana watu hao kwa sura na hata namba ya gari lao analijua (ingawa inaweza kuwa feki). Hata walipokuwa wameficha sura zao kwa kofia pale kwenye eneo la tukio aliweza kuwatambua kuwa ni wale wale.

Sasa watu wenye akili inawawia ngumu kuelewa hicho kigugumizi cha huyo dereva kugoma kwenda kuisaidia polisi katika uchunguzi wa hilo tukio sababu yake ni nini haswa? Dereva amefichwa, huko Nairobi haonekani na huku kwetu haonekani. Mke na watoto wake ha2amuoni. Tuelewe nini sasa? Jee naye katekwa na kama katekwa ni nani huyo kamteka kama siyo chama chake. Tunaambiwa eti atasaidia tu jeshi la scotland yard la uingereza au la FBI la amerika lakini siyo jeshi hili la Siro katika uchunguzi wa tukio hili! Ni shida bin shida. Ni siasa za kupambana na serikali iliyowekwa kihalali na watanzania walio wengi!
 
Dr Akili,

..TL alishambuliwa na watu wawili wenye silaha.

..pia anasema eneo hilo hulindwa masaa 24, lakini siku ya tukio kulikuwa hakuna ulinzi.

..sasa haijulikani ni sababu zipi zilizopelekea walinzi wasiwepo siku ya shambulizi.

NB:

..pia kama walinzi reaction yao ni kukimbia wakiona kuna shambulizi, hata kama siyo wao wanaoshambuliwa, basi tuna kazi kubwa kwelikweli.
 
Nitangulize maneno machache juu ya ujinga [ujinga siyo tusi] wangu juu ya nani alihusika na jaribio la kutaka kuondoa uhai wa Tundu Lissu. Mimi sijui kabisa nani alihusika. Lakini pia najua tofauti kati ya kujua, kuhisi, kudhani, na kusadiki. Wenye akili mtakuwa mmenipata, natumai.

Sasa bana, jana Mh. Lissu kaongea na waandishi wa habari huko Nairobi, Kenya, ambapo kimsingi kamtuhumu rais Magufuli na CCM kuhusika moja kwa moja na hilo jaribio la mauaji dhidi yake.

Upande wa serikali naona umeamua kuchukua ‘the high road’ kwa kukataa kulumbana na ‘mgonjwa’, kama ulivyosomeka ule ujumbe wa msemaji wa serikali. Nikiri tu kuwa ule ujumbe ulinichekesha sana. Ulikuwa mfupi na wenye kueleweka.

Sasa kwa vile Mh. Lissu kaamua kutoa tuhuma zake hadharani namna ile, he is now fair game!

Yeye na makamanda wenzake hawaeleweki. Hawaeleweki kwa sababu, kwa upande mmoja wanadai kuwa serikali, rais Magufuli, vyombo vya dola, na CCM ndo walihusuka na mpango mzima. Na kwa upande mwingine wanalialia kuwa eti mpaka sasa bunge halijampa haki zake, mara sijui polisi hawafanyi uchunguzi wa nani aliyetaka kumuua na blah blah zingine kama hizo.

Ni dhahiri kuwa Lissu anaingiza siasa kwenye hizo tuhuma na shutuma zake. Vivyo hivyo, huenda hata upande wa serikali nao umeamua kucheza siasa.

Now it’s on. Nasubiri tu siku Magu aje alizungumzie hilo suala. Makamanda mtalia na kusaga meno maana bwana yule mdomo wake hauna breki.

Nyie chekeleeni tu hivyo vijembe vya huyo kamanda wenu Lissu kwa sasa. Lakini siku Magu atayoamua kujibu mapigo mtatafutana.

Muwe na Jumamosi njema.
Kwani huyo mr wako hapo super market mdomo wake una breki?!!
 
Ukituhumiwa huwezi kujichunguza mwenyewe. Baada ya Lissu kusema aliyosema ni wazi sasa serikali haipaswi kutumia vyombo vyake kufanya upelelezi juu ya nani kahusika.

Ni muda muafaka sasa wa kuleta wachunguzi huru ili watoe majibu huru.

wanaletwa na nani?
 
wanaletwa na nani?

