Alipokosea Rais Magufuli na anavyoendelea kukosea

Alipokosea Rais Magufuli na anavyoendelea kukosea

KISHADA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
2,226
Reaction score
3,293
Binadamu tunatofautiana sana katika kila jambo. Uwezo wa kufikiri wa mwenzako ni tofauti na wako lakini katika utawala kupatia na kukosea kunapimwa kwa faida na hasara kwa kuangalia walau zile tunu za Taifa.

Kwa maoni yangu Rais Magufuli alianza vyema sana lakini kwa maoni yangu vile vile safari ilipoteza mwelekeo na anazidi kukosea.

Kushindwa kuongoza kwa check and balance:
Hili ni eneo moja muhimu. Alishindwa kusimamia hoja zile zile alizoziamini kwa maamuzi yote( rejea alivyotumbuwa baadhi ya watendaji na sababu zake na kushindwa kulisimamia suali la vyeti feki kwa baadhi ya watendaji.

Kutovumilia baadhi ya mambo yanayovumilika:
Hakukuwa na sababu yoyote kwa mnasaba wa kitaifa kudhibiti vyombo vya habari na mawazo huru kwa kiasi hiki kiichopo ikizingatiwa utamaduni huu ulishazoeleka kwa nchi ya kidemokrasia kama Tanzania. Hatimae analaumiwa na analaumika.

Kujitenga na wanasiasa wenzake wa upinzani:
Hili ni kosa kubwa katika demokrasia na utawala . Watawala wanatakiwa kuwa na ajenda ya kudumu ya siasa za kirafiki ikizingatiwa kuwa vyama vingi ni kupokezana vijiti. Ukianza kulumbana na wanasiasa wenzako ujuwe unakaribisha ukinzani wa wazi na ni rahisi kutolewa kwenye ajenda za maendeleo. Tujiulize leo Rais Magufuli ana ajenda gani Constructive ? Hakuna ajenda ya kitaifa inayowakutanisha wanasiaa wote zaidi ya chuki na kulumbana kila mmoja akitaka kumuonesha mwenzake.

Kushindwa kudhibiti matumizi ya Lugha:
Lugha ndio kila kitu. Maneno mengine yakitamkwa na kiongozi mkuu wa nchi yanamshushia heshima mwenyewe. Kuna maneno yanaudhi hata kutamkwa hapa kwenye uzi. Labda ni uanagezi au ni kukosa uelewa wa siasa za majukwaani.

Kushindwa kujibaini:
Hili ndilo kosa kubwa zaidi kuliko yote. Unaweza ukakosea na kujirudi. Rais wetu bado hajabaini kuwa kadiri akizidisha mbinyo kwa yale anayoamini yako sawa kumbe ndio Taifa linazidi kugawanyika. Kwa mfano, ile point ya check and balance inakuwaje wateule wake wavunje sheria za wazi halafu ashindwe kuwachukulia hatua? Uvamizi wa clouds, maagizo ya kuvunja sheria yanayofanywa na wakuu wa mikoa n. k. ni mifano ya wazi.

Kutotekeleza ahadi za wazi:
Hakukuwa na ulazima wa kujifunga kwa kauli za nyongeza za mishahara na madaraja kwa kutaja muda wakati huna uhakika. Hata muda wa kuja kwa bombadier hakukustahili kuwekwa ahadi kwa level ya rais. Hatimae anakosa kuaminika hata kama ana nia nzuri.

Diplomasia kwatu:
Diplomasia inayumba kidogo na kuitia mashaka nchi. Unaanza kuingia madarakani unajiondoa kwenye mikataba ya uwazi ya kidunia. Unatoa lugha za kibabe na kuchukuwa hatua ambazo zingefaa kupunguzwa makali. Unaongeza migogoro na mataifa na makampuni ambayo yanaathiri uchumi bila ya kufanywa analysis ya faida na hasara. Faida si wingi wa rasilimali tu hata vile kuwa neutral kidiplomasia hio ni faida kubwa. Kuna maeneo mengine mengi tu n.k.

MWISHO

HASARA: Nadhani kuna hasara nyingi kutokana na mnasaba wa kukosewa huko, miongoni mwao ni
i. Kulega lega kwa mshikamano wa kitaifa
ii. Kukosekana umoja na kutoaminiana.
iii. Kutolewa fursa za uhalifu kwa watu wenye nia mbaya na Tanzania.
iv. Kuyumba kwa usalama wetu na kuzidi hofu na migawanyiko.
v. Kukosekana utulivu wa kufocus maendeleo badala yake minyukano inazidi na kupotezeana muda. n,k.

Nini kifanyike?

Turudi kwenye misingi yetu, Urais ni kuvumilia na kukubali kukosolewa, Rais Magufuli kuna maeneo anapatia na mengine anakosea.

Kwangu mimi makosa ni mengi kuliko mafanikio. Makosa yanahatarisha umoja wetu wa kitaifa ambayo ni tunu kuu kuliko yote.

Tusisahau KATIBA MPYA


Kishada.
 
Mimi naona wapinzani ndiyo walikuwa wa kwanza kumbagua yeye kamalizia tu!
Tuliona walivyomkimbia bungeni mara ya kwanza

Tunaona wanavyopenda ashindwe kwenye uongozi wake utafikiri wao ni wapita njia!
Mawazo kuwa anaferi hayo ni maoni yako

Kikubwa sisi tunataka maendeleo ,mambo yenu ya demokrasia wapelekee wazungu!
 
