Binadamu tunatofautiana sana katika kila jambo. Uwezo wa kufikiri wa mwenzako ni tofauti na wako lakini katika utawala kupatia na kukosea kunapimwa kwa faida na hasara kwa kuangalia walau zile tunu za Taifa.
Kwa maoni yangu Rais Magufuli alianza vyema sana lakini kwa maoni yangu vile vile safari ilipoteza mwelekeo na anazidi kukosea.
Kushindwa kuongoza kwa check and balance:
Hili ni eneo moja muhimu. Alishindwa kusimamia hoja zile zile alizoziamini kwa maamuzi yote( rejea alivyotumbuwa baadhi ya watendaji na sababu zake na kushindwa kulisimamia suali la vyeti feki kwa baadhi ya watendaji.
Kutovumilia baadhi ya mambo yanayovumilika:
Hakukuwa na sababu yoyote kwa mnasaba wa kitaifa kudhibiti vyombo vya habari na mawazo huru kwa kiasi hiki kiichopo ikizingatiwa utamaduni huu ulishazoeleka kwa nchi ya kidemokrasia kama Tanzania. Hatimae analaumiwa na analaumika.
Kujitenga na wanasiasa wenzake wa upinzani:
Hili ni kosa kubwa katika demokrasia na utawala . Watawala wanatakiwa kuwa na ajenda ya kudumu ya siasa za kirafiki ikizingatiwa kuwa vyama vingi ni kupokezana vijiti. Ukianza kulumbana na wanasiasa wenzako ujuwe unakaribisha ukinzani wa wazi na ni rahisi kutolewa kwenye ajenda za maendeleo. Tujiulize leo Rais Magufuli ana ajenda gani Constructive ? Hakuna ajenda ya kitaifa inayowakutanisha wanasiaa wote zaidi ya chuki na kulumbana kila mmoja akitaka kumuonesha mwenzake.
Kushindwa kudhibiti matumizi ya Lugha:
Lugha ndio kila kitu. Maneno mengine yakitamkwa na kiongozi mkuu wa nchi yanamshushia heshima mwenyewe. Kuna maneno yanaudhi hata kutamkwa hapa kwenye uzi. Labda ni uanagezi au ni kukosa uelewa wa siasa za majukwaani.
Kushindwa kujibaini:
Hili ndilo kosa kubwa zaidi kuliko yote. Unaweza ukakosea na kujirudi. Rais wetu bado hajabaini kuwa kadiri akizidisha mbinyo kwa yale anayoamini yako sawa kumbe ndio Taifa linazidi kugawanyika. Kwa mfano, ile point ya check and balance inakuwaje wateule wake wavunje sheria za wazi halafu ashindwe kuwachukulia hatua? Uvamizi wa clouds, maagizo ya kuvunja sheria yanayofanywa na wakuu wa mikoa n. k. ni mifano ya wazi.
Kutotekeleza ahadi za wazi:
Hakukuwa na ulazima wa kujifunga kwa kauli za nyongeza za mishahara na madaraja kwa kutaja muda wakati huna uhakika. Hata muda wa kuja kwa bombadier hakukustahili kuwekwa ahadi kwa level ya rais. Hatimae anakosa kuaminika hata kama ana nia nzuri.
Diplomasia kwatu:
Diplomasia inayumba kidogo na kuitia mashaka nchi. Unaanza kuingia madarakani unajiondoa kwenye mikataba ya uwazi ya kidunia. Unatoa lugha za kibabe na kuchukuwa hatua ambazo zingefaa kupunguzwa makali. Unaongeza migogoro na mataifa na makampuni ambayo yanaathiri uchumi bila ya kufanywa analysis ya faida na hasara. Faida si wingi wa rasilimali tu hata vile kuwa neutral kidiplomasia hio ni faida kubwa. Kuna maeneo mengine mengi tu n.k.
MWISHO
HASARA: Nadhani kuna hasara nyingi kutokana na mnasaba wa kukosewa huko, miongoni mwao ni
i. Kulega lega kwa mshikamano wa kitaifa
ii. Kukosekana umoja na kutoaminiana.
iii. Kutolewa fursa za uhalifu kwa watu wenye nia mbaya na Tanzania.
iv. Kuyumba kwa usalama wetu na kuzidi hofu na migawanyiko.
v. Kukosekana utulivu wa kufocus maendeleo badala yake minyukano inazidi na kupotezeana muda. n,k.
Nini kifanyike?
Turudi kwenye misingi yetu, Urais ni kuvumilia na kukubali kukosolewa, Rais Magufuli kuna maeneo anapatia na mengine anakosea.
Kwangu mimi makosa ni mengi kuliko mafanikio. Makosa yanahatarisha umoja wetu wa kitaifa ambayo ni tunu kuu kuliko yote.
Tusisahau KATIBA MPYA
Kishada.