..kama imepita miezi 3 tangu shambulio litokee, na bado Polisi hawana majibu, basi ni vema serekali ikaomba msaada toka nchi marafiki. kila mtu angependa ukweli ujulikane na kuliko kukaa ktk hali ya kushutumiana.
 
sasa unaanzaje kumshutumu mtu ambaye hauna uhakika?

mwenye shida hasa ya kujua nani alimpiga risasi lissu, ni lissu mwenyewe, sio serikali...

aliyeshindwa kuziba mdomo wake ni lissu na wenzake
 
..mtu yeyote yule ambaye amesumbuliwa na serekali kama ilivyotokea kwa TL, akifikwa na janga kama lile, ni lazima atahisi ni serekali ndiyo wamemtendea ubaya.

..kwa hiyo tusimlaumu sana TL. Mambo aliyoyapitia hata kabla ya kupigwa risasi, ni wachache wanaweza kuyastahimili.

..lingine ni kwamba Jeshi la Polisi lazima lichunge na kulinda heshima yake kwa weledi mkubwa.

..How do they do that? Ni kwa kutenda HAKI wakati wote, na kwa watu wote.

..Jeshi la Polisi nalo lina interest kubwa ya kujua nani ametenda unyama ule. Jaribio lile limetokea ktk eneo wanaloishi viongozi ambao wanalindwa saa zote.

..Sasa kama kumetokea shambulizi ktk eneo hilo na Polisi wameshindwa kuwakamata wahusika basi kuna tatizo ktk utendaji na weledi wa jeshi letu. Heshima yao imechafuka.

..They have to do something, and start acting like they are doing something.
 
Huna akili, kama hivyo ndivyo mbona wachunguzi huru mnakataa ambao wangewaumbua hao walio mzunguka? mbona siku ile walinzi waliondolewa na hatujaambiwa kwa nini hawakuwapo? mbona kamera za CCTV zilizokuwepo zimeondolewa na haisemwi ni nani kaziondoa? kwa hiyo hao walio mzunguka Lissu ndio wameenda na kuondoa kamera kwa jirani waziri na kwa Naibu spika?
Kwa hoja kama hii yako mtu akikuita mpumbavu atakuwa kakutukana? nadhani jibu ni hapana bali atakuwa amekuelezea ulivyo
Jina lako linaakisi akili zako na ndio sababu ukaandika hivyo.
 
Kama wenye akili wengi nawe ni mmoja wapo basi hilo kundi la "wenye akili" hilo sio jina sahihi la kuwaita bali "wenye upumbavu" wengi.
Kama washambuliaji lilikuwa kundi la wahuni ilikuwaje waingie kwenye makazi ya viongozi bila hofu na walinzi wawe hawapo siku hiyo? CCTV ziko wapi na nani kazing'oa? Lazima uwe kwenye kundi hilo la "wenye upumbavu" wengi ndio huwezi kujiuliza maswali kama hayo.
Wenye akili nyingi huwa hawafikiri in a simple way kama ulivyofanya. They think in a more complex way wakiangalia all possible circumstances or scnerios. Mfano wa possible scnerio mojawapo ni huu:

Saa hizo wabunge wengi walikuwa wanarejea kwenye eneo hilo walilopanga kwenda kupata chakula cha mchana kwenye nyumba zao. Eneo lina nyumba nyingi ila geti la kuingilia eneo hilo ni moja likiwa na mlinzi mmoja (armed or unarmed). Magari yaliyobeba hao waheshimiwa yanaingia kila baada ya muda wa dakika tano au kumi. Gari la Mh Lissu linakuja likiwa limeongozana na gari la waheshimiwa wengine (Nissan nyeupe). Kwa mazoea yetu waheshimiwa hawa wabunge na wengine huwa hawapendi mlinzi wa geti asimamishe magari yao getini na kuanza kukagua waliomo ndani na kuwahoji wao ni akina nani. Kwetu tendo hilo la kudodosa waheshimiwa ni ukosefu wa nidhamu kwa mlinzi mwenye tabia kama hiyo. Kwetu nidhamu ya mlinzi ni kufungua geti mara moja anapoona gari la mheshimiwa linapokuja ili mheshimiwa na alioambatana nao waweze kuingia bila bughudha ya kufanyiwa thorough search! Ndivyo watanaznia tulivyo, tumelemazwa na amani. Kwa kutumia mwanya huo 'waheshimiwa' waliokuwa kwenye shangingi nyeupe iliyoongozana na shangingi nyeusi ya Mh Lisu waliingia kwa pamoja ndani ya eneo hilo na kusimamisha magari yao. Then in seconds mmoja wa waliokuwemo kwenye lile gari jeupe alitoka na kuanza ku spray bullets from a heavy automatic gun!! Wenye akili wanaona scnerio ilivyokuwa kihalisia na reaction ya huyo au hao walinzi wa geti la waheshimiwa kama alikuwa au walikuwa karibu na risasi zilipokuwa zinamiminwa. Reflex reaction kwa askari yo yote kwenye such a situation ni kulala chini and craw fast to a nearet cover to save his life. Hayo mambo yalitokea in seconds na hao assillants kutokomea, geti likiwa bado liko wazi na magari mengine ya waheshimiwa wabunge hayajafika kwenye eneo hilo kuja kupata chakula cha mchana.

