Zero Hours
JF-Expert Member
- Apr 1, 2011
- 12,942
- 18,693
Mnapoteza muda kumkosoa Magufuli. Akimwaga mboga nwageni ugali bhna. Mnakuwa mazuzu mno
We jamaa nimekudharau sana ! Una hoja dhaifu zisizo na mashiko yoyote ! Kama na wewe unalipwa na ccm kwa kuandika hapa basi hela za ccm zitakuwa zinaliwa kijinga sana !KISHADA Kishada umeandika sana but hivi nikweli haya umeandika yana reflect kile kinafanyika na hapa ndipo watanzania tunakosea sana
Na dalili zinaonyesha hataki kutoka madarakaniNchi ishamshinda huyo,alifikiri kuongoza nchi ni kama kumuongoza mkewe na wanawe ..
leo unapiga makofi huyu kesho huleti mboga nyumbani ilmradi unaitwa baba basi tafrani tu
Chombo chaenda mrama atakaye kirudisha sijui ni nani
Nafikiri hili ni kubwa. Sijui kwa nini wengine wanafungwa!Kushindwa kudhibiti matumizi ya Lugha:
Lugha ndio kila kitu. Maneno mengine yakitamkwa na kiongozi mkuu wa nchi yanamshushia heshima mwenyewe. Kuna maneno yanaudhi hata kutamkwa hapa kwenye uzi. Labda ni uanagezi au ni kukosa uelewa wa siasa za majukwaani.
Hata asipotoka leo wala kesho ,ataishi milele ? Kiburi cha mwanadamu mwisho wake ni futi sita ardhini .Na dalili zinaonyesha hataki kutoka madarakani
Unajua maana na umuhimu wa check and balance?Namshauri aongeze spidi ya kuwabana vilivyo ili tuondokane na upuuzi...Taifa lilibaki nyuma kwa hayo mnayoyaita checks and balance
....miradi ya maendeleo ilikuwa haiendi na fedha zinaliwa tu
Na kweli ameshindwa ameshatoka kwenye agenda ya maendeleo amekalia udaku na shilawadu, nani kasema nini na kamsema nini so shakable hana msimamo.Mimi naona wapinzani ndiyo walikuwa wa kwanza kumbagua yeye kamalizia tu!
Tuliona walivyomkimbia bungeni mara ya kwanza
Tunaona wanavyopenda ashindwe kwenye uongozi wake utafikiri wao ni wapita njia!
Mawazo kuwa anaferi hayo ni maoni yako
Kikubwa sisi tunataka maendeleo ,mambo yenu ya demokrasia wapelekee wazungu!
Hizi nchi unazozitaja, ziliharibiwa na viongozi wao waliojiona mamiungu watu, wasiokosea, wasiojuwa democracy ya kuchagua na kuchaguliwa kwa wengine. Lazima nchi ikusambaratikie na hicho ndicho kinachoikabili Tanzania baada ya Maghufuli !!!!. Libya, Zaire, Gambia, na sasa Uganda na Rwanda ni tatizo la viongozi kujiona wao ndio wao. Na nchi haikupata kuwa na wengine.Toa na mfano wa Libya uchumi ulikuwaje kabla ya hiyo demokrasia yenu bandia ya wazungu !
Congo /Zaire imeharibiwa na demokrasia ya ki Africa?
Au wazungu wanoiba utajiri wa Congo!
We are African ,tujitambue siyo kila kitu kuiga
Mkuu hujuwi kuwa democrasia na Maendeleo yanakwenda sambambaMimi naona wapinzani ndiyo walikuwa wa kwanza kumbagua yeye kamalizia tu!
Tuliona walivyomkimbia bungeni mara ya kwanza
Tunaona wanavyopenda ashindwe kwenye uongozi wake utafikiri wao ni wapita njia!
Mawazo kuwa anaferi hayo ni maoni yako
Kikubwa sisi tunataka maendeleo ,mambo yenu ya demokrasia wapelekee wazungu!
Mbona mawaziri mapolisi makatibu wakuu na watoto wao hawapoteiNilitamani mpaka hatua hii iwe amekemea kupotea kwa watu. Halafu Magufuli nimjuwae mimi aendelee kuambiwa kuwa mauaji yanafanywa na " WATU WASIOIJULIKANA " halafu iwe yupo yupo tu hata kukemea ?
Binadamu tunatofautiana sana katika kila jambo. Uwezo wa kufikiri wa mwenzako ni tofauti na wako lakini katika utawala kupatia na kukosea kunapimwa kwa faida na hasara kwa kuangalia walau zile tunu za Taifa.
Kwa maoni yangu Rais Magufuli alianza vyema sana lakini kwa maoni yangu vile vile safari ilipoteza mwelekeo na anazidi kukosea.