Namshauri aongeze spidi ya kuwabana vilivyo ili tuondokane na upuuzi...Taifa lilibaki nyuma kwa hayo mnayoyaita checks and balance
....miradi ya maendeleo ilikuwa haiendi na fedha zinaliwa tu
 
!
!
Anataka kufanya kila kitu matokeo yake hafanyi lolote.
Anaamini anajua kila kitu ambacho kiko mbali na ukweli.
H
 
Sasa mnavyomsema hivi kwenye mitandao ndo anazidi kufanya madudu,kibaya zaidi yeye anaona yupo sawa kabisa
 
Mimi naona wapinzani ndiyo walikuwa wa kwanza kumbagua yeye kamalizia tu!
Tuliona walivyomkimbia bungeni mara ya kwanza
Tunaona wanavyopenda ashindwe kwenye uongozi wake utafikiri wao ni wapita njia!
Mawazo kuwa anaferi hayo ni maoni yako
Kikubwa sisi tunataka maendeleo ,mambo yenu ya demokrasia wapelekee wazungu!

Hakuna maendeleo hapo. Kuna uwoga na ubabaishaji kwa ajili ya kuficha huo uoga. Misingi ya nchi inatikiswa na heshima ya Tanzania iko majaribuni.
 
Natamani rais wetu angeendelea na ule utamaduni wa utani aliokuwa nao kwa wanasiasa wenzake ili maisha yaende.

Natamani angewashirikisha wenzake kwenye ishu za kitaifa

Natamani angekuwa mfano wa kutoa hutuba za kuwaunganisha watu sasa kuliko jana

Natamani angebadili siasa na kurejesha upendo ule tuliouzowea
 
Mimi naona wapinzani ndiyo walikuwa wa kwanza kumbagua yeye kamalizia tu!
Tuliona walivyomkimbia bungeni mara ya kwanza
Tunaona wanavyopenda ashindwe kwenye uongozi wake utafikiri wao ni wapita njia!
Mawazo kuwa anaferi hayo ni maoni yako
Kikubwa sisi tunataka maendeleo ,mambo yenu ya demokrasia wapelekee wazungu!

Duh this comment comes from sound or unsound mind

Tz bado has a long way to go
 
1.Rais ni mwongo maana aliongea tarehe 14/10/2017 kuwa kuna Watumishi wa Umma 59,000+ watapandishwa madaraja mwezi Novemba lakini hadi sasa hajapanda hata mmoja.

2.Rais alisema baada ya uhakiki kumalizika kutakuwa na maslahi bora kwa Watumishi wa Umma lakini hadi sasa wamepewa za uso.

Waandishi wa habari hizi hazifai kupamba kwenye front page maana sijawahi kuziona.

Kutoka hifadhi ya misitu ya Madihani
Mwanachama wa CCM.
 
Natamani nimuone mh Rais akiwa ameshikana mikono na Mbowe kwenye sherehe za kitaifa

Natamani aanzishe debaTE YA KITAIFA YA uTENGAMANO NA AJUTIE HALI ILIYOPO.

Natamani atoe hutuba kuwa yalioyopita yamepita na aanze upya kupigania Uzalendo shirikishi baada ya debate kubaini tulipokosea.
 
Hapa hatutaki Ukereketwa. Wengine tunaandika haya kwa huzuni sana. Yaani tunahisi Rais wetu kakosa kuitumia fursa vizuri. Alianza vyema sana lakini alipotea muda mchache sana baada ya safari.

Leo hii huyu angekuwa championi wa umoja na utengamano

Uzalendo shirikishi, jemedari wa haki, usawa na Maendeleo

Lakini bahati mbaya sasa Tanzania kumejaa visasi na chuki, Dhulma na watu kupotea kwa nini ?
 
Kuna wakati nilimuona Rais Magufuli kama tunu na zawadi. Niliogopa niiposikia zile kauli zake tata na vitisho. Tukashuhudia uwoga wa watendaji kutumbuliwa hadharani. Weledi ukaanza KUSHUKA KWA WATENDAJI KUOGOPA MASUALI HADHARANI

Nikajiuliza kwa nini Mh Rais asijipe muda wa kutafakari ili atafute dawa vizuri lakini kuchwa kucha ilikuwa ni kutumbuwa tena bila staha.

Maskini kuna wazee wa watu wameumwa presha na wengine walifariki kwa vihoro .

Mungu awerehemu sana.
 
Mimi naona wapinzani ndiyo walikuwa wa kwanza kumbagua yeye kamalizia tu!
Tuliona walivyomkimbia bungeni mara ya kwanza
Tunaona wanavyopenda ashindwe kwenye uongozi wake utafikiri wao ni wapita njia!
Mawazo kuwa anaferi hayo ni maoni yako
Kikubwa sisi tunataka maendeleo ,mambo yenu ya demokrasia wapelekee wazungu!


Safi sana, wapeleke marekani na ujerumani. Kakosea, kakosea tu! ina maana hamna hata alipopatia hii ni ajabu sana. Ok, nafikiri hii ndio check and balance
 
Back
Top Bottom