Ni ujinga kuamini kuwa walinzi waliokuwapo eneo hilo la geti na sehemu zingine hawakuhojiwa na polisi. Pia ni upumbafu kufikiri kuwa mlinzi au walinzi waliokuwepo getini wangaliweza kujibu mapigo hayo ya risasi. Vita ya risasi si lelemama, adui yako akikuwahi unachoweza kufanya kama una bahati ni ku take cover. Pia ni ujinga kuamini kuwa kwa sababu eneo hilo linalindwa na askari basi ni salama kwa asilimia 100%. Hata kambi za jeshi na vituo vya polisi vimewahi kumiminiwa risasi na askari kuuawa mara nyingi tu, sasa sembuse hilo eneo na kwa mazingira yetu kama hayo.

Pia ni upumbafu kuamini kuwa uwepo wa CCTV kwenye eneo hilo ndiyo solution ya kuwezesha kuonekana sura za wahalifu hao. Even the most expensive high definition external CCTV camera haiwezi kunasa 360 degrees view at any one time na clearity ya hizo picha ni hafifu if the object is more than 1 meatre from the camera. Ni ujinga kuamini kuwa polisi hawakuchunguza hizo images za CCTV cameras zilizo kuwa karibu na eneo. Wenye akili wanaamini images hizo kama zilinaswa zilikuwa blurred images kwani tukio lilitokea more than 1m from the cameras. At worst wanaamini kwa mazoea ya upiga dili wa nchi yetu ulipokuwa umefikia, huyo mkandrasi aliyepewa tenda ya mabilioni ya kufunga hizo CCTV alifunga aina ya Lugumi. Isitoshe wahalifu kukwepa sura zao kuonekana kwenye ma CCTV au kwa watu wengine huwa wanavaa masks au miwani + kofia zilizoshushwa chini kuficha sura zao.

Wenye akili wanaamini mtu pekee anayejua sura za hao wahuni pamoja na gari lao ni dereva wa Lissu pekee kwani kwa maneno yake alishawaona mara nyingi kuanzia Dar hadi Dodoma wakimfuatilia Lissu. Wamewahi hata kukaa pamoja nao kwenye bustani ya hotel moja huko Dar wakiwa kwenye mishemishe hizo, jambo lililomfanya Lissu atoe taarifa kwenye vyombo vya habari. Watu wenye akili wanashindwa kuelewa sababu cha kigugumizi cha dereva huyu kuogopa kwenda kusaidia jeshi la polisi katika uchunguzi wa maovu haya. Eti atatoa ushirikiano kwa jeshi la scotland yard au la FBI ya america pekee na si kwa jeshi hili la afande Sirro! Kweli chadema sasa ni chama cha mapambano dhidi ya serikali iliyowekwa madarakani kihalali na wananchi walio wengi. It is a confo
Dr Akili,

..TL alishambuliwa na watu wawili wenye silaha.

..pia anasema eneo hilo hulindwa masaa 24, lakini siku ya tukio kulikuwa hakuna ulinzi.

..sasa haijulikani ni sababu zipi zilizopelekea walinzi wasiwepo siku ya shambulizi.

