Fanya kazi yako kisomi zaidi.Fuata sheria na uwe tofauti na boda wote.Jitahidi wekeza upate boda yako mwenyewe halafu itumie hiyo kuandikia proposal upate mkopo benki ili upate boda nyingine.Ajiri kijana kadiri siku zinavyoenda fungua kampuni ya boda boda ajiri vijana wengi zaidi.Hakikisha unaaminika na watu wenye maduka makubwa au watoa huduma uwe unatoa deliveries.Weka matangazo ya kampuni yako na namba za simu watu wakupigie popote wanapohitaji usafiri na utoe huduma kwa uaminifu.Nilimaliza chuo kikuu mwaka 2019 kule UDOM na sasa nipo kitaa bila kazi maalum.
Kuna jamaa mmoja yeye ni mjumbe wa nyumba kumi ni kabila moja na mimi akaja akaniambia nianze kuendesha bodaboda ili nipate pesa ya kujikimu.
Nilianza kuendesha bodaboda mwaka jana 2020 nikawa napata pesa za vocha ila jambo la kushangaza jamaa anaanza kuwaambia watu kuwa "mnamuona mwita amesoma sana mpaka chuo kikuu lakini ameishia kuwa dereva wa bodaboda kama vijana walioishia darasa la saba tu".
Sasa sijui nimfanyeje mtu huyu?
Baadaye huyo bwana atakuheshimu.