Kushindwa kuongoza kwa check and balance:
Hili ni eneo moja muhimu. Alishindwa kusimamia hoja zile zile alizoziamini kwa maamuzi yote( rejea alivyotumbuwa baadhi ya watendaji na sababu zake na kushindwa kulisimamia suali la vyeti feki kwa baadhi ya watendaji.
Kutovumilia baadhi ya mambo yanayovumilika:
Hakukuwa na sababu yoyote kwa mnasaba wa kitaifa kudhibiti vyombo vya habari na mawazo huru kwa kiasi hiki kiichopo ikizingatiwa utamaduni huu ulishazoeleka kwa nchi ya kidemokrasia kama Tanzania. Hatimae analaumiwa na analaumika.
Kujitenga na wanasiasa wenzake wa upinzani:
Hili ni kosa kubwa katika demokrasia na utawala . Watawala wanatakiwa kuwa na ajenda ya kudumu ya siasa za kirafiki ikizingatiwa kuwa vyama vingi ni kupokezana vijiti. Ukianza kulumbana na wanasiasa wenzako ujuwe unakaribisha ukinzani wa wazi na ni rahisi kutolewa kwenye ajenda za maendeleo. Tujiulize leo Rais Magufuli ana ajenda gani Constructive ? Hakuna ajenda ya kitaifa inayowakutanisha wanasiaa wote zaidi ya chuki na kulumbana kila mmoja akitaka kumuonesha mwenzake.
Kushindwa kudhibiti matumizi ya Lugha:
Lugha ndio kila kitu. Maneno mengine yakitamkwa na kiongozi mkuu wa nchi yanamshushia heshima mwenyewe. Kuna maneno yanaudhi hata kutamkwa hapa kwenye uzi. Labda ni uanagezi au ni kukosa uelewa wa siasa za majukwaani.
Kushindwa kujibaini:
Hili ndilo kosa kubwa zaidi kuliko yote. Unaweza ukakosea na kujirudi. Rais wetu bado hajabaini kuwa kadiri akizidisha mbinyo kwa yale anayoamini yako sawa kumbe ndio Taifa linazidi kugawanyika. Kwa mfano, ile point ya check and balance inakuwaje wateule wake wavunje sheria za wazi halafu ashindwe kuwachukulia hatua? Uvamizi wa clouds, maagizo ya kuvunja sheria yanayofanywa na wakuu wa mikoa n. k. ni mifano ya wazi.
Kutotekeleza ahadi za wazi:
Hakukuwa na ulazima wa kujifunga kwa kauli za nyongeza za mishahara na madaraja kwa kutaja muda wakati huna uhakika. Hata muda wa kuja kwa bombadier hakukustahili kuwekwa ahadi kwa level ya rais. Hatimae anakosa kuaminika hata kama ana nia nzuri.
Diplomasia kwatu:
Diplomasia inayumba kidogo na kuitia mashaka nchi. Unaanza kuingia madarakani unajiondoa kwenye mikataba ya uwazi ya kidunia. Unatoa lugha za kibabe na kuchukuwa hatua ambazo zingefaa kupunguzwa makali. Unaongeza migogoro na mataifa na makampuni ambayo yanaathiri uchumi bila ya kufanywa analysis ya faida na hasara. Faida si wingi wa rasilimali tu hata vile kuwa neutral kidiplomasia hio ni faida kubwa. Kuna maeneo mengine mengi tu n.k.
MWISHO
HASARA: Nadhani kuna hasara nyingi kutokana na mnasaba wa kukosewa huko, miongoni mwao ni
i. Kulega lega kwa mshikamano wa kitaifa
ii. Kukosekana umoja na kutoaminiana.
iii. Kutolewa fursa za uhalifu kwa watu wenye nia mbaya na Tanzania.
iv. Kuyumba kwa usalama wetu na kuzidi hofu na migawanyiko.
v. Kukosekana utulivu wa kufocus maendeleo badala yake minyukano inazidi na kupotezeana muda. n,k.
Nini kifanyike?
Turudi kwenye misingi yetu, Urais ni kuvumilia na kukubali kukosolewa, Rais Magufuli kuna maeneo anapatia na mengine anakosea.
Kwangu mimi makosa ni mengi kuliko mafanikio. Makosa yanahatarisha umoja wetu wa kitaifa ambayo ni tunu kuu kuliko yote.
Tusisahau KATIBA MPYA
Kishada.
Kama alivyo mtoa post,kana kwamba yupo sahihi asilimia 100,akaze tu had tuzijue sura zenu$%£¥₩Sasa mnavyomsema hivi kwenye mitandao ndo anazidi kufanya madudu,kibaya zaidi yeye anaona yupo sawa kabisa
Nasikia yupo mbioni kumtumbua Sirro