NB:

..pia kama walinzi reaction yao ni kukimbia wakiona kuna shambulizi, hata kama siyo wao wanaoshambuliwa, basi tuna kazi kubwa kwelikweli.
Nani kakwambia kwamba hao walinzi hawakushambuliwa? Hivi wewe ulishaona ukiwa karibu na K47 with a full magazine inavyotema risasi in burst gear operation? Nina hakika wewe reflex reaction yako itakuwa ni kujinyea, kujikojolea, shahawa kukutoka na kuzimia bila hata hizo risasi ku kupata!!! It is no joke my friend. Zione kwenye movie tu na kudhani ni burudani. It is a catastrophy or disaster in the real meaning. Full magazine za SMG ni risasi 30 ile ya K47 ni risasi 47. Silaha iliyotumika kwenye tukio la Lissu ilikuwa K47 kwani risasi zilizoweza kuhesabika kwenye tukio ni 38 na lazima kuna zingine zilizowakosa kosa walinzi hao na wengine waliokuwa karibu na eneo hilo kwani mtumiaji wa bunduki hiyo hakuwa na uwezo wa kulenga shabaha. Mtumiaji wa bunduki hiyo angalikuwa ni trained wa shabaha story hii ingalikuwa ni ya kutisha ile mbaya - walinzi wote na watu wengine waliokuwa karibu pamoja na Lisu na dereva wake wangali rest in peace hapo hapo!!! K47 ni muziki usio na mchezo kwa mtu anayeijua kuitumia barabara. Hata kama kikosi cha FFU kingalikuja kwenye eneo hilo kama kisipochukua tahadhari ya kutosha kinaweza chote kikawa rested in peace!
 
Wenye akili nyingi huwa hawafikiri in a simple way kama ulivyofanya. They think in a complex way wakiangalia all possible circumstances. Kwa mfano:
1. Saa hizo wabunge wengi walikuwa wanarejea kwenye eneo hilo walilopanga kwenda kupata chakula cha mchana kwenye nyumba zao. Eneo lina nyumba nyingi ila geti la kuingilia eneo hilo ni moja likiwa na mlinzi mmoja (armed or unarmed). Magari yaliyobeba hao waheshimiwa yanaingia kila baada ya muda wa dakika tano au kumi. Gari la Mh Lissu linakuja likiwa limeongozana na gari la waheshimiwa wengine (Nissan nyeupe). Kwa mazoea yetu waheshimiwa hawa wabunge na wengine huwa hawapendi mlinzi wa geti asimamishe magari yao getini na kuanza kukagua waliomo ndani na kuwahoji wao ni akina nani. Kwetu tendo hilo la kudodosa waheshimiwa ni ukosefu wa nidhamu kwa mlinzi mwenye tabia kama hiyo. Kwetu nidhamu ya mlinzi ni kufungua geti mara moja anapoona gari la mheshimiwa linapokuja ili mheshimiwa na alioambatana nao waweze kuingia bila bughudha ya kufanyiwa thorough search! Ndivyo watanaznia tulivyo, tumelemazwa na amani. Kwa kutumia mwanya huo 'waheshimiwa' waliokuwa kwenye shangingi nyeupe iliyoongozana na shangingi nyeusi ya Mh Lisu waliingia kwa pamoja ndani ya eneo hilo na kusimamisha magari yao. Then in seconds mmoja wa waliokuwemo kwenye lile gari jeupe alitoka na kuanza ku spray bullets from a heavy automatic gun!! Wenye akili wanaona scnerio ilivyokuwa kihalisia na reaction ya huyo au hao walinzi wa geti la waheshimiwa kama alikuwa au walikuwa karibu na risasi zilipokuwa zinamiminwa. Reflex reaction kwa askari yo yote kwenye such a situation ni kulala chini and craw fast to a nearet cover to save his life. Hayo mambo yalitokea in seconds na hao assillants kutokomea, geti likiwa bado liko wazi na magari mengine ya waheshimiwa wabunge hayajafika kwenye eneo hilo kuja kupata chakula cha mchana.

