Aliyefungwa kwa baraghashia yu huru

yuko huru kwa sababu mahakama kuu iliona kuwa ulikuwa si uamuzi sahihi lakini wengine ndio wanaona mahakama kuu imeamua tu vile kwa sababu ya shinikizo la waaislam

labda wos anaweza kutusaidia ..............jee kuna sheria ya maandishi inayokataza kofia mahakamani?
Kwa kweli Gaijin sijakutana na legislation hii ila huenda ipo Ila as a rule of practice mahakamani kuna miiko yake ikiwemo huu utaratibu wa kuvua kofia, kusimama pale hakimu au jaji anapoingia au kutoka na pia kukaa kimya bila kupiga kelele ya aina yoyote ile karibu na eneo la mahakama. Kuna hakimu aliwahi kumfunga mtu kwa masaa machache kwa kupiga honi eneo la mahakama, kuna mtu aliwahi kuhukumiwa faini kwa kosa la kuonyesha dharau mahakamani ( contempt of court)..na hata hili la baraghashia utaona ni along same lines - contempt of court ila adhabu was manifestly excessive.
 
WOS, umejitakia mwenyewe... mwenzio huyo ana agenda yake na wala si haki ya huyo aliyefungwa, yeye kaja hapa na politikal agenda lile jukwaa lao limedoda siku hizi
Kwani Acid, tunapaswa kuwaogopa watu tuonapo kuna upotoshaji?
Hapo juu kuna mtu amenibeza kuwa hoja yangu haina substance kwa vile sikuonyesha kumkandamiza mvaa baraghashia! Hii haifai hata kidogo.
 
Nijuavyo hata kwenye western world, ukiingia mahakamani unakuta imeandikwa uvue kofia na pia ni common understanding miongoni mwa watu kwa sababu imo katika culture yao moja kwa moja.

tukija Tanzania, kwanza hakuna anaejua kuwa kuingia na kofia mahakamani ni kosa kwa sababu kwetu kofia haina maana ya ukosefu wa nidhamu na kwa baadhi ya watu ina maana ya heshima ( kama mtu anajiona anaivaa mbele ya mungu, hawezi kudhani kuwa ni ukosefu wa heshima kuivaa mbele ya binaadamu)

bila ya shaka kutokujua sheria hakuna maana ya kuwa hujavunja sheria, lakini kutokana na kukosekana sheria ya moja kwa moja inayokataza mtu kuvaa kofia mahakamani ndio kulikopelekea mahakama kuu kufuta uamuzi wa hakimu wa mwanzo. Alitakiwa hakimu atumie logic zaidi madhali sheria haijaandikwa wazi
 
Kwa vile jamii yetu ni ya watu wenye imani mbalimbali, basi ni vyema angalau kuwe na sheria (kama haipo) inayoruhusu watu kuvaa head garments hususan kwa sababu za kidini.

Sioni ubaya wowote mtu kuvaa baraghashia mahakamani ili mradi kavaa kinadhifu kwenye mavazi mengine. Kwenye jurisdictions kibao Marekani (nchi iliyoanzishwa kwenye misingi ya Judeo-Christian) wanaruhusu kuvaa head wear kwa misingi ya kidini na kiutamaduni ingawa kwa kiasi kikubwa mahakimu wanakuwa wanapewa discretion ya kuruhusu au kutokuruhusu.

Sijui kwa mahakama zetu Tanzania lakini ingekuwa vizuri kama wangebandika dress code mbele kwenye mlango mkuu wa kuingilia watu. It's as simple as that.

Pia ni bora mtu uvae conservatively unapoenda mahakamani. Usitake kushindwa kesi yako kwa sababu huku create good first impression.....
 
Ukweli ni kwamba huu ni moto ambao hakimu Luhwago aliuwasha bila ya kuangalia wakati. Kuelekea kipindi hiki cha uchaguzi serikali kamwe isingeweza kuhatarisha kura nyingi kutokana na maamuzi kama haya ambayo ni tata na ambayo yalishashupaliwa na umati.

Ukweli ni kwamba kutokana na maelezo ya kesi yenyewe, hakimu alikuwa yu sahihi kumwadabisha ndugu Sururu kwa kukaidi amri yake ya awali ya kuvua baraghashia. Tatizo linakuja katika usahihi wa hakimu kumtaka ndugu Sururu avue baraghashia
 
mmh! kweli nchi hii ina vituko,sasa inamaana huyo jaji yupo juu au hajui sheria? na kwanini wasubiri Tamko?, tutaaminije kama kweli uamuzi huo ni wa kisheria au si kwasabaubu ya shinikizo la BAKWATA?mbona uamuzi umetolewa haraka sana, maana mi nijuavyo mahakama zetu huchelewesha sana kesi muda.kwa jumla mi naona uamuzi huu umetokana na shinikino, itz too degerous
 
Waislamu wanapenda sana tunavyopoteza muda kujadili upuuzi kama huu..........mtu kadharau mahakama mwislamu au mkristo piga ndani hiyo ndiyo haki na yamefanyka kwa wakristo kwa nini waislamu ndiko sheria zote haziwezi kufanya kazi?.........waislamu waliweza hata kulifanya bunge kupoteza muda likijadili mahakama ya kadhi kwa faida ya waislamu na wakilipwa posho
 
mahakama ya kadhi takuhusu wewe au itawahusu waislamu! ..
 
Mkuu hivi unaakili wewe ama? Nimesema nitaka rufaa wa baragashia arudi jela hiyo orodha umeitoa Madrasa

Kubishana na wajinga ni kupoteza muda.
Ninaanza kuwa na wasiwasi kwamba CCM sasa ni chama cha kidini kwa sababu washabiki wake wakubwa hapa JF ni wadini (waislamu zaidi) sana na hawaleti hoja za maana badala yake ama wanasifia tu ccm au wanataka kutugawa kupitia dini zetu
 
Bernard James

Jaji Kiongozi Fakihi Jundu jana aliliambia Mananchi Jumapili mahakama iliamuru kuchiliwa kwa mzee Sururu baada ya kuridhika hapakuwa na sababu za kutosha kisheria kutoa hukumu hiyo.

“Muda mfupi baada ya kusomwa hukumu hiyo maofisa wangu walinipa taarifa na kuchukua hatua ya kuitisha faili la kesi. Jana majira ya saa kumi jioni ofisa wa mahakama alikuwepo gerezani kuhakikisha Bwana Sururu anaachiwa huru na kuungana na familia yake,” alisema jaji kiongozi.

Aliongeza: “Wakati Bakwata (Baraza Kuu la Kiislamu Tanzania) wanahoji uhalali wa hukumu hiyo tayari tulikwishachukua hatuai. Hatukusubiri kusukumwa na mtu yeyote. Sisi tulihisi tatizo katika hukumu hiyo na kuchukua hatua mara moja”.


Chanzo: Wavuti ya Mwananchi

Tanzania ingekuwa nchi nzuri kweli kama itokeapo mwananchi yeyote kutokutendewa haki na mahakama za chini Jaji kiongozi angechukua hatua za haraka jinsi hii.
 
waislamu kitabu chetu kina sheria zetu! ambazo baadhi ukizikiuka ni dhambi kubwa saana! ndio maana tunataka mahakama ya kadhi.! kwa ajili yetu TU! mfano katika swala zima la mirathi ... dini yetu imeweka wazi nani apate nini.. hatutaki sheria zenu za wamisionari ..:becky:

 
Hivi Mh Lyatonga mrema pamooja na kesiz ake zote alikuwa/anavua ile barghashia yake akiingia mahakamani?:confused2:
 
Back
Top Bottom