Ni ujinga kuamini kuwa walinzi waliokuwapo eneo hilo la geti na sehemu zingine hawakuhojiwa na polisi. Pia ni upumbafu kufikiri kuwa mlinzi au walinzi waliokuwepo getini wangaliweza kujibu mapigo hayo ya risasi. Vita ya risasi si lelemama, adui yako akikuwahi unachoweza kufanya kama una bahati ni ku take cover. Pia ni ujinga kuamini kuwa kwa sababu eneo hilo linalindwa na askari basi ni salama kwa asilimia 100%. Hata kambi za jeshi na vituo vya polisi vimewahi kumiminiwa risasi na askari kuuawa mara nyingi tu, sasa sembuse hilo eneo na kwa mazingira yetu kama hayo.

Pia ni upumbafu kuamini kuwa uwepo wa CCTV kwenye eneo hilo ndiyo solution ya kuwezesha kuonekana sura za wahalifu hao. Even the most expensive high quality high definition external rotating CCTV cameras hazina uwezo wa kutoa clear images at all 360 degrees anytime and at all distances from object. When the object is more than 3m from camera huwezi pata clear images za kuweza kutambua sura za hao wahalifu. Wenye akili wanajua kwamba the effectiveness as a security tool kwa kunasa sura za wahalifu wa aina hii is almost zero. Tumeshudia huko ulaya magaidi yanavyamia na kushambulia kwa risasi kumbi za burudani na kuua watu, cctvs zao hazikuwa na msaada wa maana katika kuwatambua wahalifu hao. Hapa kwetu ambapo tulizoea madili hiyo kampuni iliyolipwa mabillion kufunga hizo CCTV kwenye eneo hilo la serikali si ajabu kuwa quality ya hizo cameras zilizofungwa ni za quality ya lugumi, hivyo aidha no images or just blurred images.

Isitoshe siku hizi ili kukwepa kuonekana sura zao kwenye ma cctv au kwa watu wengine, wahalifu wa aina hii huvaa masks au miwani myeusi + kofia zilizoshushwa chini kuficha sura zao. Mtu pekee anayejua sura za assaillants hawa pamoja na gari yao ni dereva wa Lissu. Yeye kwa maneno yake alishasema hata kabla ya hitimisho la tukio kwamba ameshawaona mara nyingi tu kuanzia Dar. Wameshawahi hata kukaa kwenye bustani moja ya hoteli fulani huko Dar na wahalifu hao wakiwa kwenye mishe mishe hiyo ya kutaka kumzuru Lissu. Bahati nzuri siku hiyo wakaweza kuwakwepa watu hao na wakatoa majigambo kwenye vyombo vya habari kwa mafanikio hayo.
Dreva wa Lissu anawafahamu vizuri sana watu hao kwa sura na hata namba ya gari lao analijua (ingawa inaweza kuwa feki). Hata walipokuwa wameficha sura zao kwa kofia pale kwenye eneo la tukio aliweza kuwatambua kuwa ni wale wale.

Sasa watu wenye akili inawawia ngumu kuelewa hicho kigugumizi cha huyo dereva kugoma kwenda kuisaidia polisi katika uchunguzi wa hilo tukio sababu yake ni nini haswa? Dereva amefichwa, huko Nairobi haonekani na huku kwetu haonekani. Mke na watoto wake ha2amuoni. Tuelewe nini sasa? Jee naye katekwa na kama katekwa ni nani huyo kamteka kama siyo chama chake. Tunaambiwa eti atasaidia tu jeshi la scotland yard la uingereza au la FBI la amerika lakini siyo jeshi hili la Siro katika uchunguzi wa tukio hili! Ni shida bin shida. Ni siasa za kupambana na serikali iliyowekwa kihalali na watanzania walio wengi!
Mkuu umeandika vitu vya mcng sana ila sifikiri kama misukule ya ufipa itakuelewa.Hoja ni kwanini huyo dereva anakingiwa kifua sana?Wanadai serikali inahusika kwanini wasije kumwaga ushahidi wao?Yani mtu yuko ladhi daily kuongea na waandishi wa habari ambao hawana hata msaada kuhakikisha uchunguz unakamilika kwa wakat na haki yake inapatikana lkn sio polisi.Hivi ni vitu vya ajabu sana na ni taifa la majuha lisiloweza kuhoji hili.
 
..kama imepita miezi 3 tangu shambulio litokee, na bado Polisi hawana majibu, basi ni vema serekali ikaomba msaada toka nchi marafiki. kila mtu angependa ukweli ujulikane na kuliko kukaa ktk hali ya kushutumiana.
Polisi walete majibu wakat dereva mmemficha huko Nairobi? Huo ni uchunguz gan wa upande mmoja?Hivi huko chadema mnafikiri kwa kutumia nn? Sababu za mcng za kumkingia kifua dereva ni zipi?Nguvu anayotumia lisu kuongea na vyombo vya hbr kwann asitumie kuhakikisha anahojiwa na polisi?Kwa akili ya darasa la saba huoni lisu na dereva wanakwepa kuhojiwa kwa sababu zisizo na mashiko?
 
..mtu yeyote yule ambaye amesumbuliwa na serekali kama ilivyotokea kwa TL, akifikwa na janga kama lile, ni lazima atahisi ni serekali ndiyo wamemtendea ubaya.

..kwa hiyo tusimlaumu sana TL. Mambo aliyoyapitia hata kabla ya kupigwa risasi, ni wachache wanaweza kuyastahimili.

..lingine ni kwamba Jeshi la Polisi lazima lichunge na kulinda heshima yake kwa weledi mkubwa.

..How do they do that? Ni kwa kutenda HAKI wakati wote, na kwa watu wote.

..Jeshi la Polisi nalo lina interest kubwa ya kujua nani ametenda unyama ule. Jaribio lile limetokea ktk eneo wanaloishi viongozi ambao wanalindwa saa zote.

..Sasa kama kumetokea shambulizi ktk eneo hilo na Polisi wameshindwa kuwakamata wahusika basi kuna tatizo ktk utendaji na weledi wa jeshi letu. Heshima yao imechafuka.

..They have to do something, and start acting like they are doing something.
HAKI INAENDA NA WAJIBU.niambie nini wajibu wa lisu na anatimiza vipi wajibu wake kuhakikisha anapata haki yake? Nini wajibu wa dereva? Mnavyoropoka ovyo kuwa polisi mara hawatimiz wajibu mara hawajawakamata washukiwa nk mnatumia vigezo gani kuwa dereva wa lisu asiye suspected? Kwann lisu asihojiwe?kwanini dereva anakingiwa kifua?Ni matokeo gani sahh mnategemea wakat huyo lisu hajahojiwa?dereva hajahojiwa?au mnamajibu yenu tayar mfukoni kias hamuoni umuhim wa hawa kuhojiwa?Acheni upumbavu.
 
Nitangulize maneno machache juu ya ujinga [ujinga siyo tusi] wangu juu ya nani alihusika na jaribio la kutaka kuondoa uhai wa Tundu Lissu. Mimi sijui kabisa nani alihusika. Lakini pia najua tofauti kati ya kujua, kuhisi, kudhani, na kusadiki. Wenye akili mtakuwa mmenipata, natumai.

Sasa bana, jana Mh. Lissu kaongea na waandishi wa habari huko Nairobi, Kenya, ambapo kimsingi kamtuhumu rais Magufuli na CCM kuhusika moja kwa moja na hilo jaribio la mauaji dhidi yake.

Upande wa serikali naona umeamua kuchukua ‘the high road’ kwa kukataa kulumbana na ‘mgonjwa’, kama ulivyosomeka ule ujumbe wa msemaji wa serikali. Nikiri tu kuwa ule ujumbe ulinichekesha sana. Ulikuwa mfupi na wenye kueleweka.

Sasa kwa vile Mh. Lissu kaamua kutoa tuhuma zake hadharani namna ile, he is now fair game!

Yeye na makamanda wenzake hawaeleweki. Hawaeleweki kwa sababu, kwa upande mmoja wanadai kuwa serikali, rais Magufuli, vyombo vya dola, na CCM ndo walihusuka na mpango mzima. Na kwa upande mwingine wanalialia kuwa eti mpaka sasa bunge halijampa haki zake, mara sijui polisi hawafanyi uchunguzi wa nani aliyetaka kumuua na blah blah zingine kama hizo.

Ni dhahiri kuwa Lissu anaingiza siasa kwenye hizo tuhuma na shutuma zake. Vivyo hivyo, huenda hata upande wa serikali nao umeamua kucheza siasa.

Now it’s on. Nasubiri tu siku Magu aje alizungumzie hilo suala. Makamanda mtalia na kusaga meno maana bwana yule mdomo wake hauna breki.

Nyie chekeleeni tu hivyo vijembe vya huyo kamanda wenu Lissu kwa sasa. Lakini siku Magu atayoamua kujibu mapigo mtatafutana.

Muwe na Jumamosi njema.
Sasa wewe mama kwani bunge ni Serikali?unaandika upuuzi tu hapa.
 
Polisi walete majibu wakat dereva mmemficha huko Nairobi? Huo ni uchunguz gan wa upande mmoja?Hivi huko chadema mnafikiri kwa kutumia nn? Sababu za mcng za kumkingia kifua dereva ni zipi?Nguvu anayotumia lisu kuongea na vyombo vya hbr kwann asitumie kuhakikisha anahojiwa na polisi?Kwa akili ya darasa la saba huoni lisu na dereva wanakwepa kuhojiwa kwa sababu zisizo na mashiko?
Daaah simply as this! Kwa hiyo huyo dereva ndie aliyempiga risasi Bosi wake? So so cheap reasoning capacity! I dont have any political party Affiliation but for this is completely trash! Revisit and come again with tangible aspects
 
Utaahira huthibitika kwa hoja za mja. Issue sio za nani, issue ni JE ANA HAKI YA KUTIBIWA NAZO?
Mtanzania ye yote hata kama ni mlala hoi kiasi gani ana haki sawa ya kutibiwa na hizo pesa ndani au nje ya nchi hii. Si sawa hata kidogo kwamba ni wabunge na vigogo tu ndizo fedha hizi zimetengwa kwa ajili yao. Watanzania wote wana haki sawa kutibiwa nje ya nchi kwa fedha hizi. Ili mtanzania ye yote bila kujali cheo chake aweze kupata haki hii ya kutibiwa nje ya nchi kuna utaratibu wa kisheria wa kufuata (regulation). Ni lazima jopo la madaktari bingwa kutoka kwenye hospitalu yetu ya Taifa wawe wamethibitisha kuwa maradhi ya mhusika nchi yetu haina uwezo wa kuyatibu na kwamba matibabu yanayopatikana nje ya nchi yatakuwa na manufaa kwa mgonjwa husika.

Shida inakuja pale wanasiasa wanapolazimisha kupelekwa kutibiwa nje ya nchi hata pale matibabu hayo hayo yanapatikana hapa hapa kwa quality ile ile. Au wanalazimisha kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu ya ugonjwa ambao hautibiki sehemu yo yote dunia hii. Wanaamini kuwa magonjwa yote yanatibika na kupona, kitu ambacho si kweli. Lazima watu wafe kwa magonjwa au kwa ajali. Lazima wengine wapate ulemavu wa kudumu kutokana na ajali au mashambulio kama ya risasi. Huwezi kukwepa hata uende ulaya. Science ni ile ile, uwe ulaya au Afrika.
 
HAKI INAENDA NA WAJIBU.niambie nini wajibu wa lisu na anatimiza vipi wajibu wake kuhakikisha anapata haki yake? Nini wajibu wa dereva? Mnavyoropoka ovyo kuwa polisi mara hawatimiz wajibu mara hawajawakamata washukiwa nk mnatumia vigezo gani kuwa dereva wa lisu asiye suspected? Kwann lisu asihojiwe?kwanini dereva anakingiwa kifua?Ni matokeo gani sahh mnategemea wakat huyo lisu hajahojiwa?dereva hajahojiwa?au mnamajibu yenu tayar mfukoni kias hamuoni umuhim wa hawa kuhojiwa?Acheni upumbavu.

..unajirudia rudia tu.

..Utaratibu ni Mwanasheria Mkuu wa Tanzania kumuandikia barua Mwanasheria Mkuu wa Kenya ili Tundu na dereva wahojiwe na Polisi wa Kenya.

..Hivyo ndivyo sheria ya Tanzania inavyoelekeza.

..Sasa serekali[Mwanasheria Mkuu + IGP] ya Tanzania ina kisingizio gani cha kutoomba ruhusa inakaribia miezi 4 tangu TL ashambuliwe?
 
Back
Top Bottom